Poleni na shughuli.
Nimeona niwaandikie kwani maswali niliyonao yanaweza tatuliwa vyema na mawazo ya wadau katika blog zenu.
Nitashukuru sana mkinisaidia.kuna utafiti mmoja wa kisayansi unafanyika hapa tanzania,kwa bahati nzuri na mimi nashiriki,nimekumbana na suala moja ambalo (halihusiani na utafiti) lakini katika hisia zangu nimeona ni tatizo hivyo napenda wadau tulifikirie wote.
Amini usiamini kuna watoto kati ya umri wa miaka 7 mpaka 15 wameathirika na ukimwi na wanahudhuria mahospitalini kuchukua dawa lakini hawanataarifa kama ni waathirika na hawana elimu yoyote kuhusu ukimwi zaidi ya kusikia maredioni na kwenye TV tena kidogo mno.
Je ndugu zangu ni haki kuendelea kuwaficha au ni bora waambiwe maana tukumbuke ni wanetu,wadogo zetu,na pia tusikatae michezo mingi tu hatarishi inaendelea huko mashuleni na mitaani.
Tafadhali kaka michuzi na dada jiang naombeni muirushe hewani natumae itawasaidia wengi.
Nitashukuru tu nikiona maoni hakuna haja ya kutoa contact.
Akhsanteni na kazi njema.
1 comment:
Kwa aliyeleta mada hiyo ni safi.
Mtazamo wangu, kwa watoto miaka 7-11 wanatakiwa wasiambiwe kwa kuwa uwezo wa kuelewa mambo unakuwa bado ni mdogo na hata kumueleza kuhusu ukimiw, umetoka wapi, unavyoenea na jinsi ya kujikinga inakuwa ni kumuharakisha kujua mambo asiyopaswa,
Lakini kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka 12 kwa KIZAZI HIKI CHA SASA, wanapaswa kuambiwa kwa kuwa wanaanza michezo ya ngono mapema sana na si tu kwa wale waliokwisha pata ugonjwa kwa yoyote. Wakipata elimu itawasaidia kutopata maambukizi mapya kwa walio na VVu na kwa wasio na VVU watachukua hatua ikli wasipate. yangum.
Post a Comment