Showing posts with label Myth. Show all posts
Showing posts with label Myth. Show all posts

Thursday, January 29

Watoto wa Kike na Baba, wa Kiume na Mama

Mama's Boy, Mwita akiwa amebebwa na mama yake, Gladys Fahari.
Dady's Girl, Aurelia Croft akiwa na baba yake Richard Croft.
***
Inasemekana kuwa watoto wa kike huwa wanawapenda sana baba zao, on the other side, watoto wa kiume nao wanawapenda sana mama zao. Jamani wadau kuna ukweli wowote?

Thursday, January 22

Uzi Mweusi Mkononi Kwa Mtoto

Huku mitaani kwetu, hasa ukwa sisi tunaoishi uswahilini ni kitu cha kawaida kabisa kuona mtoto amefungwa uzi mkononi, wenyewe wanasema unafukuza watu na vitu vibaya wanaotaka kumdhuru mtoto. Wadau hiyo imakaaje kaaje, na kwa waliowahi kufanya hivyo watupe faida zake, ukute utandawazi unatuharibu, vitu vingine vina faida tunadharau.

Thursday, January 15

Kubemenda Mtoto???

Wadau hivi nani hajawahi kusikia kuhusu kubemenda mtoto huko majumbani na mitaani kwetu. Ila mimi pamoja na kupekua huku na kule wakati wa ujauzito na hadi leo sijawahi kuona kubemenda kwa nchi zilizoendelea. Hivi kweli kuna kitu kama kubemenda mtoto? Ni nini hasa? na inasababishwa na nini?