Showing posts with label Siblings. Show all posts
Showing posts with label Siblings. Show all posts

Thursday, December 6

Kaka na dada wakifanya homework!

Wadau Jasmine na J wakifanya homework home kwao Mabibo...fuatilia uone colabo hiyo.








Monday, June 11

Beautiful Bibi Ever

 Emmanuel keshajizoelea mwenyewe analelewa na bibi.

Bibi na mjukuu, Watoto wetu wote wanapitia katika mikono ya Bibi Joan. 
Wakiwa kwake wapo kwenye mikono salama.
 Wajukuu (Geofrey, Joan, Cleopatra na Emmanuel) wanakupenda mno mama.

Saturday, May 26

J&J wanawapa Hi!

Wadau wenzenu Jasmine na kaka yake Japhary wanawapa hi. 

 Cute J mdogo.

Luvly J mdogo na J mkubwa.

Sunday, May 6

Joy & Joel



...wadau Joy & Joel... wako wasweeeeet!

“Watoto wangu nawapenda sana mungu awaongeze katika maisha yenu,” from loving mama.

Wednesday, February 29

X ingizo jipya!

New family member anaitwa Xyleen Lerato Mapunda...hii ni few minutes after birth!
During my time out nimeleta kitu kipya! Huyu ni mdogo wake Xchyler, anaitwa Xyleen (tamka Shyleen) kifupi ni Xy (Shy). So unaweza kuniita 'Mama X squared'.

Kaka mtu, aka Biggie aka X anampendaaaaaa balaaa...! I know for sure anampenda kuliko mtu yeyote!


X alikuwepo tangu mwanzo, alikua anamsubiri kwa hamu huyo mtoto...


Safari yake ilianzia wakati uleeeee nikiwa SA, so ndio maana tukampa jina la kati  la Lerato lenye sili ya ki-Tswana lenye maana ya pendo.
...Pozi la tumbo....



Bize hadi siku ya mwisho...
 Hii ilikua kama siku tatu before kumpokea mgeni huyo...nilienda kazini hadi Ijumaa, Jumamosi mchana nikaenda hospitali, nikajifungua usiku wa kuamkia Jumatatu.





Binti shashiriki matukio mengi ya kifamilia, ikiwamo hii graduu ya dady...
 Kuna walionitumia msg kuuliza kama huyo hapo ni X, yes, ni yeye akiwa na memba mpya wa familia, wakimpa tafu dady kwenye mahafali. (Huyo ni classmate wa dady, Hoyce Temu).




anapenda sana kucheka.

Leo anatimiza miezi sita ya kuzaliwa, so alizaliwa August 29, 2011. Ana kajino kamoja, hiyo picha ya kajino bado sijaipata, maana ni la chini, so kulipata kwenye pozi si kazi ndogo! Katika miezi sita hii kuna mengi ya kusema juu yake, ila mtamjua tu taratibuuu...


...na hapa kwenye bembea yake humtoi!

Of all the things anapenda kula, anything, ila haswa nyonyo!!!
hapa na dady home...

Nashkuru Mungu nimepata shost wa ukweliiii...swali ni nimejizaa au sijajizaa???

Mdau na wewe una update? Iwe la mdau huyo huyo wa zamani tunayemjua au una ingizo jipya we tuma kwenye mamanamwana@gmail.com, maana nimewamisi wadau wangu balaaa!

Tuesday, May 25

Jameel & Rehema wanawapa hi!

 Wadau Jameel na Rehema Mwakitalu wanawapa hi wadau wooooote wa Mama na Mwana.

 
 Rehema akiwa amepoziii...

Sunday, May 23

Asra, Abra na Naira wanawapa hi!

 Mdau Abra akiwa amepozi...

Mdogo wake Abra, anaitwa Asra...hawa wadau hawajaonekana siku nyingi sana...Mashallah, wamekua, hongera wazazi kwa kukuza.

Hapa Abra anatuletea mdau mpya ambaye ni cousin wao, anaitwa Naira...Karibu!

wadau wote watatu...baautiful!

Abra, Asra na Naira wanawasalimia wadau woooote, wanasema wanawapenda sana.

Tuesday, May 18

Karibu Baraka

 Jana tu nimeulizia baby no 2, nimepata jibu toka kwa Edda Mmasi, anasema yeye tayari keshatuletea mdau wa pili.
Malaika huyu mpya, anaitwa Baraka, amezaliwa Ijumaa ya tarehe 30 April.

Cuuuuuuuuuuuuuuuuuute!
Alizaliwa kwa operation, maana alikua 4kg, Mungu amejalia, mdau na mama, Edda Mmasi wanaendelea vizuri. Kaka yake mkubwa anaitwa Prince, ni mdau wa siku nyingi sana hapa kwenye playground yetu.

Hapa kaka mkubwa akinywa soda kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka miwili, ilikua February 2.

tam tam ya pool table...

Party ilikua home, then akaenda kujivinjari South beach, kama anavyoonekana hapo chini...

Miwani imemtoa bomba!
*****
Mama na Mwana pamoja na wadau woooote tunampongeza mamie Edda kwa kuleta mdau mpya wa kucheza naye hapa kwenye playground yetu, pia tunamuombea mdau mpya Baraka, Mungu amjaalie afya njema na maisha merefu yenye kheri na baraka tele amzidi hata wa jina wake Baraka Obama.

Thursday, April 8

Abra anajidai na baby sister

 Mdau Abra alikua akituambia amepata baby sister sasa anawiki moja anaitwa Asra

Huyu ndio mdau mpya Asra...
 
...na huyu ndio da'mtu Abra...

*****
Hiyo seti ya majina nimeipenda, Abra, Asra.

Sunday, December 6

Collin na Colman

Collin na mdogo wake Colman Francis wa Arusha...naona wadau wanazidi kufanana siku hadi siku.

Wednesday, November 4

Bro & Sis love

Kaka Vicent akihug na kukiss na dada yake Vallencia.
Hii picha inapendeza sana, maana sio kwamba wamepozishwa, wameamua wenyewe.
Cuuuuuuute!

Tuesday, October 13

Valle & Vice wanakula raha!


Wadau wa siku nyiiingi, Valencia na kaka yake Vicent wamepatiwa na mama yao, maana wana ugonjwa wakuchezea maji (kama X) basi mama yao, Lulu Kilonzo akaona isiwe tabu, akawanunulia hilo bwawa la plastiki, anawajazia maji humo wachezeee wee hadi wachoke.
Kwa kweli Lulu kama ulikua kwenye mawazo yangu, maana hata mi kila siku nawaza kumnunulia X, maana anavyopenda maji, we acha tu!
Nataka nijue bei yake tu, niliangaliaga zamani kidogo haikua bei mbaya sana, na kulinganisha na bwawa la ukweli, hiki kijibwawa ndio ukombozi wetu!

Sunday, October 11

Audery, Christian na Faraja

Wadau pacha Audrey na Christian wakiwa na kaka yao Faraja wakicheza kwenye sehemu maalum ya kuchezea mchanga, huu hauna vumbi!

Friday, August 14

Beautiful Sisters - Rogathe & Billie

Beautiful sisters Rogathe akiwa na dada yake Billie.
Wadau wa Mwanza hawa.

Friday, June 12

Valencia na Vicent - Kama Pacha

Valencia na Vicent Kusekwa ndani ya pozi kali.
Mama yao, Lulu Kilonzo, aliniambia hawa watoto wako kama mapacha, sikuamini sana, ila sasa naanza kuamini, maana hebu check midomo yao ya chini, na wanavyoangalia, si utani wanafanana sana.

Friday, April 10

Brian & Glory

Brian (miaka minne na nusu) akiwa na mdogo wake Catherine Glory, ambaye ni ingizo jipya kwenye familia. Cathy alizaliwa tarehe 4, Feb 2009.

Thursday, January 22

Agnes & Josephine

Agnes Mkumbi akiwa na mdogo wale Josephine Mkumbi nyumbani kwao.