Showing posts with label Ujauzito. Show all posts
Showing posts with label Ujauzito. Show all posts

Tuesday, May 22

Best wishes Naomi

 
Mdau Naomi Lugoe yuko kwenye hatua za mwishomwisho kutuletea malaika...

...hizi picha nimezipiga last week, though yuko mwishoni, bado ana nguvu na uchangamfu wake kama kawaida. 
Mama na Mwana wish you all the best. xoxo.

Wednesday, April 14

Msaada: Mahitaji ya kwenda nayo hospitali wakati wa kujifungua

Habari dada Jiang na hongera kwa kutuhabarisha mambo mengi kuhusu watoto.
Naomba msaada wako, mimi naitwa Stella nina ujauzito wa miezi nane naomba unisaidie kama ifuatavyo:
Nikifikia wakati wa kujifungua hospitali natakiwa niende na nini na nini?
Na ajili ya mtoto atakayezaliwa;
Ni vitu gani natakiwa kununu kwa ajili ya mtoto?
Nakutakia kazi njem.

*****
Hello Stella, 
Mahitaji kwa ajili ya mtoto bonyeza hapo kulia kwako, chini ya Bongo Blogs palipoandikwa Mahitaji ya Awali, utapata mahitaji yote yanayotakiwa.
Kuhusu vitu unavyotakiwa kwenda navyo hospitali, inategemea na hospitali, as zingine hawaruhusu umvalishe mtoto chochote cha kwako na wala haiitajiki uende na chochote, wakati kwingine, hadi uzi na sindano utatakiwa ubebe, hapa wadau watasaidia experience zao kwenye hospitali mbalimbali.
Nakutakia kila la kheri, Mungu akujaalie ujifungue salama, tumuone mdau mpya!
Asante, Jiang.

Thursday, March 4

Msaada tutani: Boyfriend kakataa mimba!

Hello Jiang,
kwanza nakupa hongera kwa kazi unayofanya nafikiri kuwa na kazi ya ofisi,mama wa mtoto na kublog si mchezo,endeleza kasi nzuri.
mimi ni mdada wa miaka 27,pia samahani kama nitakuwa nimekusumbua lakini katika kuangalia nimeona wewe uko very positive na maisha hasa kuhusu watoto,nimejifunza kutotafuta ushauri kwa mtu ambaye ni negative mara nyingi,
sasa tatizo langu ni hili imetokea katika maisha yangu ya mahusiano nimekuatana na mtu tukapendana kwa muda ambao nakiri sio mrefu wa kutosha tukafanya zile habari za wapendanao lakini ile siku tu kumbe haikuwa salama kwangu nikapata ujauzito,kweli nilikosea kukubali kufanya mambo ayo in the first place mbaya
zaidi sikutumia kinga kweli hapo najua nimekosea hasa usinishutumu nimeshakiri
Shida inakuja baada ya kumuambia huyo boyfriend akasema hana muda  wa   kulea  mtoto sasa hivi kwanza anataka kwenda nje ya nchi mwezi wa tano(mambo yakienda sawa wangu atazaliwa mwezi wa sita)  kwa  sababu  hiyo niitoe hiyo mimba, nijibu tu kwamba lakini mbona watu wanalea watoto zao wakiwa mbali akageuka ooh umenitegeshea kulala na wewe siku moja tu umeingia mimba kwani hukujua kama ni siku ya hatari? nikamjibu tu unakumbuka nilivyokulazimisha tutumie kinga ukakataa? hakukubali ukweli, basi uhusiano ukaanza kuyumbia pale siku moja akawa nje ya dar nikaamua tu kutoka moyoni nikijua atakuwa na msimamo tofauti,najuta hata kwanini niliwasiliana naye siku hiyo,akaniuliza enhee vipi hiyo mimba umeishaitoa mimi nikamuambia bado, akauliza kwani ina muda gani nikamuambia ndio inamaliza mwezi inaelekea mwezi wa pili,akaniambia sasa kinashindikana nini si tutoe tu bado ndogo hiyo,nikamwambia siko tayari mi naona kwa sasa sina kipingamizi nitamlea tu huyu mtoto,(nilishawahi kutoa mimba kabla,mungu anisamehe nikaapa sitarudia tena maishani mwangu)
Basi ndio akaniambia unajua sio vizuri kuzaa watoto wawili wakati hujaoa                        na nilishakuambia mi nina mtoto wa miaka miwili sasa itakuwaje mi nikamuambia sio shida nitaficha tu kwa watu kwamba sitataja jina la baba kama swala ni aibu,akasema hivi kwa nini umengangania nikamwambia mi naona kwa umri na kazi na upendo nilionao kwa watoto sina sababu ya kutoa mimba kwa sasa,akaniambia sasa sikia nikuambie nina mke ana mtoto mmoja na nategemea mwingine mwezi wa pili (huu tuliopo) na kama naendelea na msimamo wangu fine lakini hataweza kumtunza mwanangu na wala nisimtafute tena anafurahi tumejuana hawezi kuvunja ndoa yake kwahiyo ananitakia maisha mema, siku ile nilikuwa kwa rafiki yangu vinginevyo hata ningeweza kuanguaka na kuzimia kabisaa uchungu wake siwezi kuelezea kiufasaha,rafiki yangu akaniambia usitoe kaza roho mtoto utamlea tu yeye(rafiki ameolewa)
basi ukichanganya na maamuzi binafsi niliyochukua nikaamua kulea tu huu ujauzito peke yangu nimeendelea nao weee lakini huko kazini hali mbaya siitwi tena kwenye projects kama zamani yani nimechacha mpaka sasa nimetafuta kazi wee mpaka nimeishia kukubali kazi za kawaida sana hivi ninavyoongea mimba inaelekea kutimiza miezi mitano lakini honestly siko stable kifedha na baba mtoto hanibip wala kunisms.
kinachonipa hofu kuna siku nikiamka asubuhi moyo unaona nimeelemewa nakata tamaa ya kila kitu naona sitaweza naishia kulia tu lakini baadae najipa moyo ila naona kama inazidi sasa yani sina uhakika na maisha tena yani sijui hata nisemeje
ndio maana nakuomba tu ushauri maana mtoto namtaka ila haya mzingira niliyopo naona kama nitapata shida sana kuna wakati najuta sana
hebu nishauri ndugu sijui hata nifanyeje tena
natanguliza shukrani
narudia tena samahani kwa usumbufu

Saturday, January 10

Ujauzito - Dalili No. 1

Ushahidi: Home Pregnancy Test

Hot maternity wear, siku hizi kupendeza ukiwa na mimba ni kitu cha kawaida, nguo fashionable kibao kama Regina anavyoonekana hapa.
***
Kama una dalili zote hizo tisa, au nyingi kati ya hizo na bado huamini kama u mjamzito basi kwa uhakika zaidi nunua home pregnancy test kit yako ujipime uone. Hii ndio test ya mwisho kabisa.

Kama kipimo hicho kinaonyesha positive then, CONGRATULATIONS, YOU ARE GOING TO BE A MOTHER!

Friday, January 9

Ujauzito - Dalili No. 2

Joto La Mwili Kuwa Juu Saa Zote


Mtu mjamzito huwa ana joto kali kuliko ilivyo kawaida, so kama watu wakikusalimia kwa kukushika mkono wanasema unajoto kali, na unajua sio kawaida yako na wala huna homa, na ukijichunguza mwanyewe unaona kweli joto limezidi,then ujue labda tayari.

Thursday, January 8

Ujauzito - Dalili No. 3

Period Kuyeyuka
***
Hii ni moja ya dalili tatu kuu, ingawa mwanamke unaweza kumiss period kwa sababu tofautitofauti, ukweli ni kwamba huwezi kuwa mjamzito na period ikaja kama kawaida, na swali la kwanza unalojiuliza mwanamke kama ukikosa period ni mimba, hata kama unatumia kizuizi!

Wednesday, January 7

Ujauzito - Dalili No. 4

Kukojoa Mara Kwa Mara

Siku hizi ukiwa mjamzito vifashion kibao, Regina anaonyesha.
***
Kabla hata mtoto hajaanza kukandamiza kibofu chako akiwa mkubwa tumboni, utaanza kwenda msalani mara kwa mara kwanini? Well, mimba inafanya kiwango cha maji kiongezeke mwilini, so safari za kile kichumba kidogo zinaanza mapema.

Tuesday, January 6

Ujauzito - Dalili No. 5


Kuvimba Mwili GhaflaRegina Kumba akiwa amekula pozi, mtoto huyu tunamsubiri kwa hamu mwezi ujao, maana tayari ni memba.
***
Mabadiliko ya hormones kunaweza kukakufanya ujisikie kama umevimba, na nguo zinaweza zikawa zinakubana flani hivi ingawa wala hata hujaanza kunenepa, na watu wengine wanakuona kawaida tu.

Monday, January 5

Ujauzito - Dalili No. 6

Kutopenda Harufu

Mimba changa inasababisha mtu asipende harufuharufu hata kama ni nzuri. Wengine hata perfume za waume zao hawataki kuziskia, jasho lao ndio kabisaaa. Na unaweza ukajikuta vyakula fulani ulivyokua unavipenda unachukia harufu yake hata hutaki vikusogelee.

Sunday, January 4

Ujauzito - Dalili No. 7

Kichefuchefu au/na kutapika

Wanawake wengi huwa wanapata kitu kinachoitwa morning sickness, lakini haiji hadi mwezi baada ya mimba kutunga. Na wachache hawapati hiki kitu kabisaaa.
Na hilo jina la kizungu lisikudanganye, kutapika sio morning sickness tu, kama wewe ni wa kutapika unaweza kutapika asubuhi, mchana au usiku!

Saturday, January 3

Ujauzito - Dalili No. 8

Damu ya Upandikishaji

Hii ni kwa baadhi ya wanawake, sio wote, damu kidogo inaweza kutoka siku ya 11 au 12 (hasa muda ambao unaanza kugutukia kuwa period imechelewa) baada ya mimba kuingia.
Ila damu yenyewe ni nyepesi sana, na ni kidogo sana, na wataalam wanasema inasababishwa na yai kujipandikiza kwenye kuta za nyumba ya uzazi, ambzo zimejengwa kwa damu.

Friday, January 2

Ujauzito - Dalili No. 9

Uchovu

Unajisikia mchovu bila sababu, mmh, labda tayari. Haijulikani kwa nini watu wanajisikia uchovu hata mara tu baada ya kupata ujauzito, maana hamna uzito wowote ulioongezeka.

Thursday, January 1

Ujauzito - Dalili No. 10

Maziwa Kujaa

Maziwa yakujaa, au ukiyagusa yanauma flani hivi, ni dalili ya mwanzo kabisa ya mimba ambayo hata hivyo watu wengi hatuifahamu. Sababu kubwa ya kutoifahamu ni kwamba kwa wanawake wengi period ikikaribia hali hii huwa inatokea tu mara nyingi, so hapa tunaiconfuse ya mimba na ya period.

Wednesday, December 24

Dalili Kumi Kuu Kwamba U-Mjamzito

Mie, enzi hizooo.
Kwa mtu anayetamini kuwa mama, dalili ndogo tu anaanza kufurahia, kwa anayeogopa ndio anachanganyikiwa ghafla. Najua mwanamke yeyote kamili anaanza kuhisi kuwa yu mjamzito mara tu baada ya kumiss period yake.

Since hii ni blog ya kuelimishana kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo watoto, mwaka mpya mambo mapya. Kuanzia tarehe moja hadi tarehe kumi January 2009, nitapost dalili kumi kuu za kukuambia kuwa u-mjamzito, kuanzia ya mwisho hadi ya kwanza, yenye uhakika.
Stay Tuned…
NB: Nitumieni hizo picha za ujauzito niambatanishe na postings zangu.