Kama unataka mwanao awe smart a.k.a msongo a.k.a kipanga
hakikisha unamsomea. Yap, hata kama ni mdogo na haelewi kitu soma kitabu
akusikilize. Actualy, msomee tangu akiwa tumboni, wanasema ile sound ya kusoma
ni nzuri sana katika kumfanya mtoto awe concentrate.
Tafiti zinaonyesha kwamba watoto wanaosomewa home tangu
wakiwa wadogo, huwa ni rahisi sana kuelewa shule, hivyo ni rahisi kujifunza.
Kusoma kunamfundisha mtoto vitu vingi; maandishi, maneno
mapya, matumizi ya maneno, na pia inamfundisha kwamba information inatoka
kwenye vitabu…
Ufanyeje?
- Mwekee vitabu kwenye kabati lake, ili avizoee...
- Mwonyeshe mtoto kwamba kusoma ni raha, so usome kwa furaha – unakumbuka vile vitabu vya series za Someni kwa Furaha?
- Tafutia kusoma siku na saa maalum, sio unakurupuka tu, ili iwe kwenye ratiba yenu.
- Sehemu ya kusomea iwe eneo maalum, lenye utulivu…sio huku wengine wanaangalia TV huku na nyie mnahangaika kusoma!
- Ongelea story mlizosoma pamoja, sio mkifunga kitabu ndio imeishia hapo, zifanye part ya maisha yenu, hapo hatasahau kitu alichojifunza na ataenjoy sana kusoma.
- Msomee mtoto kila siku ukiweza!
There you go...rudi wiki ijayo for siri nyingine...
No comments:
Post a Comment