Monday, August 13

Mtoto kaanguka, unafanyaje?


Mara nyingi hawa malaika wetu ni watundu sana, so kuumia ni jambo la kawaida. 
Cha muhimu ni kujua dalili hatari za mtoto kuumia vibaya, ili uweze kumhudumia haraka... shuka chini ili nikujuze...

Endapo mwanao akianguka vibaya kutoka katika baiskeli, mti, ama uwanjani kwa mfano, unatakiwa kuwa makini sana katika kumhudumia majeraha ama sehemu alizoumia, hasa kama ameangukia kichwa ama mgongo . Unatakiwa uhakikishe mwanao hajaumia sana kama vile; kupasuka au kuchubuka sana, au kuvunjika mifupa na majeraha ya ndani.

Na kama mwanao anaonekana yuko ok na umeridhika na hali hiyo, basi anaweza kuwa hakuumia sana. Mshukuru Mungu kwa hilo lakini hakikisha unamcheck mara kwa mara. Endelea kuwa makini na umchunguze kwa masaa 24 baada ya kuumia hasa kama aligonga kichwa.

Tahadhari: Kama hujaridhika na hali inayoonyeshwa na mwanao baada ya kuanguka na unahisi atakuwa amepata jeraha na anaonyesha kuwa tofauti na kawaida yake ni bora umpeleke kwa hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

MKIMBIZE HOSPITALI IWAPO:

 Bofya palipoandikwa ZAIDI BOFYA HAPA » upate zaidi:

  • Ataonyesha dalili ya kupoteza fahamu: Kama mwanao hawezi kuhema mpeleke hospitali HARAKA SANA. Kama unaweza ita hata ambulance! 
  • Atakuwa na utokwaji wa damu kwa wingi ambako huwezi kuizuia mara moja.

Mwone dakatari endapo utagundua yafuatayo:

  • Dalili za kuvunjika mfupa wa ndani, ikiwa na pamoja na kugundua utofauti kwa mwanao kama vile kuchechemea.
  • Dalili za kuteguka kwa fuvu: Hasa katika kichwa. Juu ya fuvu la kichwa au pembeni karibu na sikio. Na pia endapo damu inaonekana katika uweupe katika jicho la mwanao; au hata kutaka kutoka kwa damu katika pua au masikio.
  • Dalili za concussion, kama vile kucheza cheza kwa jicho ama pupil ambako hakulingani (yaani kama makengeza ghafla); mabadiliko ya utembeaji kwa mwanao, muonekano wa kidhaifu au kutojielewa; tatizo katika kuongea, kuanglia, kutapika ama kulala sana yaani kwa muda mrefu.
  • Kulia muda mrefu na kwa sauti sana, haya yote yataonesha kuumia ama kupata jeraha la ndani.1 comment:

Anonymous said...

My dear, mwanangu alianguka toka kwenye bookshelf mpaka chini akagonga paji la uso..alivimabaje sasa... nikamkanda na barafu halafu nikamlaza ila kila baada ya saa 2 nikawa namuamsha nione kama yuko sawa... basi anaamka anasema mama nataka kulala mwenzio nimeumia... namuacha analala...mara ya mwisho nimemuamsha akanambia unanisumbua nataka kwenda kulala kwa dada nikajua yuko poa, ila nilichanganyikiwa sana.