Friday, November 27, 2009

Mcuuuuuuuute Feven

Naitwa Feven Mushi, natokea kijitonyama Dar. Napenda kucheza " Stand Up and sit down" na kuangalia cartoon and my favorites are "In the Night garden, 3rd and Bird, Boogie Bibbies, Me Too and Tractor Tom.
Hoping wadau wenzangu they do enjoy them as I do.
*****
She is sooooooooooo cuuuuuuuuuuuuute!

Wednesday, November 25, 2009

Athkah, Shaymaa na Meglaila wakiwa na aunties na bibi yao

Mdau Shaymaa akiwa anakula nchi ndani ya Zanzibar Beach Resort.

Shaymaa na dada Meglaila wakipunguza ukali wa joto.

Wadau Athkah, Shaymaa na Meglaila.

Bibi na wajukuu...naona bibi anaona raha sana ku-spend time na wajukuu.

Athkah na aunt Shangwe.
Athkah na Aunt Lara...

Wadau Athkah, Shaymaa na MegLaila wakiwa na Aunt Reyna.

Athkah akideka kwa bibi, afu kafanana nae, au macho yangu?

Meg na mam'ke, Shangwe...mi nimependa rangi zenu, chocolate!

Tuesday, November 24, 2009

Hoi, na X wangu


Hapa nilibambwa na Zeze wa 8020Fashions, nilishakua hoi na fujo za X.
X alikua ametoka kula, hii ni t-shit ya pili, ile ya kijani ni ya tatu, maana hii hakukaa nayo muda mrefu kabla hajaichafua.
Kanuna huyo maana anaona anabanwa, yeye anataka ashuke akaendelee na fujo zake...all in all, ali-enjoy sana.

Monday, November 23, 2009

Mambo ya Children's Day Jana

Jana ndio ilikua ile sherehe ya watoto, pale Diamond Jublee.
Wadau wa kutosha walikuwepo, na watoto wali-enjoy kwa kweli.
MC wa party alikua Jimmy Kabwe, namsifu kaka anaweza kusherehesha watoto, maana aliwapa raha haswa, nahisi bila yeye pasingenoga sana.
Watoto walianza kwa mashindano ya kuimba, wakawa wanapanda jukwaani kwa kuimba, unajua tena watoto wa kileo, nyimbo gani wasioijua?
Huyu hapa, jina lake limenitoka kidogo, ingawa namfahamu siku nyingi, kutokana na kipaji chake cha pekee cha uimbaji, na live anaimba vizuri zaidi.

Baadae wadau wakajimwaga stejini kuchaza nyimbo mbalimbali.
Wengi walinifurahisha, pamoja na huyu bi-dada, siku-catch jina lake, (sha ambiwa anaitwa Cassandrah, malaika wa Mange). Mrembo amemetisha kila kitu pink, na imemtoa maana alipendeza haswa.

Hawa watatu walikua wanacheza kama mstage show, yani wanachaza kwa mpangilio kwa pamoja, nao walinifurahisha sana wanavyocheza. Afu nahisi hao wakubwa ni twins, huyu mwingine ni mdogo wao.
Kama ndio hicyo, lazima wanafanya mazoezi ya kucheza nyumbani, pata picha ukiwa mzazi wao, maana lazima ni watundu tu!

Huyu mdau m-cute nae nilipenda anavyocheza, ingawa pia sikupata jina lake.

Wanamuziki wakafunga show kwa kuimba na kucheza na watoto. Hapa ni Profesa Jay, aliwarusha watoto ile mbaya hasa pale alipoimba hapo vipi, wadau wanajibu....
Wanamuziki wengine walikuwepo ni AY, Matonya, THT, na wengine hata sijashika majina yao, ila watoto wanawajua wote, na wanajua nyimbo zao.
Kwa ufupi, palifana hasa kwa watoto.

Children's Day: Xchyler akiyarudi magoma

Makofi ni sehemu ya mikogo yake...

Yuko serious kwenye kucheza, hataki utani....

Weeeweeeee, utamtaka!

Hapa sio kwamba anatambaa, ila alikua anacheza mpaka chini!

Ila mwisho aliishia kulala mikononi mwa bibi, maana si kucheza tu, X alifanya fujo sana, alikua anazurura na kukimbia ukumbi mzima, nilikua na kazi kubwa ya kukimbizana nae, kiasi kwamba hata mimi usiku nililala hoi!

Children's Day: Face paints

Mdau Faidha katoka mchicha, alimetchisha na kabegi ka pink mgongoni.

Mdau mtoto wa baba Bridgittejana nilimuona live. Na baba alikuwepo, mi niliongea na ma'mtu Consolatha Ngowi baba nilimuona kwa mbaaaali.

Huyu anaitwa Kashe (3yrs).

Iman (2yrs) kama spider man, afu alipatana sana na X, basi akawa anampa bisi zake mwenyewe, X anazila tu!

Brigdett na Faidha.

*****
Wadau mliokuwepo ntumieni picha za wadau nizitumie, mi jana nilisahau memory card ya camera yangu, so nilipiga picha chache sana, ila ningependa kutumia picha nyingi, nyi tumeni tu mi nizirushe.

Friday, November 20, 2009

M-cute Melisa/Michelle

Huyu ni mdau mpya, anaitwa Melisa au Michelle.
Ma'mtu Tulinave Lupembe anasema, 'Nampenda sana mtoto wangu mpenzi Melisa/Michelle, ni mtoto anaependa kutabasamu na ni mchangamfu, Mungu ampe maisha marefu yenye furaha tele, afya na upendo kwa sisi wazazi wake Mr. & Mrs Stephano John Mgaya wa Kimara Stop over Dar.'

Thursday, November 19, 2009

Angel akiwa Moshi kwa babu

Mdau Angel hapa yuko nadady Mika kwa babu Moshi.
Angel anasema anawapenda wooote!

Siku ya watoto

Mdau unakaribishwa kwenye hafla hii ya red ribbon jumapili hii ukumbi wa diamond jubilee hall jijini dar, ambapo mali na wasanii nyota kutumbuiza, wabunifu wa mitindo wote watapanda jukwaani kucheza mitindo mbalimbali ya dansi.

Wednesday, November 18, 2009

Colman na Aunt Angel

Colman Francis wa Arusha (mdogo wake na Collin) akiwa amepozi na aunti yake anaitwa Angel, jamani aunti yake anampenda sana Colman.
Naona Colman kaenda upande wa baba maana alivyofanana na shangazi, utadhani mama yake! Na wamependeza sana!

Tuesday, November 17, 2009

Prescious Prescious...

Mimi naitwa Precious Anthony wa Dar es salaam.
Nina Umri wa miezi miwili sasa, ningependa kubadilishana mawazo na wadau wa hii blog. Hii picha ni siku nipoingia ulimwenguni, nitazituma nyingine zaidi baadaye.
Asante. Nawakilisha.
Precious.
*****
Na sisi tunakuambia karibu sana Prescious, hii picha inanifanya nitamani mtoto mchanga...sooo beautiful.

Monday, November 16, 2009

Francisco, shabiki wa Real Madrid


Mdau Francisco, aka Cesc, huyu ni kaka'ke Raul (mdau mpenda kula) naye ni mule mule, kula balaa, wakishakula ni kucheza kwenda mbele.
Ni mpenzi wa mpiga kumzidi mtu mzima, anaijua first eleven ya Real Madrid kwa kichwa.
Baba Cesc.

Sunday, November 15, 2009

Collin kaanza IT mapemaaa!

Mdau Collin Francis wa Arusha akiwa katika pozi ofisini kwa mama yake.
"Ameanza mapema fani ya baba yake ya IT. sijui akikuwa atakuwaje sasa, ndo atakuwa mtaalamu zaidi."

Hapa kabadilisha kibao na kuanza kumdekea mam'ke Joyce Francis, anamuomba eti amnunulie Trekta!
Joyce anajiuliza, "sijui limemtokea wapi maana kila saa naambiwa, sijui amesikia shule!"
Kalisikia kwenye KIlimo Kwanza, so mama nunua tu hilo trekta, acha kujiuliza maswali.

Saturday, November 14, 2009

Raul anapenda kula!


Huyu ni mdau Raul Tengeneza, anawapa pole akina mama ambao wanao hawapendi kula, yeye na chakula ni kama uji na mgonjwa. Anapenda kula balaa, na akisha kula ni kujiramba na kicheko. Ila anapenda kuangalia TV balaa, tena hapendi kukaa mbali mpaka wazazi tuna hofu na uzima wa macho yake. hapo sijataja utundu, maana akishakula hakuna lingine zaidi ya kuharibu kila kilichoko mbele yake, hakuna linalompita, na anajua kudesa ni balaa, msifanye jambo akaona.
Hii ni toka kwa Baba'ke.

Arthina kwa mapozi...


Mi nimezimia pozi za mdau Arthina...

Friday, November 13, 2009

Bridgitte, dady's girl

Mdau mpya, Bridgitte akiwa na bab'ke, kwa kweli hapo mama huna chako, unless wewe na baba muwe mmefanana!Na wamependeza sana!
Mam'tu Consolatha Ngowi ndio amegundua siri ya mtoto wa kike na baba anasema, "Jamani mtoto wangu huyu ni kipenzi cha baba,yaani kama anakula dad akiingia tu ujue ndo biashara itaishia hapo,atataka dad ndo amlishe! mara dad nibebe,unakuta hapo hata dad tai hajavua!!!nimegundua kuwa watoto wa kike na kipenzi cha baba."


Rispa says hi

Mcuute Rispa.

Thursday, November 12, 2009

Josh amkaribisha cousin toka US

Joshua akiwa uwanja wa ndege na cousin wake Brianna wakimsubiri cousin wao mwingine Annmarie toka USA.

Huyu ndio, Annmarie, mgeni mwenyewe aliyekua anasubiriwa.

Annmarie na Brianna.

Wenyeji, Josh na Brianna.

Collin ndani ya suti

Mdau Collin Francis wa Arusha akiwa amepozi na suti yake, si utani ametoka mchicha sana.