Last week niliongelea umuhimu wa chanjo, sina haja ya kurudia leo (kama hujui bofya kibufe cha AFYA hapo juu utaona) ila swali ni; mama na baba mtarajiwa hivi mnajua mlolongo wa chanjo atakazo zipitia mwanenu kabla ya kufikishwa mwaka mmoja. Yaani atadungwa sindano kabla ya kujua kusema tata… unajua lini anatakiwa apate chanjo hizo? Unajua hizo chanjo zinazuia nini?
Bofya palipoandikwa ZAIDI BOFYA HAPA » upate ratiba nzima ya chanjo za muhimu na zinachozuia.
Ratiba ya chanjo kwa watoto wa umri chini ya mwaka mmoja:
Umri
|
Aina ya Chanjo
|
Ugonjwa Unaozuia
|
Sehemu Inapotolewa
|
Kuzaliwa
|
Kifua kikuu (BCG)
Polio
|
Kifua kikuu
Kupooza
|
Bega la kulia
Mdomoni
|
Wiki ya 6
|
Polio 1
Pentavalent
|
Kupooza
Dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa
mgongo na kichomi
|
Mdomoni
Paja la kushoto
|
Wiki ya 10
|
Polio 2
Pentavalent
|
Kupooza
Dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa
mgongo na kichomi
|
Mdomoni
Paja la kushoto
|
Wiki ya 14
|
Polio 3
Pentavalent 3 (Dtp – hep b – hib)
|
Kupooza
Dondakoo, pepopunda, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa
mgongo na kichomi
|
Mdomoni
Paja la kushoto
|
Akikamilisha miezi
9
|
Surua
|
Surua
|
Paja la kulia
|
Hii nimeitoa hospitali flani hivi, ilikua imebandikwa kama tangazo kutoka wizara ya afya. According to the tangazo, chanjo hizi zote ni salama na ni bure kwenye hospitali zote, private na public. Ingawa nimekopi kadri ya uwezo wangu mnisamehe kama nimekosea spelling za medical terms, maana mie sio dokta, but I hope nimesaidia wazazi wenzangu kupata general knowledge kuhusu hizo chanjo.
3 comments:
ahsante sana dada kwa habari. wazazi na tuzingatie chanjo hizi kwani muhimu saana kwa afya za watoto wetu...
hongerav mama x .umetusaidia wa mama .mi ni mama na mwanangu kapata chanjo zote.lakini nilikua sizijui maana yake.asante kw kutujuza
hongerav mama x .umetusaidia wa mama .mi ni mama na mwanangu kapata chanjo zote.lakini nilikua sizijui maana yake.asante kw kutujuza
Post a Comment