Showing posts with label HIV/AIDS. Show all posts
Showing posts with label HIV/AIDS. Show all posts

Thursday, February 23

HIV/AIDS test


Wapenzi wa blog hii naimani ratiba hii mtaipenda sana kwakua ipo
katika lugha ya kiswahili na vyakula ni vile vile vinapatika nyumbani
tanzania na kwingine kokote dunianai kwa urahisi sana hata kariakoo
sokoni vyote vinapatikana kwa bei nafuu.

Mafunzo jinsi ya kuandaa kila siku tutakua na funzo la siku hiyo
nitaweka post kuaznia leo kwa ratiba ya Jumatatu (leo) tembelea blog kwa
maelezkezo jinsi ya kuandaa www.activechef.blogspot.com

Nitaweka mafunzo jinsi ya kuandaa kuanzia mwanzo mpaka mwisho na
mahitaji yote pia nitaweka list ya vitu vyote unavyotakiwa kununua kwa
wiki nzima pia ukiniambia idadi na umri wa mtoto ninaweza kukuambia
bajeti ununue kiasi gani ili chakula kisikae sana na kisiharibike.

Nawatakia siku na kazi njema
Chef Issa

Tuesday, December 1

Siku ya Ukimwi Duniani: Mzazi timiza wajibu wako, namba hizi zipungue


Leo ni siku ya Ukimwi duniani, well, kila mtu anajua hilo, basi mimi nataka nikwambie vitu ambavyo inawezekana hujui, kuhusiana na Ukimwi na watoto Tanzania, takwimu hizi ni hadi kufikia mwaka 2007.
  • Watoto 140,000 walikua wanakadiriwa kuwa wanaishi na vijidudu vya Ukimwi
  • Jumla ya watoto yatima 970, 000 wazazi wao walifariki kwa Ukimwi
  • Inakadiriwa kuwa wanawake 760,000 (wenye miaka 15+) walikua wanaishi na Ukimwi, hivyo kuhatarisha maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto
Hiyo nguo (mi naiitaga kinyelamumo, sjui wengine mnaitaje) imeandikwa
UKIMWI: Ni tatizo la kila mmoja.
Wazazi tuepushe tatizo hili kubwa kuwa la watoto wetu kwa:
  • Kupunguza maambukizi baina yetu, ili tusiwafanya wawe yatima wa Ukimwi
  • Kupunguza maambukizi ya mama-kwa-mtoto, ili wasizaliwe wakiwa wameshaambukizwa Ukimwi
  • Kupunguza maambukizi ya Ukimwi kwa vijana, kwa kuwaelimisha watoto wetu juu ya janga hili tangu wakiwa wadogo
  • Kuwatunza na kuwalea vizuri ndugu, jamaa na marafiki wenye Ukimwi, na pia yatima wa Ukimwi
Love, Jiang.

Friday, February 20

Wadau Tunaomba Mchangie Hili

Poleni na shughuli.
Nimeona niwaandikie kwani maswali niliyonao yanaweza tatuliwa vyema na mawazo ya wadau katika blog zenu.
Nitashukuru sana mkinisaidia.kuna utafiti mmoja wa kisayansi unafanyika hapa tanzania,kwa bahati nzuri na mimi nashiriki,nimekumbana na suala moja ambalo (halihusiani na utafiti) lakini katika hisia zangu nimeona ni tatizo hivyo napenda wadau tulifikirie wote.
Amini usiamini kuna watoto kati ya umri wa miaka 7 mpaka 15 wameathirika na ukimwi na wanahudhuria mahospitalini kuchukua dawa lakini hawanataarifa kama ni waathirika na hawana elimu yoyote kuhusu ukimwi zaidi ya kusikia maredioni na kwenye TV tena kidogo mno.
Je ndugu zangu ni haki kuendelea kuwaficha au ni bora waambiwe maana tukumbuke ni wanetu,wadogo zetu,na pia tusikatae michezo mingi tu hatarishi inaendelea huko mashuleni na mitaani.
Tafadhali kaka michuzi na dada jiang naombeni muirushe hewani natumae itawasaidia wengi.
Nitashukuru tu nikiona maoni hakuna haja ya kutoa contact.
Akhsanteni na kazi njema.

Monday, February 2

Mtoto wa Kiume Atahiriwe Akiwa na Umri Gani?

Poll yetu ya kwanza kabisa ya mtoto wa kiume atahiriwe akiwa na umri gani imefungwa rasmi tarehe 31 january.
napenda kuwashkuru wale wote walioshiriki kupiga kura pale wanapoona ndio chaguo lao.
Hadi inafungwa poll hii ilipigiwa kura na watu 127.
Matokeo ya Mtoto wa Kiume Atahiriwe Akiwa na Umri Gani? ndio haya.
Kabla ya Arobaini: 41 (32%)
40 hadi Miezi Sita: 33 (25%)
Chini ya Miaka 2: 25 (19%)
Zaidi ya Miaka 2: 13 (10%)
Atajua Mwenyewa Akishakua: 15 (11%)

*****
Kutahiri kwa wanaume ni kuondoa kwa ngozi ya mbele ya uume. Utafiti wa mambo ya kale unaonyesha kuwa ilikua inafanywa tangu enzi za Misri ya Kale.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakadiria kuwa asilimia 30 ya wanaume wote duniani wametahiriwa, ambapo kati yao, asilimia 68 ni waislam.

Kuna utata mkubwa hasa kwenye nchi zilizoendelea kuhusu kutahiriwa. Wanaounga mkono wanasema kuwa maumivu ya kutahiriwa ni kidogo ukilinganisha na na faida za kiafya zinazotokana na kitendo hicho.

Wakati wanaopinga suala hilo wanadai kuwa lina madhara kiafya hasa katika kujamiiana, na wanasema linakiuka haki za binaadam linapofanywa kwa mtoto ambaye hashiriki kwenye maamuzi hayo.

Utafiti na WHO wanakubaliana kwamba kutahiri mtoto wa kiume kunapunguza kwa kiwango kikubwa uwezekano wa wanaume waliotahiriwa kuambukizwa virusi vya ukimwi.
*****
Kwa kweli nimekosa utafiti unaoonyesha lini ni vizuri kutahiri mtoto ingawa watu wengi pamoja na madaktari wanasema ni vyema kumtahiri mtoto akiwa mdogo ili kupunguza maumivu as mtoto mdogo anakuwa bado hajui maumivu, au kitaalam wanasema senses zake zinakuwa mbali, bado hazijawa fully formed, ingawa huko nchi zilizoendelea wanasema kwamba maumivu hayana tofauti kati ya mtoto na mkubwa.

Nikiwa mama wa mtoto wa kiume, na mtu ambaye kwa kiasi kikubwa nategemea sana ushauri wa kitaalamu kufanya maamuzi yaliyosahihi, wataalam hawajanisaidia kabisa katika suala hili, hivyo basi ntatumia tamaduni zetu kufanya ninaloona ni sahihi.
*****
Narudia tena kuwashukuru wote mlioshiriki.

Poll mpya inakuja soon…