tumehama

Showing posts with label Elimu. Show all posts
Showing posts with label Elimu. Show all posts

Tuesday, February 19

Form IV 2012 Results: Zaidi ya nusu wana zero, tunaenda wapi?

Hii sio news mpya, maana sasa ni mwaka wa tatu matokeo ya sekondari hayaridhishi kabisa!!!
Kama ulikua hujui, mwaka huu ndio kali zaidi maana zaidi ya nusu ya wanafunzi wote aliofanya mtihani mwaka 2012, yaani 65% wamefeli kwa kupata zero!!!
Nimekaa hapa nayaangalia haya matokeo wala siamini ninachokiona...inasikitisha kwa kweli!!!

Sasa tatizo kama hili wote tunajua haliwezi kuwa la wanafunzi wala la eneo, wala sisi tunaowalipia wanetu private hatutatiwi tuliacha kwa vile tu sio wanetu...HAPANA! Kwa sababu hii nchi ni yetu sote, mwisho wa siku tunachanganyikana wote na kwa effort za kila mmoja, kwa nafasi yake ndio tutaweza either kupeleka mbele gurudumu la maendeleo or kuliacha liserereke nyuma na kutuangamiza...so si suala la kufun=mbia macho hata kama mwanao anasoma St. Academy!

Katika vitu vyote, nimelelewa na kufunzwa kuwa hakuna kitu cha muhimu ka a ELIMU!!!
Na kwa kweli, nakumbuka nilivyomshangilia JK alipoingia madarakani first timekuhutubia bungeni alisema kwenye serikali yake kitu cha kwanza ni Elimu, cha pili ni Elimu, na cha tatu i Elimu!!!!
Elimu sio kitu cha kuchezea...

Sasa inasikitisha sana kusikia kuwa zaidi ya nusu ya form four wamefeli, zero kabisaaaa, yaani wamezungusha!!! Sio kwamba nasema hivyo kuwakejeli, as siamini kuwa ni kosa lao, ila ndio ukweli!!!!
Ile exception iliyokuwepo wakati sisi tunasoma ya  kumshangaa mtu aliyepata zero, maana wanakua wawili watatu sasa wanashangaliwa waliopata one  hadi three maana ni wawili watatu!!!
Ingia website ya baraza HII HAPA chagua shule yeyote uone hali inavyosikitisha...yaani ni zero na four ndio zilizojaa!!! Sasa hawa watoto waliopewa hope na kufaulu kwenda sekondari za kata kwa wingi wanaenda wapi after this? 

Hii inamaanisha nini? Yaani hamna kilichoingia kichani kwao tangu wainge Form I? Maana mtu akipata zero maana yake hajajifunza kitu, au? Kwa hiyo tunawapeleka sekondari ili iweje? Wakakue? Wakakutane na kujuana? Maana kiukweli hamna walichojifunza!!!

Na kwa future ya taifa letu inamaanisha nini? Tunatengeneza taifa la wajinga au sio? Ila tofauti na wa zamani, hawa tumewapa hope kidogo...ingawa wamefeli na kupata zero wamefunguka kiduchu...afu tunawaacha tu mtaani...tunatengeneza bomu, litakuja kulipuk baadae...maana kama wenye vyeti vya 

Nashauri serikari itafute mkakati wa kutatua hili tatizo maana so far tulichofanya ni kujenga shule kila kata tu...sio kwamba napinga uwepo wa shule za kata, nazisapoti sana na tangu mwanzo wakati wengi wanapinga shule za kata mie nilizisapoti, as lazima tuanzie sehemu na kwenye sector ya elimu ni majengo....

Ila sasa baada ya majengo, tumekaa tumebweteka...kama vile hayo majengo, tena madarasa mawili matatu na ofisi, ndio yatafundisha wanafunzi...kupitia kazi yangu nimeona kwa macho yangu shule ya sekondari yenye mwalimu mmoja...mazingira yenyewe tata , msituni!!! kijana ambaye hazidi miaka 27, kamaliza chuo, ndio kapangiwa kufundisha hiyo shule, iko porini mbali na makazi ya watu, afu nyumba yake iko hukohuko....afu hakuna hata network (kwa wakati huo ilikua 2008 kama sikosei)...hawezi hata kuchat na vijana wenzie aliosoma nao angalau asijione mnyonge, halafu kufata mshahara ni wilayani, mbali, kukodi pikipiki kwenda na kurudi si chini ya 80,000/- (hakukuwa na usafiri mwingine kati ya wilaya na vijijni) halafu unategemea huyo mwalimu akae!!! Kila mwalimu akikaa mwezi mmoja, ukifika mwisho wa mwezi akienda wilayani kuchukua mshahara harudi tena!!!!
Kwa mazingira hayo niambie hata huyo mwalimu akiwa na moyo mgumu akaamua akae ana moyo wa kufundisha? mwanafunzi ana moyo wa kosoma? na mwalimu mmoja, wawili au watatu watafundisha masomo yote kwa form one hadi four? Happo unategemea nini kama si zero, hata mwenye four kajitahidi sana...kwanza hao wenye zero wapewe cheti cha kufanya mtihani ingawa wanajua hawajui chochote!

Katika hili nadhani serikali inatutatia...seriously, serikali haiko serious kwenye elimu, future ya nchi yetu, kwa hiyo 10 years, 20 years to come, tusilalamike nchi yetu ikizidi kutitimia kwenye lindi la umasikini, uhalifu, ujinga na kila kitu cha ovyo, maana kwenye maisha ya karne hizi hamna kitu muhimu kama elimu....tutaibiwa madini na gesi zetu weeee hadi ziishe tubaki na mashimo, maana kama nchi tumechagua kuwa taifa la wajinga!!!! kama asilimia 6.2, tu ndio waliofaulu basi it is hightime Tanzania kama taifa tujiulize tunakwenda wapi???

Kiroho safi tu, mimi ningekua waziri wa elimu, ningepisha, ili aje mwinine anayeweza atatue tatizo, as for the time being ameshindwa kutatua tatizo. Kibongobongo, najua hatopisha, ndio maana nasema ningekua mimi! Ila Kawambwa ameshasikia maoni ya wengi katika ili, na bosi wake kasikia, tufanyeni tuone mnafanya kitu basi, sio kila kitu hadi kiundiwe tume...waziri utakua shujaa sana usema viatu havinitoshi, subiri nivue ajaribu mwingine, labda, narudia tena labda atatokea mvaaji vinayemtosha!

Kwa upande wetu wananchi, watanzania wenzangu, hebu tutafute kitu cha kufanya...lets brainstorm nini kifanyike kuokoa elimu yetu, kuokoa nchi yetu!!! 



Friday, February 1

Tujuzane tafadhali

Ni muda gani mzuri kwa watoto wa kike kuanza kusuka? 
Mi napenda kumsuka Patra ingawa naona kama namuonea
 vile kwani hajui chochote kuhusu urembo wa nywele
 wala chochote ingawa pia huwa anapendeza.
 


Tuambiane ukweli na tujadili wazazi. Upi ni muda muafaka?

Tuesday, August 28

Sale ya vitabu bomba @Mlimani City

 Unaijua Scholastica Bookshop? Zipo mbili, ya Samora Ave na Mlimani City...yap, ile Bookshop iliyopo  ndani ya Mlimani City Complex... Yes, wana bonge la sale la vitabu...ni vizuri sana...
Unakumbuka ile topic ya IJUE DUNIA katika kumwongezea mdau akili? Hapa utapata majibu yote unayotaka kuhusu dunia...kuna encyclopidia na story books kibao on sale! Mi nikadaka encyclopedia zangu za watoto by Disney nne, nilichanganyikiwa kidoogo ninunue zote!

...Hii inahusu World Leaders, nilipenda nilipomuona Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere hapo... 

...katika Statesmanship tumetisha...
Pita pale uibuke na vyako uvipendavyo, maana viko katika topic mbalimbali!

Wednesday, August 22

Siri za kumfanya mwanao awe na akili: Jifunze lugha!


Parlez-vous français? Do you speak English? Unazungumza Kiswahili? 
Kama umeelewa bofya kushoto hapo...

Thursday, August 16

Eti mwalimu awatembeza uchi darasanai wanafunzi waliofeli...

Hii stori nimeiona kwenye HABARI LEO kwa kweli imenisikitisha sana!
Yaani mwalimu unatembezawanafunzi uchi darasani kisa wamefeli?
Kweli ni udhalilishaji wa HALI YA JUU!
Mwalimu hajui psychological effect ya suala kama hilo kwa hao watoto? Si afadhali angewachapa tu! Amenisikitisha sana kwa kweli!
Yani, I cant imagine adhabu ya kupewa huyo mwalimu, hebu akasote Segerea huko aone raha yake!!!

Wednesday, August 15

Siri za kumfanya mwanao awe na akili: Kuwa mbunifu




Ingawa nchi yetu huwa hatuwathamini wasanii, ila research zinaonyesha tofauti na tunachofikiri…maana nasi kwa kudhani!!!!

Ndio maana kwa wenzetu wanakazania kuchora, kupaka rangi na aina mbalimbali za sanaa kwa watoto wadogo, kwani wameshafanya research wakagundua kwamba vitu hivyo vinawafanya watoto kuwa na akili.
Watoto wanaojifunza sanaa huwa wanaperform vizuri sana hata kwenye masomo mengine, pia huwa wana ubongo wa kujitegemea akak independent mind.

Ufanyeje?

Wednesday, July 4

Siri ya kumfanya mwanao awe na akili: Ijue Dunia




Sio lazima uwe kama kina Jolie-Pitt ndo uwe unaweza kutembelea dunia hapana kuna njia nyingi za kuijua dunia. Hapa kinachomaanishwa ni kwamba ijue dunia hata kwa kusoma tu! Yes, ukijua kuhusu tamaduni mbalimbali za hapa nchini na duniani, utamfundisha mwanao, naye atajikuna anavijua hivyo vitu bila tatizo. Kiasi kwamba akikuta watu wanabishana kuhusu 'lazima mwanaume amtolee mahari mwanamke ili awe mkewe,' anawarushia tu bomu moja, la “mbona wenzetu wahindi mwanamke anamtolea mahari mwanaume?”, wanaona katoto kajinias! Si unajua knowledge is power!

Dunia kubwa, sijui nianzie wapi?

Tuesday, June 26

Siri ya kumfanya mwanao awe na akili: Lisha ubongo


Unashangaa? Yes, unaweza kumfanya mwanao awe smart kwa chakula tu! Ndio coz kuna vyakula vinarutubisha ubongo kuliko vingine,  sasa ukivikazania hivyo utakuta mwanao anakua smart kuliko wengine wasiokula vyakula hivyo. Huamini? Basi bonyeza hapo palipoandikwa bofya hapa utiririke namie.

Wednesday, June 20

Siri za kumfanya mwanao awe na akili: Bukua nae


Kama unataka mwanao awe smart a.k.a msongo a.k.a kipanga hakikisha unamsomea. Yap, hata kama ni mdogo na haelewi kitu soma kitabu akusikilize. Actualy, msomee tangu akiwa tumboni, wanasema ile sound ya kusoma ni nzuri sana katika kumfanya mtoto awe concentrate.
Tafiti zinaonyesha kwamba watoto wanaosomewa home tangu wakiwa wadogo, huwa ni rahisi sana kuelewa shule, hivyo ni rahisi kujifunza.
Kusoma kunamfundisha mtoto vitu vingi; maandishi, maneno mapya, matumizi ya maneno, na pia inamfundisha kwamba information inatoka kwenye vitabu…

Ufanyeje?

Siri za kumfanya mwanao awe na akili

Kuna vipanga wanaozaliwa hivyohivyo...afu kuna vipanga wa kutengeneza.
Sasa coz wazazi mlikua vipanga msi-assume na wanenu watakuwa vipanga automatically, mkalipa ada na kuwabwagia manyanga teachers!
Dunia ya leo sio ya kulaza damu, so usisubiri baraka za Mungu peke yake, tengeneza mtoto mwenye akili, hata kama amepewa nyingi na Mungu ukiongezea ndo zinakaa, sometimes usipozizingatia ndo zinapotea...afu watu wanashangaa wazazi wana akili, watoto vipi?
So, fuatilia hapahapa, kila wiki, ntakumegea siri moja baada ya nyingine ya jinsi ya kumfanya mwanao awe na akili...
Soma post inayofata upate siri ya kwanza...

Monday, June 18

Schools exhibition ilikua hivi...

Hii exhibition ilifanyikia Mlimani City nje...

 Hii ni Baobab Sec School... 

 ...mwanafunzi asiyeona wa Uhuru Maalum akichapa kwenye typwriter yao maalum (kiukweli ina jina lake nimelisahau).

 ...hizi shanga zimetengenezwa na watoto wasioona wa Uhuru Maalum...

 Hapa ni banda la shule ya Uhuru wasichana...nilipapenda sana...kulikuwa na chemsha bongo za hesabu, si utani kila mtu alisimama kujaribu...

 ...Mie nilijaribu hii hapa...nilipata kufanya jibu liwe 9 kila upande, ila kwenda 10, nilichemka...very simple test, ila inachangamsha ubongo, na kumsaidia mtoto asiogope hesabu na anakua anajumlisha chapchap...
 ...ukijumlisha hapa kila upande jibu ni 10!



...Ila ilinisikitisha, shule zilikuwa chache sana...so haikusave purpose, maana kama mtu umeenda kuangalia shule ili ujue nzuri hapa usingepata jibu...

Sunday, May 27

Mmeshafanya homework?


Kama kawaida...Bibi to the rescue! (what will I do without you mama?) Namba 3 ilinishinda mie, afu nna hasira za karibu, ikabidi bibi achukue usukani, waende taratibu hadi kieleweke!
Kwa wale wenye schoolers wawe wa vidudu, primary au sekondari nawakumbusha tu kufanya homework, kama ulisahau...
Lunch itakua ishaliwa, mdau ameshashiba, kama ilisahaulika, basi homework ifanyike, ili kesho asitoe hadithi ya mbuzi kala daftari langu kwa ticha!

Hizi homework si za watoto tu, na wazazi tunahusika...fanya naye, hata kama wa sekondari jihusishe kwenye anoyojifunza, ili ujue ana uelewa gani...hata kama una elimu ndogo kuliko yeye, ukisoma hapa basi si unajua kusoma, basi soma naye somo la Kiswahili, ukiwa artistic kama kina mie, basi msaidie hata kupaka rangi...

Sio unamwachia anko, anti, sometimes dada kila siku...au mama kumwachia baba, or baba kumwachia mama kila siku--hafai. Afu akipata zero unashangaa, sasa kama ulikua hufatilii unaishia kujisifu tu "mwanangu ana akili, anajua bilinganya kwa kizungu, yaani full english, kiswahili hata hajui!" utajuaje            kuwa anaelekea kwenye zero???

Swali ni mmeshafanya homework leo? Kama bado FANYA sasa!



Tuesday, May 15

Feza's Mother's Day celebration

 Wamama wa watoto wanaosoma  Feza Nursery School tulialikwa Jumamosi iliyopita kwenye sherehe ya Mother's Day ambayo waalimu walituandalia.
Tulikaribishwa na mkuu wa Feza Nursery School. Ms Bushra...

...wamama tulikua wengi wa kutosha... 

 KGI, kina Xchyler, ndo walianza kwa kutuimbia...very touching song about mama...

...hapa wanasema I love you... 




Hawa ni KG III...nalifanya kama poem about mama...hapa wanasema, whatever I give you, you give it back much much more...sikumbuki maneno yote, ila maana ni kama hiyo...pia ilikua bomba sana! 

Thursday, May 10

Newton parent's day



Mdau Newton Newton wa Morogoro akijitayarisha kwenda shule....
Hii ilikua ni parent's day ya hapo shuleni kwao. Shule inaitwa Top Star Pre & Primary School, ya mji kasoro bahari, Morogoro.

...mlango school bus anajifungulia mwenyewe...

 ...cuuute...



...wanacheck ripoti zao wenyewe...



...boy is cuteee, mama is cuteeeer... Kupendeza muhimu parent's day...

Unashiriki maisha ya shule ya mwanao, unahuthuria parent's days, au unatuma 'dada', au anti/anko?



Wednesday, May 2

Matokeo ya Form VI 2012 - Ni Marian Girls tena...

Matokeo ya Form VI yashatoka, kama kawaida wadada wa Marian Girls ya Bagamoyo wamewaburuza tena...ntawaupdate top ten baadae kidogo...

Haya hizi hapa...

TOP TEN SCHOOLS:

1. Marian Girls - Pwani
2. Feza Boys - Dar
3. Kisimiri - Arusha
4. Kibaha - Pwani
5. Ilboru - Arusha
6. Mzumbe - Morogoro
7. Msalato - Dodoma
8. Tabora Boys - Tabora
9. St Mary's Mazinde Juu - Tanga
10. Consolata Semonary - Iringa

Top 5 Sayansi:



  • 1. Fauth Asenge - Marian
  • 2. Zawadi Mdoe - Feza Boys
  • 3. Belnadino Mgimba - Minaki 
  • 4. Janal Juma - Feza Boys
  • 5. Immaculate Mosha - Marian Girls

  • Top 5 Biashara:



  • 1. Alex Isdor - Kibaha
  • 2. Ephraim Tumwindike - St Joseph's Cathedral
  •  3. Vaileth Mussa - Weruweru
  • 4. Selemani Manyiwa - Kibaha
  • 5. Husein Issa - Azania

  • Top 5 Lugha Art:



  • 1. Faridi Abdalla - Mpwapwa
  • 2. Jema Rwihura - Weruweru
  • 3. Mariam Hincha - Weruweru
  • 4. Neema Mbandwa - Igawilo
  • 5. Hemedi Hussein - Tosamaganga


  • Ila kupata matokeo yote BOFYA HAPA


    Wednesday, September 15

    Xchyler day one shule


    Xchyler, aka X aka Kaila ameanza shule mwanzo wa mwezi huu...tarehe 1 September.


    Shule ni St Joseph's Kindegarten School...kama ulisoma Forodhani basi ndio hapo hapo!

    (Akirudi home na bibi)
    Najua tu mtajiuliza kisa cha kuchelewa kuwapa habari hii, kiukweli siku hiyo tulienda tu kuangalia kama kuna nafasi, maana nilikua nasafiri kesho yake (trh 2) bahati nzuri kukawa na nafasi moja tu, basi hapohapo akavalishwa uniform afu akaongoza darasani...Sister alidhani atatulilia, wapi, ndio kwanza yuko, 'Bye mama, Bya dady'...keshaona wenzake!!!
    Pia nilivyosafiri nilisahau kuondoka na memory card, na sikujua niliiacha wapi, imetafutwa muda mrefu kabla haijapatikana last week...ila nikaamua nivute zaidi wape habari hiyo leo....
    ...sababu, leo, Mr & Mrs Mapunda, tunatimiza miaka mitatu (3) ya ndoa yetu! 
    Hivyo, mama na baba Xchyler, tunachukua nafasi hii kuwashukuru wooote waliofanikisha harusi yetu miaka mitatu iliyopita, na kwa wote wanaoendelea kutupa moyo na kutuunga mkono kwenye maisha yetu ya ndoa. Pia tunawashukuru wazazi na ndugu zetu (siblings) kwa mwongozo na mapenzi makubwa kwetu na mwanetu!
    Na mwisho tunamshukuru Mungu kwa kutujalia maisha yenye mapenzi na kutujaalia furaha ya maisha yetu, Xchyler, na tunaendelea kuomba azidi kutuzidishia baraka kwenye maisha yetu.
    Aksanteni wote.

    Wednesday, July 28

    Kayla day one shule

    bigggg smileeee....Mdau Kayla Mgula akichakelea siku ya kwanza ya shule...

    unaambiwa siku hiyo alikuwa na furaha ile mbaya hakubembelezwa kuoga wala kunywa uji.

    bye mommy...
    hapa ndio shule penyewe sasa...

    Mama na Mwana wanamwambia mdau aendelee na moyo huohuo wa kupenda shule, kwani elimu ndio ufunguo wa maisha.

    Friday, April 30

    Matokeo Form Six: Ni Marian Girls tena

    Shule ya Marian Girls inaendelea kuongoza kwenye matokeo ya mitihani ya taifa ambapo imeongoza kwenya matokeo ya kidato cha sita mwaka huu yaliyoangazwa  leo mchana.

    Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako amezitaja shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 30  na zaidi kuwa ni:
       1. Marian Girls (Pwani)  
       2. Mzumbe (Morogoro)  
       3. Uru Seminari (Kilimanjaro)
       4. Kibaha (Pwani)
       5. Feza Boys (Dar es Salaam)
       6. Tabora Boys (Tabora)  
       7. Tukuyu (Mbeya)
       8. Kifungilo (Tanga)
       9. Ilboru (Arusha)  
      10. Malangali (Iringa)

     Kwa upande wa shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 30 ni:
       1. Rubya Seminary (Kagera)
       2. Maua Seminary (Kilimanjaro)
       3. St. James Seminary (Kilimanjaro)
       4. St. Joseph Kilocha (Iringa)
    5. Dungunyi Seminary (Singida)
       6. Same Seminary (Kiliomanjaro)
       7. Usongwe (Mbeya)
       8. St. Peter’s Seminary (Morogoro)
       9. Viruka (Dar es Salaam)
       10. Vwawa (Mbeya)

    Ndalichako alizitaja shule kumi zilizoshikilia mkia katika kundi la shule zenye watahiniwa 30  na zaidi  kuwa ni High-View International (Unguja) Fidel Castro (Pemba), Sunni Madressa (Unguja), Neema Trust (Dar es Salaam) Mtwara Technical (Mtwara), Mureza (Tanga), Tarakea (Kilimanjaro) Uweleni (Pemba), Arusha Mordern (Arusha) ya kumi kutoka mwisho ni Maswa Girls (Shinyanga).

    Katika kundi la shule zenye wanafunzi pungufu ya 30, ya mwisho kabisa ni Nkasi (Rukwa), Maont Kilimanjaro (Kilimanjaro), Mbarali Preparatory (Ungunja), Lilian Kibo (Dar es Salaam), Ghomme (Dar es Salaam), Adolec (Kagera), Mzizima, Dar es Salaam Christian Seminary na EDP Royal za Dar es Salaam na Sekei ya Arusha.

    Monday, October 5

    Best Wishes Form IV

    Mama na Mwana pamoja na wadau wote tunawatakia kheri wanetu, wadogo zetu, dada na kaka zetu wote wanaoanza mitihani ya Kidato cha Nne leo hii.

    Wizara ya Elimu imesema kuwa jumla ya wanafunzi 351,958, wavulana 183,755(52.2%) na wasichana 168,203 (47.8%) wanafanya mtihani huo leo.

    Kila la kheri woooote!

    Thursday, May 21

    Mbagala sio mabomu peke yake...


    Wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Maendeleo huko Mbagala Kuu karibu na mabomu wakifanya mtihani wa moko jana. (Picha hisani ya BongoPicha)
    *****
    Kufanyia mtihani chini sio kwa ajili ya mabomu, ni tatizo la siku zote, walimu kwa kutumia akili zao (ambazo mimi zimenishangaza) waliamua wanafunzi hao wafanyie mtihani huo wa moko chini kwani darasani wanakaa wanne wanne kwanye dawati moja, so watagelezeana.
    Mimi nna uhakika mtiani wenyewe, neshno, hawafanyii chini, sasa sielewi kwa nini hao walimu wasiwape homework za kutosha wanafunzi wengine woote, ili darasa la saba wafanye mtihani kwa raha, maana moko ni kipimo cha mtihani wa kweli, hapa mwanafunzi hawezi hata kupim spidi yake, na lazima yaje matokeo mabaya, ambayo yanaweza kuvunja moyo wanafunzi wengine wakaona wao ni wa kufeli tu.
    Huu uamuzi wa walimu hawa umenisononesha sana.