Showing posts with label Totoz Day Out. Show all posts
Showing posts with label Totoz Day Out. Show all posts

Thursday, November 8

Circus Mama Afrika ilikua bomba sana!

Kwa sasa imeshaisha...lakini je ulipata nafasi ya kuhudhuria Tigo Mama Afrika Circus?
Nilienda na wadau kibaoooo...na ilikua bomba sana, wote tulienjoy,wakubwa na totoz.

 Harrieth, Xchyler na Xyleen (yuko bize na kinachoendele mbele...

...hizo red lips ni pipi tu... 

Thierry naye alikua na baba na mom...Josh na Janet. 

...kuna time mtoto aliitwa mbele kushiriki kupiga ngoma... 

...Xchyler alitamani sanakwenda kupiga ngoma...hadi akasogea mbele kabisa...ila haikuwezekana...

 Haroon, mdogo wake Harrieth akiwa na baba na mom, Edward n Regina...

...makofi tafadhali....

 ...kwa kweli ilikua bomba sana,...kama ulikosa this time, usikose next time...kama ulienda najua hutakosa, as mie sitakosa...

Tuesday, June 5

Dar Zoo ilikua bombaaaa!

Hapa ndo tumefika na tumeshachoka hoi!!!...asikuambie mtu ni mbaliiiii balaa...ilifika point nikajua tumepotea, maana naona vibao vya shule za Kisarawe huko!!!

...hawa ni watoto karibu wote wakiwa na Regina...

...kwanza chakula...huyu ni Khreflo Mfumu akigombana na mfupa wa kuku, mwili haujengwi kwa matofali!

...Regina na malaika wake; Herrieth na Haroon...  (H)...(vidoleeee)

...Rosemary Mizizi na Kloe na Khreflo... (K)

...mie na Xchyler na Xyleen wangu (X)...kidole cha X tumekikosaje?

...kaka Khreflo akikagua wanyama...

...raha ilikua hapa sasa...

...asikuambie mtu, Arabs make it look soooo easy in movies...kupanda huyu mnyama si mchezo nilipiga kelele, Xy akanishikilia kwa nguvu, X hapo mbele alikua ngangari ( maana nilikazana kumbambia, beib usiachie, shika kwa nguvu!!!)

...Ila ride yenyewe sio issue, issue kupanda na kushuka...




...ahaaa..sasa tunapumua...ila it was a great experience, ukienda Dar Zooo make sure umepata Camel Ride!!!!

...wengine hao wakapanda...na bado wanaugulia maumivu ya miguuu lol!

...hii Xchyler aliitaka alipoiana tu...ni kibajaji cha punda...watoto walifurahi sana!!!


...Kwa kweli tuli-enjoy sana...make sure una mafuta ya kutosha!!! ni mbali haswa!!! Pia gari la chini chini halifai, kuna rough road parefu, au mtu wa I-Love_my-car, u will cry!!!  wenye watoto wadogo, pack tu uji/maziwa/vyakula vya kusaga this is like a whole day thing. Kiingilio ni kawaida tu, wakubwa 5,000 wadogo (from 2yrs) 2,000!
And, jamani usiondoke bila camel ride!

Monday, June 4

Onja Dar Zoo


 Jumamosi tulitoka na watoto wetu...Totoz Day Out...tukaenda Dar Zoo...yaani usipime...

Regina na watoto karibu wote... picha zote nawamwagia later...now subiri nifanye kazi za mzungu!

Wewe ulifanya nini na mwanao weekend iliyoisha? Nitumie pichaz tu-share na wenzetu hapa!