Showing posts with label Xyleen. Show all posts
Showing posts with label Xyleen. Show all posts

Friday, January 18

Zulu ana-make news

Kiukweli nilikua sijaiona hii...hizi ni enzi zile Xyleen akiwa anaigiza, alikua anaitwa Zulu.

Zulu is not his real name and he is actually a she – Xyleen Mapundo. Xyleen is not Ngwallo’s baby; she belongs to a colleague named Jiang Alipo. This is not a studio, it’s the home of Robert Lawlor, a veteran TV producer and Cuso International media volunteer in Tanzania.

some yote hapo: ZULU

Monday, January 7

My motherhood favourate things!

Happy New Year, jamani msharudi au bado mko holiday?Mie niko full hapa...
Juzi kati nilikua nasoma article ya favourate things za Oprah, nikapata wazo (call it kukopi na kupaste if you like LOL) mimi favourate things zangu ni zipi?

Nimezilist hapa, kizuri kula na wenzio, kibaya... nazitumia kila mara, nazipeeeeeenda balaa!

Organics Shea Butter detangling hair lotion

Ningejuaje bila kuwa na binti...afu nikapata mtu anayepractise ya kizuri kula na wenzio...Nimenunuliwa na workmate, Anna Temu (mama LeRoy & Lakisha), kuchana nywele sio issue tena, acha nifuge afro la mwanangu mie kwa raha zangu maana nywele keshapewa na bibi'ye!
Thanks Anna (mwenyewe anadai analipia mahari taratibu)

UNATAKA KULA NAMI VIZURI VINGINE? ZAMA NDANI...

Monday, December 31

Surprise- Xy kabatizwa!

...Yes, X-mas hii tulikua kwa bibi Mbingaaaa! 
Siku ya mkesha wa X-mas, wakati wakristo duniani kote wakisubiri kusherehekea birthday ya Yesu, mwanangu alizaliwa katika Kristu....
Xyleen akabatizwa kanisa lile lile alilobatiziwa baba yake na kaka yake!!!

...Hapa na mama wa ubatizo...
...final touches...kila mtu lazima apendeze...

 ...baba alikua na double duty...mpiga kinanda na baba wa mtoto anayebatizwa...
 ...maji ya baridi  na baridi la Mbinga balaa...!

...Big Brother alikua ni fujo mwanzo mwisho!

 ...akiwa na Bibi Keko...

 ...na mam...

At last binti yangu alizaliwa kwenye Krisu na kuwa mkristu kamili kwa jina la Lerato Xyleen Mapunda...

Saturday, December 29

Onja: Xmas tulikua Mbinga!!!

X-mas ya Mbinga hawatumii miti ya plastic...kitu cha kujikatia mwenyewe on Xmas morning...Xchyler akiwa na cousin bro, Raphael baada ya kukata matawi ya kutosha!

 Xyleen alideka sana...kila saa 'bebee'...
 hapa yuko na cousin sister, Lisa...


...maembe yako mengi sana...toka mtini hadi mdomoni! 

...Xchyler akiwa na cousin, Felix, wakicheza na mbuzi! 

...ingawa kibaridi cha December sio kikali kama cha September (tulipoenda two years ago) ila kipokipo...so kuota moto muhimu...Xchyler akiwa na cousin brothers...dogo alijifanya anajua kila kitu hadi kuchochea moto!!!

 ...kama wewe ni mdau wa zamani unamkumbuka huyu mbwa...anaitwa Zuma, Xchyler alifurahi sana kumuona tena...
...akamuintroduce to sister...Binti alikua anamuogopa, actually chochote chenye miguu minne kilikua kinaogopewa, huku anatamani kushika...anaita 'duduuu'

...at last ilibidi tuagane tu...we real had great time, no wonder wachaga hawaachi kwenda kuhesabiwa, na sisi ndio tumeanza mwaka huu, tuna mpango wa kuendeleza,kila december tunaenda kuhesabiwa kwa bibi Mbinga while bonding with cousins, sister n brothers!

Mo pictures coming...subiri suprise ya yaliyojiri huko!!!

Thursday, December 20

Kina X on the way to Mbinga

Haya Xchler na Xyleen on their way kwa bibi na babu Mapunda. 
Wanaenda kuhesabiwa.
Wasalimieni bibi na babu. Mtuletee zawadi ya picha.

Tuesday, November 20

Am counting my blessings!

These are my blessings I count everyday n  thank God for them sana sana sana.
Kila siku nikilala nao na kuamka nao salama, ni amani sana moyoni kwangu hata kama mfukoni sina kitu! With these three sihitaji zaidi!

Ila...ile ligi bado inaendelea...now that tumefunga hesabu...nani katoa fotokopi?

Monday, November 12

Xy's One year photoz

...hii ndio picha niliyompiga kwa ajili ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja.

Vipi...ningeingiza kwenye shindano la photogenic Bebi ingeleta mchuano?




...hapa ndipo moyo wangu unapodunda! 

Tulipiga picha nyingi...Bofya hapo kushoto kuziona...Bahati mbaya mlengwa hakuwa kwenye mood...so hamna picha aliyocheka na pipi ndio ilikua inamfanya asilie!!!

Thursday, November 8

Circus Mama Afrika ilikua bomba sana!

Kwa sasa imeshaisha...lakini je ulipata nafasi ya kuhudhuria Tigo Mama Afrika Circus?
Nilienda na wadau kibaoooo...na ilikua bomba sana, wote tulienjoy,wakubwa na totoz.

 Harrieth, Xchyler na Xyleen (yuko bize na kinachoendele mbele...

...hizo red lips ni pipi tu... 

Thierry naye alikua na baba na mom...Josh na Janet. 

...kuna time mtoto aliitwa mbele kushiriki kupiga ngoma... 

...Xchyler alitamani sanakwenda kupiga ngoma...hadi akasogea mbele kabisa...ila haikuwezekana...

 Haroon, mdogo wake Harrieth akiwa na baba na mom, Edward n Regina...

...makofi tafadhali....

 ...kwa kweli ilikua bomba sana,...kama ulikosa this time, usikose next time...kama ulienda najua hutakosa, as mie sitakosa...

Thursday, August 30

Xy's birthday - Onja

...hii ndo tam tam yenyewe...Yes, tweety, nilimchagua mam'tu, since binti hana uchaguzi kwa sasa... 



 ..part hii hakuipenda sana...

...biggie tulimpick toka shule moja kwa moja kwenye birthday, na uniform zake! 


...brothely love...

Wednesday, August 29

Happy, Happy Birthday My Girl

Binti yangu, mrembo wangu, malaika, princess aka Binti Mapunda...
Wazazi wake tunamwita Xyleen Lerato Mapunda...
Kaka mtu  anamwita Schai-Schai...
Babu yake anamwita Lerato/Rato...
Kwenye Fema TV Talk Show anaitwa Zulu...
Kwa ufupi mwite Shy...
Anatimiza mwaka mmoja leo!
Mungu anipe nini...
Nashukuru sana kwa kupata binti, ambaye kila siku ananifundisha kitu kipya juu ya kuwa mama.

PS: Hamna sherehe...n'tamfanyia vile anavyopenda zaidi; nitashnda naye siku nzima na kumtoa for lunch!

Friday, June 29

Likizo hii tulikua Mikumi!

Hata sijapiga hodi, ila kwa taarifa tu kwa wadau wa mji kasoro bahari ni kwamba wiki hii yooote toka  Jumapili tulikua mjini kwenu (tuko hadi Jumapili) na itabidi mtuzoee tu, maana daddy kahamia Moro, so this is our second home, n we r loving it...




So Jumanne tukajimuvuzisha Mikumi, utalii wa ndani. Xchyler alikua very exited kuona wanyama, hasa giraffe maana ndio his fav animal, Xyleen alikua wala hajui linaloendelea kashangaa tu amekurupushwa usiku wa manane. Ndio, ukitaka kuwafaidi wanyama aitha uende asubuhi sana au jioni sana, tulichagua asubuhi sana! So tumeingia tu kwenye gari, totoz wote usingizi!


kuona yaliyojiri huko mbugani bofya hapo kushoto...

Sunday, June 10

I believe I can fyl...

...angle hii ya picha ni nzuri sana...jaribu mtoto ambaye haogopi, picha inakua nzuri sana, acha huyu binti yangu anayeogopa utadhani kaambiwa ntamwachia... mpigapicha akipata timing nzuri afu ukamrusha kabisa anaonekama kama anapaa...jaribu afu nitumie hiyo picha kwenye mamanamwana@gmail.com
Jumapili njema.

Friday, June 8

Mnafanyaga streaching kwa watoto?


Hii ni muhimu kwa watoto jamani...hasa wachanga, (maana walijikunja for 9 months tumboni) ingawa wao unawafanyia taratibu, kama massage, Xyleen imebidi tu azoee tu, maana alikua hapendi kabisaaa...hapa yuko na bibi... big boi Xchyler alikua anapenda sana...

Monday, June 4

Onja Dar Zoo


 Jumamosi tulitoka na watoto wetu...Totoz Day Out...tukaenda Dar Zoo...yaani usipime...

Regina na watoto karibu wote... picha zote nawamwagia later...now subiri nifanye kazi za mzungu!

Wewe ulifanya nini na mwanao weekend iliyoisha? Nitumie pichaz tu-share na wenzetu hapa!