Tuesday, August 14

Utayarishaji wa maziwa ya ng'ombe kwa watoto wachanga

Hivi maziwa ya kopo siku hizi yanauzwaje? Sijui kwa kweli, coz huwa nanyonyesha at least kwa miezi sita! Huu uwembamba usipime, maziwa huwa yanajaa, nakamua ya kutosha siku nzima na mtoto anaendelea kunyonya nikiwepo.

Unashangaa, kama ulikua hujui hata wewe unaweza ukakamua maziwa yako ukayaweka kwenye chupa ukayatunza vizuri kwenye friji, saa ikifika mtoto anapashiwa anakula...yaani hamna tofauti na unavyofanya kwa maziwa ya ng'ombe.

Juu ya hilo, pia mie nilibahatika kujua jinsi ya kuchanganya maziwa ya ng'ombe before sijawa mjamzito, so nimeendelea tu kutumia ujuzi wangu kwa watoto wangu. Anyway, hata Xyleen hakutaka habari ya maziwa ya kopo, aliyakataa kabisaaaa.

Ila sasa sio kila maziwa ya ng'ombe yanafaa kwa mtoto...na maziwa ya ng'ombe kama yalivyo hayamfai mtoto wa binadamu chini ya miezi sita. Ndio mana inashauriwa kama umeamua kumpa mwanao maziwa halisi ya ng'ombe, sharti uyachanganye na maji kwa kipimo maalum.

Kwa nini yachanganywe na maji

Simple, wanasema maziwa ya ng'ombe yana virutubisho mara mbili ya vile vilivyomo kwenye maziwa ya binadamu as mtoto wa ng'ombe anatakiwa akue mara mbili ya mtoto wa bonadamu, so lazima yachanganywe.

Jinsi ya kuchanganya maziwa halisi ya ng'ombe na maji kwa ajili ya mtoto


Kwa kifupi unachanganya maziwa na na maji ambayo ni nusu ya ujazo wa maziwa hayo na sukari kiduchu. Yaani kama maziwa ni lita moja, basi maji yawe nusu lita, kama maziwa ni lita mbili maji yawe lita moja, I think you get the point, then unayachemsha unachanganya na sukari kidoo, then mtoto anakuwa anaendelea kupata.
Kwa details zaidi india HAPA soma kipeperushi, kiprint kikusaidie.

Faida: 

  • Gharama ndogo - lita ni 1,200 tu, na mtoto hamalizi lita mbili kwa siku!(ukishachanganya)
  • Uhakika wa kupata - ukishajua pa kupata kwa uhakika, wala huna wasiwasi, we ni kwenda kufata au kuletewa tu, wakati watu wanahangaika sijui kopo gani limekua adimu ghafla!
  • No TFDA ban - hivi unafanyaje ukisikia maziwa anayotumia mwanao TFDA wametangaza ni feki na una makopo 6! Unayatupa? Na ametumia hayo tangu azalie? Unasali tu. Uzuri wa maziwa halisi ya ng'ombe ni wwe tu na ng'ombe wako!

Hasara:

  • Maziwa haya yanaweza kuchanganywa na kitu chochote huko yanakotoka bila wewe kujua, kama blue band, maji (afu na ww unayatia maji, balaa), unga, ili mradi yaonekane mazito, yana cream na mengi.
  • Unaweza kupewa maziwa ya ng'ombe aliyetoka kuhomwa sindano za kutibu/kuzuia magonjwa. hayo madawa yanaenda kwenye maziwa na mtoto naweza kudhurika nayo.


Zingatia:

Unakotoa maziwa kuwe usalama - hii ni muhimu kuliko chochote, maana kama ng'ombe amechomwa sindano afu hawakumwaga yale maziwa kwa kipindi fulani, wakayauza hivyohivyo, hutayana, ila hayo maziwa lazima yatakuwa na madawa ambayo yataenda kwa mwanao. Au yakawa yamechanganywa na kitu mtoto akanywa bila wewe kujua.

Ushauri:

Kama umeamua kufanya hivi, tafuta mtu unayemjua vizuri, au ndugu ndio awe anakupatia maziwa hayo, ili akuhakikishie usalama wake.
Au kama vipi tumia maziwa ya dukani ambayo hayajachanganywa na chochote - I prefer Tanga Fresh au Asas, Xyleen anayapenda sana na mie napenda kununua cha Tanzania, pia naamini yako fresh zaidi kuliko yaliosafiri umbali mrefu!

3 comments:

Anonymous said...

Asante kwa maelekezomazuri.kuna watoto hawapatani na maziwa ya ng'ombe. kama kuna mwenye experience ushauri atumie maziwa gani au mbadala gani?

Anonymous said...

asnte kwa post nzuri ila hujatuambia namna ya kuyatunza, tuna refrigerate au ku freeze? For how long

Mama Jeremiah said...

Kuhusu mtoto asiyyepatana na maziwa ya ng'ombe, nakushauri mama uendelee kunyonyesha, au la, tumia maziwa ya soya. Mimi mwanangu hapatani na maziwa ya ng'ombe na soya. (nipo nje ya nchi) Hivyo natumia maziwa ya mchele (rice milk). Nimenyonyesha kwa muda wa miezi 9 (ni mama wa nyumbani)na kuanza kumpa vyakula vingine kidogo kidogo hadi sasa ana miaka 5 na hatumi maziwa yeyote. Mtoto pia anapenda kula hivyo sina shida sana kwenye kumlisha.

Kwa jinsi ninavyoelewa ni kuwa mtoto anaweza kuwa na afya njema tuu hata bila kunywa maziwa ya ng'ombe. Unatakiwa uweze kumpa vyakula vyenye virutubisho ili aweze kupata mahitaji yote muhimu ya mwili.