Thursday, June 21

Kulea wasichana vs wavulana


Hii picha ya zamani sana...X akishangilia kombe...unajua boys are more competitive than girls?Si wote tunajua wasichana ni tofauti na wavulana? Sasa unazijua tofauti zao? Loh, ushafika mbaaaali, acha zile kubwa, kuna zingine za kiukuaji wakiwa wadogo na ni ndogondogo sana… Usihame blog, shuka na mie hapa upunguze parenting frustrations na uone utakavyokuwa surprised!
(bofya hapo kushoto palipoandikwa ZAIDI BOFYA HAPA »)Kujijua kijinsia
Uligundua lini kwamba prince wako, au princess wako anajijua kwamba yeye ni girl au boi? Ni mapema kuliko unavyofikiria, mtoto anajijua ujinsia wake tangu akiwa na mwaka na nusu!

By the time anafika miaka miwili anaanza kuwatambua boys wenzia au girls wenzie na anaanza kuigiza kigirl au kiboi. Before that, ni sie wazazi tu tunawa-imposie kuwavalisha magauni, pink sijui blue, sijui kuwanunulia dolls vs cars, wenyewe ukiwapa chochote before miaka miwili hawataidentify kuwa ni cha boys au cha girl, na wataalam wanasema inamchukua takribani hadi afikishe miaka sita kujua vizuri hasa tofauti yake the opposite sex.

Ukuaji wa kimwili
Tangu kuzaliwa hadi wakati wa kubalehe boys na girls wanakua kwa kasi inayolingana, kuanzia urefu hadi uzito! Si tunaonaga boys wazito?
Ni hadi wafikie umri ule wa matata ndio girls wanawaacha boys nyuma, kwa wao kukua chapchap, kurefuka faster…lakini don’t work, boys huwa wanacatch up baada ya miaka michache na kuwaacha girls nyuma!

Motor skills
Boys wako vizuri sana kwenye motor skills kubwakubwa, kama kukimbia na kuruka wakati wasichana wako vyema sana kwenye motor skills ndogondogo kama kushika vitu vidogovidogo kama peni na kuandika.
Hii ndio inayofanya girls wawe wanapenda kuchora tangu wadogo wakati boys huwa wanapenda michezo ya nje. Pia kumbuka, wakati girls wengi hawapendi mashindano, boys wengi wanapenda sana mashindano, as they are more competitive.

Kuongea
On average girls wengi wanawahi kuongea kuliko boys. Girls wanakua wanajua maneno mengi mapema kuliko boys. Girls wanaweza kusoma hisia vizuri na mapema  kuliko boys – mfano princess wako anaweza kutokana na tone ya sauti tu akajua hupendi jambo Fulani, wakati prince anaweza wala asielewe. Hii wanasema, inawafanya girls wawe wanajua kujielezea na waweza kuelewana na watu zaidi kuliko boys.

Kutumia pot 
Girls wanaelewa matumizi ya poti mapema kuliko boys..ila watafiti bado hawajajua kama hii inatokana na kwamba mara nyingi anayefundisha watoto kutumia pot ni mama so girls wanaweza wakapata connection mapema au ni ubongo tu. Pia watoto wa kike huwa wanaacha kujikojolea mapema kuliko boys.


So unavyolea wanao zingatia hayo…boys watundu na hawatulii coz ya motor skills wanazoziweza ni zile kubwakubwa. It will take longer to pot train boys kuliko girls, so usiwe frustrated kwa kuona mbona dada yake umri huu alishaacha kuvaa diapers, he cant help it, ndivyo walivyo! Au unamlinganisha boi wako maneno anayoongea ni machache kuliko girl was shost wako waliozaliwa at the same time, unaona atakua na matatizo, unaanza kuhangaika hospitali – kila doctor akikuambia hana tatizo unaona anakudanganya. Ukijua tofauti zao wala haitakusumbua. Pia kumbuka kila mtoto, boi au girl, anakua kivyake.


No comments: