Pamoja na kuwa wahanga wa mlipuko wa Arusha pamoja na watanzania wenzangu hatuelewi sababu wala nia au hata ujumbe aliotaka kuufkisha huyo aliyelip[ua...
Pamoja na kuelewa kwamba alirusha bomu kanisani, that is sehemu ya ibada, katikati ya ibada, akielewa fika kwamba kutakuwa na watu wa rangi, jinsi na umri mbalimbali...
Pamoja na sikitishwa na utokeaji wa tukio hili, na mengineyo yanayofanana na haya (bila kuwa na nia ya kuyaunganisha kana kwamba yamefanywa na mtu mmoja au kwa nia moja...
Ila seriousl, mtoto kama huyo, nawengine wengi walikuwapo kwenye tukio hilo, wanakua na message gani kwenye vichwa vyao?
Wakati nchi zenye vita watu huwa wanakimbilia kwenye nyumba za ibada kujificha, huyu ambaye anakua kwenye nchi yenye 'amani' afu akiwa umri huu tukio la uvunjifu wa amani linatokea akiwa kanisani aeleweje?
Seriously, hao watu waliofanya tukio hili wamefikiria wanayoyafanya...
Tusikubali, kama taifa, kupelekwa huko wanakotaka kutupeleka, as sitaki wanangu wakue kwenye nchi ya aina hiyo...kwanza hatujui hata nia yao, so tusikubali, upendo na mshikamano wetu bila kujali rangi, makabila wala DINI uvunjwe na wasiojua dhamani yake!
No comments:
Post a Comment