Tuesday, December 15

Hatimaye TFDA waorodhesha maziwa yanayoruhusiwa

At last, Mamlaka ya Uthiditi wa Chakula na Dawa (TFDA) wametoa orodha na ku-endorse (sijui kiswahili chake) maziwa yanayofaa kwa watoto, ambayo ni yafuatayo, na nchi zinazotengeneza:
  • Lactogen 1 infant Formula - South Africa
  • Lactogen 2 Follow up Formula - South Africa
  • NAN 1 Infant Formula - South Africa
  • NAN 2 Infant Formula - South Africa
  • Lactogen 1 Infant Formula- France
  • Lactogen 2 Follow-up formula - France
  • NAN 2 Infant Formula - France
  • Cow Bell Infant Formula - France
  • NAN 1 Infant Formula - Holland
(sorry, picha nimeshindwa kupata, maana nimeona zinanichanganya, so ili kutowachanganya na nyie nimeona niachane nazo).

Akiongea na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Margareth Ndomondo-Sigonda alisema kuwa mamlaka hiyo imeamu kuwa waingizaji wa bidhaa hizo lazima wapate kibali cha mamlaka hiyo kila wanapotaka kuingiza bidhaa hizo.
Pia amewashauri wananci kutumia bdhaa zilizohalalishwa na mamlaka hiyo kujiepusha na matatizo ya kiafya.
Hayo yote yalikuja kutokana na kukamata makopo zaidi ya 14,000 ya vyakula feki, yakiwemo maziwa ya watoto ya S-26 (yalishakatazwa haya), SMA, Isomil, Cow & Gate Infant Formula, Infantcare, Nutrient optium na Ifasoy.
Wazazi tujiadhari na hizi formula, nunua hayo yaliyoklua endorsed na hakikisha ni kutoka nchi zilizotajwa hapo, au kama vipi, jichanganye kwenye maziwa ya ng'ombe wa mtaa wa pili, ila kama mwanao ni chini ya mwaka mmoja, inabidi ufuate process maalum ili yamfae.

8 comments:

Anonymous said...

WEWE MAMA NAMEKUKUBALI


disminder

Anonymous said...

Mama X, naomba basi utufahamishe hiyo process ya kuandaa maziwa ya mtoto chini ya one yr

Jiang said...

@Disminder..thanx.
@ mdau mwingine...ntawafahamisha si punde, maana inabidi niisome tena nisijenikachanganya vipimo, maana X anakunywa yasiyochanganywa siku nyinig, tangu atimize mwaka mmoja...

Anonymous said...

mama x mimi natumia SMA na sijui kama imekatazwa hembu nifahamishe vizuri manake nimechanganyikiwa,nasubiri jibu mpenzi

Jiang said...

kwa kweli hawa TFDA wametoa tu orodha ya maziwa waliyoya-endorse, (jamani nisaidieni kiswahili chake!) hayo hapo juu, lakini hawajasema kuhusu mengine.
Hayo SMA kuna waliyokamata feki, yani sio yale yenyewe, sasa hawajasema kama mtu unatumia SMA ya ukweli inakuaje, ila sidhani kama ni tatizo, nadhani kama yangekua yana tatizo wangeshayakataza, kama una hakika kuwa yako ni orijino...kujua kama ni orijino nayo ishu, ila mi ntaendelea kufuatilia kujua inakuaje.

Jiang said...

@ Mdau wa SMA...nimeichunguza website yao nimeone ni kampuni ya ukweli, mi nilishaichunguzaga S-26 ilivyokatazwa ilikua kazi kuipata kwenye mtandao, afu website ikawa haieleweki. SMA nimeona wa adress UK na Ireland, so sidhani kama wana viwanda nje ya nchi hizo, ili kujua kama unayotumia ni ya ukweli, unaweza ukaanza kwa kucheck nchi yalipotengenezwa, maana hawa wanaotengeneza vitu feki sometimez ni wajinga sana, utakua wameandika uarabuni, wakati kampuni haina kiwanda uarabuni.

Anonymous said...

THANX

Anonymous said...

mimi ninayotumia ni ya Ireland hope yatakuwa mazuri,asante kwa msaada