tumehama

Showing posts with label Baby Fashion. Show all posts
Showing posts with label Baby Fashion. Show all posts

Monday, January 7

My motherhood favourate things!

Happy New Year, jamani msharudi au bado mko holiday?Mie niko full hapa...
Juzi kati nilikua nasoma article ya favourate things za Oprah, nikapata wazo (call it kukopi na kupaste if you like LOL) mimi favourate things zangu ni zipi?

Nimezilist hapa, kizuri kula na wenzio, kibaya... nazitumia kila mara, nazipeeeeeenda balaa!

Organics Shea Butter detangling hair lotion

Ningejuaje bila kuwa na binti...afu nikapata mtu anayepractise ya kizuri kula na wenzio...Nimenunuliwa na workmate, Anna Temu (mama LeRoy & Lakisha), kuchana nywele sio issue tena, acha nifuge afro la mwanangu mie kwa raha zangu maana nywele keshapewa na bibi'ye!
Thanks Anna (mwenyewe anadai analipia mahari taratibu)

UNATAKA KULA NAMI VIZURI VINGINE? ZAMA NDANI...

Friday, May 25

Just cuuuute...

Anaitwa Jill, tulimuona kwenye picha za Mother's Day na mama yake Christina... 


 this girl is just toooo cuuuute!

Binti zetu...

Usiogope kusikia binti, wakati ndo kwanza mwanao ana miezi saba kama Cleopatra wangu, Yessss miaka kadhaa ijayo watakuwa mabinti warembo wenye kujitambua na kujipenda.

hawa wako kama wadoli...unapenda binti yako awe kama mdoli-doli? au ...
Je umemuandaaje mwanao wa kike ili atakapokuwa binti awe jasiri na mwenye kujiamini?
Je umeshawahi kuwaza unajipangaje kumjengea mwanao wa kike ujasiri na kujiamini?
bofya hapo kushoto tujadili hili...

Sunday, April 22

Mtoko wa Jumapili

...hya ni mapigo ya mtoko wa Jumapili chachi...Mdau wa Same ametoka mchicha na smart kichizi!!!
Jumapili njema.

Saturday, April 21

High heels na matumbo yetu vipi?



Check size ya hayo matumbo ya JLo (juu) na Jessica Simpson (chini) afu check urefu wa hizo heels...ni kweli wanakua wanatoka mlangoni na kuingia kwenye gari, wanashuka kwenye gari mlango huu hapa...ila duuuuh, is this not dangerous?
Na sie tunaotaka kutoka sambamba nao; wakivaa leopard print tunao, sijui BF watch na sie tumo, inakuaje hapa? tunakopi na kupaste au haya mengine tunapotezea?





Thursday, April 12

David & Noah wanamodel Denmark


Mnawakumbuka wadau hawa pacha wa-cuuute wa kaka yetu, Frank Manata wa huko Denimark. Wamekua wakaka sasa, wana miaka mitatu na hawataki kuchelewa washaanza kuzi-make..

...cuteness pays....



Yap, kwa kutumia u-cute wamepata kazi ya kumodel nguo za Danish brand inayoitwa KOOLS Jeans... wana jeans kali kama mnavyowaona wadau walivyopendeza.


 Kwa kweli huwa sijui yupi ni yupi...ila ni David & Noah.

Picha zaidi BOFYA HAPA



Sunday, April 8

Hairbandsss za Xy (Shy)

Binti yangu kwenye graduu ya dady...hairband ilimtoajeeeee?
Kuna mdau aliomba kujua zinakopatikana hairbands hizi za watoto ambazo Xy has been rocking kwa kila mtoko wake, iwe kliniki, bichi au kwenda kwa bibi...na si utani zinampendeza mtoto yeyote wa kike, awe na manywele au upara, zinawatoa mchicha tu.
Xy ana design nyingi, za kitai au kiua pembeni kama hii, zenye stones na kadhalika (picha za zingine hata sizioni).
Anyway, mie zote nimenunua au nimepewa na mtu aliyenunua duka linaitwa Zero 2 Twelve, hii nilipewa na mwenye duka baada ya kununua mazagazaga mengine na kuishiwa hela--chezea shoping ya watoto-- wamenihudumia tangu nna kitumbo, kwa kweli nnazimia service zano kichiziii!
Duka hilo kuuubwa lina mavitu ya ukweli ya watoto kuanzia mwaka 0 hadi 12, wa kike na wa kiume...
Duka lipo complex yenye Nyumbani Lounge (kwa Jide), linatazamana na Nyumbani, na huwa liko wazi hadi saa 2 usiku weekdays, so unaweza pita hata ukitoka job jioni...just make sure una hela ya kutosha, usije ukaishiwa kama mie...

Friday, November 5

Kutana na Willow

Anaitwa Willow, ni product ya Will na Jada Smith...alianza kuonekana kwenye cover la kitabu cha ma'mtu...then tukamuona na style za ajabu za nywele hadi mavazi (nnachopenda ni nguo zinafaa kwa umri wake as zinamcover)...now ametoa wimbo wake mpyaaa, Whip my Hair umenikaa kichwani si mchezo...huyu ana kila dalili ya kuja kuwa super star!

 

...na hii ni style ya nywele inayonekana mwanzo tu wa wimbo wake...kama nayo naizimia vileeee, kwa kuiangalia tu, not wearing it.


 
Hii style ya suruali nimeipena flan...hadi za watu wazima zipo, so mafashstonista msiogope kujimwaga na wanenu, kwenye mini me kwa suruali hizi... wikend njema!


Thursday, August 12

Nasri na swaga za suti!

Tumezoea kumuona na t-shit na jeans...leo kaja na suti ya ukweli!!!afu yuko serious!

....apendedhaaaa...

...suti zina mapozi yake jamani!!!

Saturday, May 1

D natural vs D wigi

Hapa mdau Dories Nkone aka D akiwa na nywele zake natural...

Hapa akijaribisha wigi la mama home...

Mi nimepanda nywele zake za ukweli, maana ni nzuri, hili wigi, amwachie mama tu, au wadau mnasemaje?

Tuesday, January 19

Yeboyebo hadi Hollywood!

Huwa sipendi kuweka picha za masupasta wa Hollywood hapa, maana naona wanaonyeshwa vya kutosha hii ni kwa ajili ya wanetu, ila hii naomba tu mnisamehe.
Angelina Jolie akiwa na wanae, Shiloh (aliyebebwa), Pax (kushoto, mwenye black) na Zahara (wa kati, mwenye pink) akiwapeleka shopping.
Kilichonifurahisha ni hicho nilichozungushia; yeboyebo! alizotinga bibie Shiloh.
Akivaa X hapa kuna wataoona nimefulia, ila yeboyebo zinapendwa sana huko nje, maana ni rahisi kuvaa na kuziosha, pia ni simple, na off course ni cheap!
Hata mimi nazizimia kichiziiii, X anazo, ila sio exactly kama hizi, yeye anaogea zake, na anajua zinaitwa yebo!

Thursday, December 3

Unywele wa Uwera

Mdau Mpya, anaitwa Uwera Getrude, mi napenda pozi zake, ni kama model wa ukweli.
Ila zaidi ya yote ni hizo nyweleee, ni ndefu na nzuri sana. Pamoja na kujaaliwa na Mwenyezi, nna uhakika matunzo ya kuzifanya zipendeze na kushine kiasi hicho ni kazi ya mama.
Hongera mam'tu, nywele za mdau zimekubali.

Hapa Uwera amezisokota mbele na kubana nyuma (toto style) na pozi zake zile zile za kimodo!
Apendezhaaaaa!

Saturday, October 31

Vallencia ndani ya makeup za mama

M-cute Vallencia akitoa tabasamu kali baada ya kujiremba na makeup za mama yake, Lulu Kilonzo. Kapatia kumetisha rangi ya shedo na kitop!

Saturday, September 19

Aurelia's Hair -do

Mdau Aurelia akiwa amepozi, nimependa hapa amependeza sana, na hasa hizo nywele ambazo huwa hataki ziguswe, naona siku hiyo aliamka vizuri zikapendezeshwa.

Saturday, February 28

Sare Sare Maua - X na Brian

X akiwa na nguo zake, hizi alipewa na aunty wake flan hivi anaitwa Love (Irene Peter) alivyokua mchanga, zikaanza kumtosha alipofika miezi sita kama kwenye hiyo picha. Ila mwanangu hapendi cap, ukimvalisha anaivua, so huwa simvalishi na cap yake.

Hii picha ya Brian Kamugisha akiwa na nguo kama hizo nimeipata juzijuzi tu, naona tofauti ni randi za hizo nguo, ambayo nimeiona baada ya kutaka kuzitumia, nilidhani zinafanana kila kitu. Naona Brian mtoto mtulivu, amevaa ca bila tatizo.

*Kwa jinsi watoto wetu walivyopendeza na hizo nguo, inabidi Nike wawatumie kwenye matangazo, haki ya nani tena.*



Friday, January 30

Saturday, January 24

Mrembo Violin

Mrembo Violin Hasitu (2yrs) looking B-E-A-U-Tiful in White. Kuna mtu ana bisha juu ya u-beauty wa mtoto huyu?

Saturday, January 17

Hii Ndio Iko On Fashion Watoto wa Kike?


Dorice
Lightness Lazaro

Glory

***
Kama mnavyo waona hao mabinti hapo juu, gauni limemetishwa na kofia juu. Si utani wametoka mchicha, ila mi sina mtoto wa kike so nauliza kama hii ndio fashion mpya maana sitaki kuachwa nyuma na fashion hata kama ya watoto nataka niijue.


Saturday, January 10

Mwanamke Nywele...

Mtoto Sarah Gingi kweli nywele amejaaliwa na mamamtu, Ericka, anajua kuzipamba, gauni jekundu vibanio vyekundu, she is sooo cuuute!