Saturday, December 6

Mdahalo: Watoto Kunyonya Vidole


Xchyler kwa kidole, yani ukitaka ugomvi nae umtoe.
Jamani mnasemaje kuhusu watoto kunyonya vidole? Mtoto aachwe aje kuacha tabia hiyo akikua au awe anakatazwa? na nipeni ushauri, akatazwe kwa njia gani, maana mi mwanangu ananipa tabu tabia hiyo.

9 comments:

Anonymous said...

Nina watoto walili, mapacha na wote wananyonya vidole kile waendapo kulala. Nafikiri waache tu wanyonye mpaka wataacha wenyewe. Ni sawa na pacifier ambazo watoto hufikia umri wa kuziacha wenyewe. Hiyo ndio jinsi ya kujibembeleza wakati wa kulala au kama kuna umuhimu wa wakati wao pekee!
Papa G

Anonymous said...

Nimefurahi sana kukutana na hii blog,ni mzazi wa watoto 2,mtoto wangu wa 2 ana miezi 11 na ananyonya vidole tokea akiwa na miezi 2,nionavyo ni vyema kumuacha mpaka pale atakapo kuwa na kuacha yeye mwenyewe.

Anonymous said...

Sula la kunyonya kidole huwa ni gumu sana kulijadili. Sijui nianzie wapi.
Ila mimi nimekuwa na watoto wawili na wote walikuwa wananyonya vidole. Kila walipofikia miaka 2.5-3 waliacha wenyewe. Ila athari yake ni kwamba wote walipoanza kuzungumza walikuwa na kithembe.
Ila pia kuna wengine huwa wananogewa. Ni vizuei kuwa unamkataza taratibu ili asizoee sana ikamwathiri maishani.
Mdau.

Anonymous said...

Kwa kuwa hakuna mtu anamtuma mtoto kunyonya kidole, wengi wanafanya hivyo baada ya kuzaliwa wengine baadae, nadhani atapokuwa anakuw unaweza kujaribu kumsitisha kidodo kidogo kuangalia usiingilie saikolojia yake. ila najua kuna mdahara watoto meno yanaenda mbele sana, piaa faida yake moja wanakuwa watulivu kwa kupata komfoti ya kidole wakati wako na njaa au usingizi , pia inakuonyesha kuwa ana nja umlishe au anataka lulala au amechoka , lakini wakiachwa wananyonya vidole mpaka wakubwa so, jaribu ila ni ngumu sana kumkataza mtoto, naomba kama kuna mtu anafahamu njia, Tusaididiane. Thanks.

Anonymous said...

hi jiang,
naitwa Dr.Sima, hongera sana kwa your new step in proffession na blessings with handsome baby boy, i would like to share hiyo kunyonya vidole.
well for infants mpaka four years you can leave them ila cha kumonitor ni usafi kuzuia infections.ila there after kama akiendelea basi kuna way foward to do.
kwanza ni kujaribu kumweleza taratibu with tricks like ahadi ya kitu kizuri kama ataacha,if fail anaplekwa kwa wataalam wa psychologoa ku try to find what stresses him/or her mpaka anajikuta anatafuta alternatives which is to suck na so wakishaeliminate course inaisha ila kwa wale wanaoendelea kewa sababu inaweza kuleta facial assymetry na kuharibu sura ya mtoto basi kuna vifaa vya kumvalisha ili kuzuia asiendelee kunyonya untill aache. next time ntatengeneza notes kabisa nikutumie.
all the bst

Anonymous said...

hi dada,
im a young mama 22 years of age with a sweet 4 months old baby boy. yeye ananyonya kidole all the time, sidhani out of stress bali kupenda tu. ananyonya vizuri nipo nae all the time (nimegraduate university so bado sijatafuta kazi), so hakuna cha kumstres pia nampa attention yangu yote. nakutumia picha ya siku ya kwanza kuzaliwa, pia ya sasa alivo 4 months pia ambayo amekaa na mdoli wake. ameanza kukaa sasa. nice day,
julie

Anonymous said...

hi dada,mimi ni mama wa mtoto wa mwaka mmoja na miezi nane ,ananyonya vidole,nimejitahidi kumwambia si vizuri aache,kidogo anaelekea,mwanzo nilimwacha coz alikuwa mdogo bt sasa anaelewa baya halitakiwi,ananyonya akijisahau akikumbuka anatoa haraka,nafikiri kwa mwaka na nusu ni umri mzuri wakuongena mtoto.

Shally's Med Corner said...

Jiang, kama alivyotoa maoni Dr. Sima hapo juu, mpaka miaka minne sio tatizo. Lakini ni bora ujitahidi baada ya hapo asiendelee. Kwani kuna baadhi ya masuala yanaweza kujitokeza kwa mtoto kama kutoota meno sawa, suala ambalo huweza kuathiri uzuri wa sura ya mtoto kwa ujumla pale anapokuwa. Ingawa kunyonya kidole sio mara zote kunasababishwa na matatizo ya kisaikolojia lakini imeonekana watoto walio na stress za aina mabalimbali huwa na tabia hiyo zaidi.
Kama mwanao keshazoea tabia hiyo inabidi tu uvumilia mpaka akue kidogo lakini uchunge usafi kwani kidole kichafu huweza kumletea infection. Anapokuwa pia na kuanza shule kama bado anazubaishwa na kidole anaweza kuwa hazingatii vizuri masomo shuleni.
Mama prince
Shally

Anonymous said...

yeah! Hayoyote yaliyosemwa ni kweli na nisawa lkn kunyonya kidole mm sioni kama ni tatizo ila tatizo linakuja pale unakuta ni binti/mvulana mkubwa let say anaumri kama miaka kumi na kuendelea forsure hakuna zaidi ya ujinga hapo i mean kwamba hata darasani huyo mtoto hafanyi vizuri coz anakuwa busy sana na kidole, na zaidi inaharibu sana meno ya mbele na siyo tuu meno jamani kina mama hata kidole chenyewe anachonyonya pia kinakuwa na kasoro. Naukibahatika kukutana na mtu mzima aliyenyonya sana kidole ulimiwake unakuwa mzito wakati wa kuongea na vitu kama hivyo so kama unaweza kuanza mapema ninzuri. nawashukuru wote.


Flojoma.