
Angelina Jolie akiwa na wanae, Shiloh (aliyebebwa), Pax (kushoto, mwenye black) na Zahara (wa kati, mwenye pink) akiwapeleka shopping.
Kilichonifurahisha ni hicho nilichozungushia; yeboyebo! alizotinga bibie Shiloh.
Akivaa X hapa kuna wataoona nimefulia, ila yeboyebo zinapendwa sana huko nje, maana ni rahisi kuvaa na kuziosha, pia ni simple, na off course ni cheap!
Hata mimi nazizimia kichiziiii, X anazo, ila sio exactly kama hizi, yeye anaogea zake, na anajua zinaitwa yebo!
4 comments:
Mwe!huyu ZAHARA mbona yuko tofauti na wenzie jamani?ni mwanae wa kumzaa kweli? hebu nifahamishe mamii kama una information kuhusu hilo!
Kuuliza si ujinga.
Zahra si mwanaye wa kumzaa, huyu dada Mungu anamuongezea kwa sababu anatoa sana. Hao weningine ni watoto amechukua anawalea tu.
YEBOYEBO.
Wabongo ukiwafuata hutavaaaa.
mimi huvaa kile nafsi yangu imeridhika nacho hata kama wengine hawapendi.
disminder
Hapo mtoto wa kumzaa mwenyewe ni huyo aliyebebwa tu, Shiloh.
Zahra na Pax waote wameasiliwa(adopted).
Zahara anaonekana tofauti sana maana yeye ni mwafrika, toka Ethiopia, alimchukua wakati ana miezi 6.
Pax anatokea Vietnam.
Jumla huyu mmama ana watoto sita.
Huyo Shiloh alizaliwa Namibia (2006).
Mwanae wa kwanza, hayupo kwenye hii picha anaitwa Maddox, sasa ana miaka tisa, alimchukua akiwa na miezi saba toka Cambodia.
Pia 2008 alizaa watoto wengine mapacha, Knox (wa kiume) na Vivien (msichana.
Hii familia huwa wanaiita familia ya Umoja wa Mataifa, maana kuna watoto toka nchi nne tofauti, na hata hao wake hawajazaliwa marekani, hawa mapacha wamezaliwa Ufaransa!
Kwa ufupi ni hayo,maana Angelina naweza nikamuandikia page nzima kwa mambo yake, mazuri na mabaya!
Nimeipenda hiyo dada yangu hata mimi kwakweli nazipenda yeboyebo kwanza zinaosheka kirahisi kwahiyo unaweza kufanya mwanao awe smart wakati wote hata Ryan na Ronald wanazo tena exactly kama za mtoto wa Angelina kasoro rangi tu, kwahiyo ndugu yangu usijali macho na midomo ya watu fanya kile unachoona ni sahihi kwa mwanao.
Post a Comment