Showing posts with label Ugunduzi. Show all posts
Showing posts with label Ugunduzi. Show all posts

Monday, February 23

Ugunduzi: Mtoto Kwanza, Wewe Mwisho

Kumbe wewe sio mbinafsi! Siku hizi uko tayari usinunue top nzuri, viatu vikali na pochi bomba, unavyovihitaji hasa ili mradi yeye apate kibanio! Halafu hakitaki!

Monday, February 16

Ugunduzi: Usipochafuka Utajifunzaje?

Unagundua nguvu ya Omo - Usipochafuka utajifunzaje? Utanyanyua mtoto aliyelowa mkojo, plus ana mauji uso mzima na kumkumbatia ukiwa umevaa pigo lako jipya la kazini au mtoko ili aache kulia! Kuchafuka kitu gani bwana, si ndio maana wanatengeneza sabuni na stain removers?

Monday, February 9

Ugunduzi: Ongea Lugha Mpya Kwa Sekunde!

Nini kuongea kiingereza kwa wiki tatu, kuna kuongea lugha mpya kwa sekunde! Unagundua kuwa unaelewa lugha mbalimbali bila kujifunza, ‘nga nga nga nga’ inaleta maana kwako! Yani akitamka tu, ushaelewa anamaanisha nini.

Monday, February 2

Ugunduzi: Usingizi ni Kwa Wasio na Watoto Tu!

Kama unapenda usingizi na ni mchelewaji kuamka kama mimi pole! Malaika huyu anakuamsha asubuhi na mapema, saa 11.30 na hapo, most of the time anakuwa kakusumbua usiku mzima! Usingizi bye, bye!

Monday, January 26

Ugunduzi: Kioo sio cha Kujitazamia Wewe!

Ukiwa naye huku unatizama kioo, badala ya kujiangalia wewe, unamwangalia yeye!

Monday, January 19

Ugunduzi : Unazidi Kuwa Mwoga

Kama ulikua unaamini kuwa wewe sio muoga, subiri ukipata mtoto ndio utajua. Unaogopa hata gari kwenda kasi, kila habari unayoisikia kuhusu hatari ya watoto unaifikiria mara 20! Ile ajali ya wale wa Tabora waliofia ukumbini unafikiria wanao walienda wapi sikukuu iliyopita. Kila kitu unakua makini zaidi.

Monday, January 12

Ugunduzi: Unazidi Kuwa Close na Wazazi Wako

Najua kila mtu anawapenda wazazi wake, na kuna wanaodhani wakipata mtoto hawatakuwa karibu sana na wazazi wao, ila jua kuwa ukipata mtoto ndio unawapenda zaidi, kuwathamini zaidi naunazidi kuwa karibu na wazazi wako.

Monday, January 5

Ugunduzi: Kijino Kimoja Dili

Xchyler akicheka na vijino vyake viwili ambavyo viliwahi sana kutoka, tatizo vinavyofuata haviji, bado tunaendelea kusubiri miezi minne imeshapita sasa.

Unagundua kuwa hujawahi kusubiri kitu kama unavyosubiri kijino kimoja kiote! Na kikitokeza tu ndio utakapojua kuwa kijino kimoja kinaweza kujaza gazeti la Daily News, as kuna mengi ya kusema kuhusu hicho kijino kimoja. Kila mtu ukikutana nae ‘ameshaanza kuota meno, anang’ata huyo’—kumbe kijino kimoja, au vikizidi sana ni tuwili tu.

Monday, December 29

Ugunduzi: Mama yako ni Specialist wa Watoto!

X akiwa amejipumzisha kwa Bibi X. Hii picha ni ya zamani, lakini hadi kesho jamaa ni kipenzi cha bibi, huwezi kuwatenganisha.

All of the sudden unagundua kuwa mama yako ni pediatrician, na si wa kubabaisha kwani ana PhD ya udokta wa watoto. Mama yako ndio dockta wa kwanza kabla ya Dr Massawe hajamuona mwanao. Zile simu za, “Mama mototo analia sana leo nimpeleke hospitali?” ni za kumwaga. Yani bibi ndio anaamua mjukuu aende au asiende hospitali, halafu juu ya hapo atachosema yeye ndio cha mwisho, hata Dr Massawe aseme nini! What could we have done without our mothers?

Tuesday, December 23

Ugunduzi: Hujawahi kupenda maishani!

Mtoto anakufanya ugundue kuwa mtu ambaye haongei, wala hajafanya juhudi zozote umpende halafu hazingatii hobbies zako (anakuzuia kujirusha, anakuamsha usiku wa manane, analia wakati hujafanya kosa) ndio unamfia kichizi. Yani hujawahi kupenda kama unavyompenda huyo, uko tayari kufanya chochote kwa ajili yake.

Monday, November 24

Ugunduzi Anaoleta Mtoto

Love at First Sight!


Joyce Macha na kipenzi chake cha ukweli, Davis, mara baada ya kujifungua.

Unagundua kuwa kweli kuna Love at First Sight!
Mtu humjui wala hujawahi kumuona, ila ulipomtia machoni kwa mara ya kwanza, ulimpenda sekunde hiyohiyo!