Wednesday, July 4

Siri ya kumfanya mwanao awe na akili: Ijue Dunia
Sio lazima uwe kama kina Jolie-Pitt ndo uwe unaweza kutembelea dunia hapana kuna njia nyingi za kuijua dunia. Hapa kinachomaanishwa ni kwamba ijue dunia hata kwa kusoma tu! Yes, ukijua kuhusu tamaduni mbalimbali za hapa nchini na duniani, utamfundisha mwanao, naye atajikuna anavijua hivyo vitu bila tatizo. Kiasi kwamba akikuta watu wanabishana kuhusu 'lazima mwanaume amtolee mahari mwanamke ili awe mkewe,' anawarushia tu bomu moja, la “mbona wenzetu wahindi mwanamke anamtolea mahari mwanaume?”, wanaona katoto kajinias! Si unajua knowledge is power!

Dunia kubwa, sijui nianzie wapi?

Rahisi, kwanza nunua ramani, prefebly ile ya duara (kama hiyo hapo pichani). Sasa hapa mnafanya kama mchezo, fumba macho, kisha mwambie mtoto aizungushe hiyo ramani, hata kama ya kawaida anazungusha tu lile karatasi, afu kidole chako kitakapodondokea ndo hapo hapo mtakapoanza safari yenu ya kuzunguka dunia kupitia vitabu/movi/lugha nk.

Cha kufanya na hiyo nchi mnaamua nyie na unaangalia umri wa mtoto; unaweza ukaamua ni salamu tu ya hiyo nchi (ukisoma hapa am sure una access na internet, hakuna kisichowezekana). So mfano kidole kimedondokea China, basi mnaamua na mwanao, kuwa wiki hii hamna salamu nyingine zaidi ya Nǐ hǎo (ndio nimejipendelea, unaweza kuta unajua maana ya jina langu, lol) na kuijua bendera ya China (kwa watoto wadogo rangi zake tu zinatosha) na ilipo duniani.

Kama ni mtoto mkubwa sasa inabidi ununue vitabu, kwa urahisi nunua encyclopedia ya nchi, kuliko kununua vitabu mbalimbali – utavimaliza? Basi mnasoma wote. Mkifanya hivyo wiki 10, tu mnakua mshatembelea nchi kumi! Mwaka una wiki 52, off course hamuwezi kutumia zote, ila mkitumia nus utu, mwaka mmoja mnakua mmeshapitia nchi 25, na dunia ina nchi zaidi kidogo ya 200, mnazimaliza in 8 years tu!

Pia nashauri, muitembelee na mikoa ya nchi yetu, isije ukawa mwenyeji sana wa dunia, afu mgeni nyumbani! Mkidondokea usukumani, basi ndio Kisukuma wiki nzima (Wasukuma nisaidieni salamu hapa, hivi ni Mwadela eeh?)


Hadi hapo tuko sawa ….kupata tips nyingine ya kuongeza akili za mwanao ungana nami same day next week. Kama ulipitwa na iliyopita, click kwenye tab ya Elimu hapo juu.

No comments: