Showing posts with label Jokes. Show all posts
Showing posts with label Jokes. Show all posts

Saturday, December 8

Wadau wanalalaje?

...ukilala na mdau mara nyingi ni fujo mtindo mmoja...
check sleeping position hizoo hapo, afu jichagulie zenu.
Wikend njema.

Saturday, November 17

Nyonyo tam jamani!!!

...mdau amenivunja mbavu mno...kalicheki "mh, kama ya mama"
...then akafanya mambo...
weekend njema nyooote!

Friday, November 9

Sunday, August 19

Unajua kusoma ripoti ya shule ya mwanao?


Ukiwa mzazi ni vizuri kuelewa namna ya kusoma ripoti za shule za mwanao hapa ni tafsiri halisi za nini walimu huwa wanamaananisha katika ripoti ya mwanao.

1. Mwanao ana upeo wa hali ya juu wa kupata taarifa toka kwa wanafunzi wenzie = Mwanao keshakamatwa mara nyingi akipiga chabo kazi za wenzie 
2. Mwanao na mchangamfu mwenye afya nyingi = Mwanao hatulii mahala pamoja ni msumbufu
3. Mwanao anaubongo wenye uwezo wa kutunga vitu vingi vipya = Mwanao muongo sana 
4. Mwanao anaonyesha tabia za utulivu usiotaka wala kutegemea usumbufu = Mwanao mvivu kupindukia 
5. Mwanao anaonyesha kipaji kikubwa cha kuwa mwanasiasa = Mwanao mbishi kupindukia 
6. Mwanao anakipaji cha kupenda kuzuru sehemu mbalimbali nje ya maeneo ya shule = Mwanao mtoro shuleni 
7. Mwanao ameweza kuendelea kuhifadhi tabia nyingi za wakati alipokuwa na umri mdogo = Mwanao kikojozi

Jumapili njema. Shukrani kwa CHEKA NA KITIME

Sunday, August 12

Watoto nao wana mpango wa kugoma...


TANGAZO LA KUSUDIO LA KUGOMA:
Huyu sijui ndio mwenyekiti wao...yuko siriaz...

Sisi watoto tulio na umri chini ya miaka mitatu tunakusudia kugoma ili kupata haki yetu ambayo tumeporwa na watu wasio na utu wala huruma. Inaeleweka wazi kuwa sisi ndie wenye haki ya jina la BABY. Kwa ufisadi wa hali ya juu jina letu limeporwa ambapo sasa vigogo, Mawaziri, Wabunge tena wa kambi zote, wazee sana, wazee wa kati, mapedeshe na masharobaro, mayanki na mafisadi wa jina hili wote eti nao wanaitwa BABY, hii si sawa kabisa. Tunaipa serikali siku saba kupiga marufuku matumizi ya jina hili kwa wasiohusika kinyume cha hapo, patachimbika, tutaanza kwa mgomo usio na kikomo nchi nzima na hatimae kuona namna ya kuweza kuunganisha nguvu na BABY wenzetu halali dunia nzima.
HILI NI ONYO LA MWISHO.

Hii nimeitoa kwa Anko Kitime, mcheki hapa, CHEKA NA KITIME uongeze siku za kuishi.

Saturday, June 23

Ni kweli haya?


Hii nimeibamba sehemu, kuhusu wanachowaza watoto kuhusu mama zao wakiwa na umri mbalimbali....
Miaka 6: I love you mommy
Miaka 10: Mom, whatever…
Miaka 16: My mom is so annoying!
Miaka 21: Nataka nihame nyumba hii!
Miaka 30: Mom, you were right.
Miaka 40: Nataka nirudi kwa mama
Miaka 50: Sitaki kumpoteza mama yangu
Miaka 70: Ntatoa chochote ili niwe pamoja na mama yangu…

Jiangalie, uko group gani, unawaza hivyo??? Na ulivyokuwa na miaka 16 je?

Tuesday, June 19

Haki 7 za mama mjamzito


1. Mama mjamzito ana haki ya kupishwa akae, hata kama amechelewa kufika eneo la tukio, na nyie wengine mmegombea hizo siti, mpisheni tu!


2. Ana haki ya kudondosha kitu na kusubiri mtu ajitokoze kumwokotea!

3. Ana haki ya kudai umiliki wa chakula cha aina fulani ndani ya nyumba. Yaani hicho chakula kikiingia tu, hata kama amekuja nacho mgeni, inabidi aki-surrender kwa boss! Na ole wake atakeyechukua kile cha mwisho kilichobaki, afu mwenyewe aamke saa 9 kukitafuta, siku hiyo ndio mtajua nani ni boss!

Wednesday, March 4

Kujiandaa kwa Uzazi

Mtoto wa Kwanza: Unasoma na kujitayarisha kwa kila kitu, unauliza kila swali kwa docta.
Mtoto wa Pili: Huangaiki kusoma maana haikukusaidia kitu wakati wa uchungu wa mtoto wa kwanza.
Mtoto wa Tatu: Unaomba operesheni mapemaaa!

Wednesday, January 28

Nyumbani

Mtoto wa Kwanza: Miezi ya mwanzo kila siku unatumia muda mrefu ukizubaa unamwangalia tu mtoto.
Mtoto wa Pili: Utatumia muda mwingi kuhakikisha mtoto wa kwanza hamtoboi macho wala kumfinya mtoto mpya.
Mtoto wa Tatu: Unatumia muda mwingi kujificha watoto wasikusumbue.

Wednesday, January 21

Kubadilisha Nepi

Mtoto wa Kwanza: Unabadilisha nepi kila saa, hata kama haijachafuka kiasi cha kubadilisha.
Mtoto wa Pili: Unaangalia kama inahitaji kubadilisha kila baada ya masaa mawili au matatu.
Mtoto wa Tatu: Unajitahidi kubadilisha nepi kabla watu hawajaanza kuhisi mtoto amechafuka au mtoto hajaanza kuonekana kama amebeba mzigo mzito kwenye nepi.

Wednesday, January 14

Kudondosha Pacifier


Mtoto Wa Kwanza: Pacifier ikidondoka unaichukua unaiosha na kuichemsha ndio unampa mtoto aitumie tena.
Mtoto wa Pili: Pacifier ikidondoka unaisuuza na maji masafi yaliyochemshwa yaliyo karibu,hata kama yamepoa, then unairudisha mdomoni kwa mtoto.
Mtoto wa Tatu: Unaifuta kwanye t shirt au khanga yako kasha unairudisha mdomoni kwa mtoto.

Wednesday, January 7

Kumeza Sarafu(coin)

Jayson James akiwa amekula pozi.
***
Mtoto wa Kwanza: Mtoto akimeza sarafu ya hela au kitu kigumu unakimbilia hospitali na unang’ang’ania wampige x ray kuangalia kiko wapi.
Mtoto wa Pili: Akimeza sarafu ya hela unasubiria kuangalia kama imeshapita na kuitoa kwa njia ya choo.
Mtoto wa Tatu: Huyu akimeza hela kama shingi mia, unaitoa kwenye hela zake ulizotaka kumpa anunulie juisi.

Friday, December 19

Kumuacha Mtoto Nyumbani Mara ya Kwanza

Mtoto Lisa-Joann Erick akiwa amepozi, mtoto mzuri kama Malaika.

Mtoto wa Kwanza: Ukimuacha mwanao nyumbani kwa mara ya kwanza, unampigia dada mara 5 ndani ya kila nusu saa, na hapo umemuachia vocha ya 5,000 akupigie mtoto akilia.
Mtoto wa Pili: Kabla ya kutoka, unakumbua kumuachia dada mia tano ya vocha ya kukupigia kukiwa na tatizo.
Mtoto wa Tatu: Unamwambia dada akubipu akiona mtoto ameumia na anatoka damu.