Monday, February 11

Huduma mbovu, mwenzetu amepoteza mtoto!

Hii story imetumwa kama comment...ila kutokana na uzito wake naiweka kama post muisome kama ilivyo: 

Jamani wadau naombeni kuuliza hivi ni kweli mtoto ukimpa maziwa ya kopo huruhusiwi kumnyonyesha maziwa yako tena?(naomba majibu tofauti na ya madaktari yanayosema maziwa ya mama tu kwa miezi 6 ya kwanza) kwa sababu naamini wapo wadau waliokuza watoto wao tofauti na maziwa yao. Nalazimika kujua ili kutofanya makosa tena baada ya kumpoteza first born wng last (3) weeks niliyemtafuta kwa shida almos (4) yrs, nikalazimika hadi kwenda kwa wataalam wa uzazi, inauma kuliko ninavyoweza kuelezea... He was a boy, alizaliwa akiwa na 3Kgs/800gms 

Nikiwa na ganzi mwili mzima baada ya kutoka thieter namwona mwanangu anavyolia hadi kukauka kwa zaidi ya masaa (24), maziwa yangu hayatoki, ndugu hawaruhusiwi kuingia wodini, nurses na doctors ndo wanaonihudumia wanasema "maziwa ya mama kwa miezi 6 ya kwanza ni kawaida maziwa kutotoka kwa siku za mwanzoni hasa mliofanyiwa siza kutokana na kutokula vyakula vinavyoweza kusaidia maziwa kutoka haraka, na kulia kwa mtoto ni kawaida kwa siku za mwanzoni, endelea kumnyonyesha yatatoka" hivi inaingia akilini kweli? 

Siku ya 3 maziwa yangu yanaanza kutoka mtoto hawezi kunyonya taya zinamuuma kwa kulia 2days, amepandisha homa hadi 39degrees, kanachomwa sindano 4 kwa siku, 2 asubuhi, 2usiku na hakali kitu, kanadhoofu na kupungua uzito, naruhusiwa kurudi nyumbani mwanangu anafariki, Je! angepata msaada/mbadala wa maziwa tangu alipozaliwa yangezaliwa yote haya? 

Madaktari wanapaswa kutuhudumia kwa kutumia taaluma zao lakini wakati mwingine watuangalie watanzania na hali zetu, tusiige kila kitu toka kwa wenzetu, ni jambo zuri lakini linahitaji kujiandaa hasa... kazini tunapewa maternity leave ya miezi (3), huku natakiwa kunyonyesha kwa miezi (6) inaingia akilini kweli? Inauma sana, sikutegemea kama yangenitokea lakini yamekuwa... 

Niliacha kazi ili nitegemee kuwa mama bora, nilisimama masomo baada ya kuanza heka heka za mimba, nilijiandaa vizuri kwa kuweka akiba kabla na baada ya kujifungua lakini haikufika popote baada ya mengi kujitokeza, baada ya kuisha kwa akiba hiyo nikaona ni heri nipoteze kila kitu cha thamani kwangu kuokoa maisha ya mwanangu, nimeuza hadi pete ya ndoa ili nijaribu kuokoa maisha ya mwanangu, nimepoteza kila cha thamani kwangu, after all nimempoteza na yeye. 

Nikiwa sielewi nianzie wapi,sina a wala z, mshono unaachia narudi tena thieter, natibiwa kwa gharama zangu kama mgonjwa wa nje, natakiwa kulipia tax kutoka kwangu T.Shs. 15,000/= kwenda na T.Shs. 15,000/= kurudi (Tshs. 30,000/= per day x 14 days = 420,000/=, sindano 10@ 8,400/= x 10 = 84,000/=, Mebo cream 12,000/= bado dawa za vidonge nimesahau hata bei yake, ukienda maina thieter ukakutana na mtu ananjaa zake hakusafishi hadi umpe ya soda, hii ndiyo Tanzania yetu inayosema Huduma za Mama Mjamzito na Mtoto bureeeeeeeee.... Haya ni yale yaliyojiri baada ya... Nani chanzo cha haya? Nishaurini wadau labda naweza kupunguza maumivu japo kidogo. 

***
Nimeisoma hii story machozi yamenitoka...sijui hata pa kuanzia, huduma zetu za afya kwa kweli zinasikitisha, hata private sometimes unafanyiwa kitu unashangaa.
Wito tu kwa wakina mama wenzangu, ukiwa hospitali usiogope, uliza kama una wasiwasi na jambo (sio unauliza kwa ukali au kwa dharau, unauliza ili upate kujua)...kama hujaridhika na maelezo, tafuta second opinion...kwenye maisha yako hakikisha una daktari unayemuamini, unayeweza kumpigia any time ukamuuliza chochote afu ukaridhika na jibu lake. Tunajua madaktari hawana uwezo wa kuzuia vifo, ila wapo ili kupunguza vifo visivyo vya lazima. Muhimu sana kuelewa kinachoendelea.
Afu kingine, wote tunajua saa ya ugonjwa mtu saa nyinigine unakua huna concentration, hasa saa ya uzazi, hakikisha kuna mtu, au watu wengine (mume, partnes, mama, dada, mama mkwe, wifi, shost) wanafuatilia kila kitu kwa ukaribu watakaoweza kukusaidia...peke yako unaweza ukashindwa kuelewa kinachoendelea.

Kuhusu kula kitu kingine: Nnavyojua, mtoto anaweza kunywa maziwa mengine, kwa sababu mbalimbali (wamama wengine hawapendi/hawataki kunyonyesha, ugonjwa wa mama, kifo cha mama wakati anajifungua, maziwa kutotoka-wengine watakua mashahidi hapa, watu wanaojifungua kwa operation mara nyingi maziwa yanachelewa so watoto wanaanza na ya kopo), so mtoto anaweza akaanza na maziwa ya kopo ya watoto wachanga (formula) au hata maziwa ya ng'ombe kama una access ya maziwamazuri unayoyaamini, unatakiwa tu ujue jinsi ya kuyachanganya, soma HAPA nilishaelezea jinsi ya kuchanganya.

Pole sana mdau kwa kupotelewa na mtoto...ila tunakuombea utapata wengine ingawa hawata-replace uliyempoteza, lakini utapata watoto wengine.

Jiang.

16 comments:

Anonymous said...

jamani acheni!i can only imagine.sometimes hosp wana mambo ya ajabu. wanajitia hawaruhusu kopo sasa maziwa hayatoki!jamani
pole mamie
wenzetu wanajeshi maternity mpk miezi 6.
hata sina cha kuongea

Anonymous said...

kwa kweli imeniuma sana! ni docta gani wkt mi wa kwangu aliniruhusu same day nimpe nan 1 since mi pia maziwa haykutoka mpk ucku sana coz nlipasuliwa asbh ya saa 2,imagine mtoto alikua tu analia ilivofika saa 4 docta akasema tumpe maziwa km kwangu haytoki.they are human kwa nn wasisikie njaa? mungu tusaidie sisi wamama na kujifungua kwetu kwa kweli inauma sana ht ukiwashtaki it`s not worth it since hawezi rudisha roho ya mtoto wetu muombe mungu sana akupe ujasiri na uvumilivu inshaalah utapata mwingine,pole sana mama!

Anonymous said...

Pole sana jaamani! Mungu tu ndio akufariji! Naona madaktari hapo walikosea walipaswa mampe toto maziwa ya kopo wakati na wewe unaendelea kuya stimulate maziwa yako hadi yaanze kutoka. Labda ushauri tu utakapo jaliwa kuwa na mtoto mwingine unapoenda kujifungua beba maziwa ya kopo just in case yako hayotoki....I pray and hope this wont happen again kwani inaumiza sana !
Once again pole sana

Anonymous said...

yaani nimesoma hii habari mpaka mwili wangu umenisisimua,nimumia sana,pole sana mama,Mungu hamtupi mja wake utapata mwingine.
Miminilijifungua kwa operation na mtoto alianzishiwa maziwa ya kopo lactogen siku hyo hiyo,ingawa yalikuwa yanamuumiza akawa anayatema ila ilimsaidia kuliko angekuwa hana kitu kabisa.

Anonymous said...

Mi nilijifungua kwa siza 4 dys maziwa hayatoki baada ya masaa 6 mtoto alikuwa akilia ikabidi apewe formula baada ya kutoka hospitali nikawa namnyonyesha yng na formula nampa.pole sana.

Anonymous said...

kwa kweli hii habari imeniuma na kunikumbusha mbali, mimi nilizaa mimba ya kwanza mapacha tena government hospital ilibidi nipelekwe hospitali ya serikali kwa sababu ilikuwa mimba yangu ya kwanza na pia nilikuwa muoga kuzaa, kufika kule nilikaa na uchungu 3 days bila kujifungua na pia nikapata low presha, ilibidi nipelekwe ICU na nilipopata afadhali nikaenda kujifungua kwa oparation, sasa baada ya kutoka huko fahamu zilinirudia na kusikia vitoto viwili vinalia kwa uchungu tena vinashindana, nikapata nafasi ya kumuita nesi ili aniletee watoto wangu niwanyonyeshe kwa sababu wanalia sana na ilikuwa usiku hakuna ndugu wala jamaa yangu, nesi alikuja juu na kunikaripia kwa ukali majibu yake hayakuniridhisha kabisa mwisho akataka kunipiga eti kisa nang'ang'ania kutaka kupewa watotot ili hali bado hali yangu haijawa nzuri,nikatulia kwa muda nilipomuona amezubaa mungu alinisimamia nikaanza kulia kwa uchungu na kutaka kutoa yale madrip na kuanza kuwafata watoto wangu. kwa bahati nzuri akaniona nanyanyuka kitandani , kaanza kunitukana na wala sikumjali nikatumia ujasiri wangu kumjibu kwa uchungu, nikamwambia hivyo vitoto vikifariki utaozea jela coz nilijua vinanjaa, nilijifungua tangu machana na hapo ilikuwa usiku kama saa mbili, mwisho tena kwa mbinde akanipatia watoto wangu mapacha ndio nikawa na amani na nikaanza kuwanyonyesha twins wangu, tena walikuwa wakike na kiume. baada ya hapo yle nesi alienda kusema kwa madaktari kuwa huyu msichana kumbe mzima tu na hivyo aende nyumbani kwako maaan ni mkorofi.

hapa najaribu kutaka kuelezea jinsi gani maensi wanayotu-treat,story ya huyu dada imenikumbusha mbali, dada usikate tamaa mungu atakutia moyo na utapata watoto mapacha kama mimi,AMEEN

Anonymous said...

Hii habari imeniuma mno!Hapa nlipo mwili umekuwa wa baridi kabisa!Pole sana dada,najua unapitia kipindi kigumu mno na hasa ukizingatia changamoto ulizopitia ili kuhakikisha unajiandaa na malezi ya mwanao!Mungu yupo,usikate tamaa,Endelea Kumwomba Mungu,wasamehe hao madaktari ninaamini Mungu atadeal nao accordingly...Utapata Watoto wengine wazuri na utawalea kwa wepesi na wala hautaamini!Pole sana mamie

Anonymous said...

Yaani habari hii imeniumiza sana sana kupita maelezo kwakweli! Jamani mie watoto wangu wote mbona nimejifungua kwa operation ila ni private hosp.but mbona watoto walikuwa wanapewa lactogen jamaniii!! mpaka mama maziwa yakianza kutoka basi unaendelea kumpa yako. Ni kweli wapo wanawapa watoto wao maziwa ya mama for 6 mnths bila ya kopo(inawezekana kabsa kinachofanyika ni hivi: Kuna wamama wengine wamejaliwa huwa yanatoka maziwa mengi na ukichanganya na vimiminika wanavyokunywa au chakula wanachokula ndio yanazidi kuwa mengi so kabla mtoto hajanyonya anakamua kwa kutumia breast pump coz yanakuwa yamejaa jaa baby hajanyonya then ndio anamnyonyesha mtoto coz normal huwa bado yapo tu kifuani hayaishi na mkumbuke mtoto anyonyavyo/ukamuapo ndio maziwa yanavyojitengeneza zaidi,Pia mtoto akiwa amelala unaona maziwa yamejaa unakamua unaweka kwa freezer/fridge wataalamu wanasema ukiyatunza kwa freezer yanauwezo wa kukaa na kutumika hata 5 days...so utaenda kazini mtoto anapashiwa tu anakunywa(yanakuwa kwa chupa yake then yanapashwa kwa maji ya moto kama tunavyopasha maziwa ya kawaida ya mtoto yakiwa kwenye chupa'ke) mpaka muda unarudi home kunyonyesha nawe maziwa yamejaa basi safiii anaendelea na maziwa ya mama tu, tena kuna baadhi ya breast pump zinauzwa na hivyo vijichupa/vikopo vya kuhifadhia hayo maziwa ukikamua,mie sina maziwa mengi sana ila nilikuwa nakamua ziwa 1 napata 150-200mls na zaidi kwa wakati mmoja so nikikamua maziwa yote 2 ni 300-400mls so hata mtoto akilala unaona maziwa yamejaa unakamua tu unahifadhi incase ameamka mama upo home mtoto ananyonya tu maziwa yako yale uliokamua yanabaki kama akiba unavyoenda kazini au ukitoka ila tu ktk kutumia ya kwenye freezer ukumbuke first in first out. Ila kama maziwa yako sio mengi hamna tatizo mtoto akinywa maziwa ya kopo. Pole sana dada MUNGU wetu ni mwaminifu sana atakupa watoto wazuri tu wengine.


Mama E.

Anonymous said...

pole mama yani wewe ungejitia wehu ukampa maziwa ya kopo wala usingechapwa wala nini ni maneno tu yao na wala hayaui,yani izi hospitali zina wahudumu washajikatia tamaa na wanasiasa wasiojali maisha yetu hakuna vipaumbele kabisa...ila ndo ivo ushampoteza mtoto Mungu akupe mwingine tena

Anonymous said...

Pole sana mamii, Mungu wetu ni mwaminifu atakujalia kilicho chema ni kumtumainia tu. Mimi nilijifungua mwaka jana, maziwa hayakutoka na mtoto alikuwa analia sana. Nilichofanya nilichukua maji ya kunywa nikaweka sukari kidogo (sikuwa na glucose wala maziwa ya kopo), nikavizia manesi hawapo nikamnywesha mtoto kama vijiko viwili vikubwa akatulia. Kila baada ya muda alipolia nilifanya hivyo hadi kesho yake maziwa yalipoanza kutoka kidogo nikakazana kula hususan chakula/supu/mtori wenye nyanyachungu zilinisaidia sana maziwa kutoka haraka. Kikubwa ni kujua namna ya kumnywesha mtoto asije akapaliwa, mimi nilikuwa na uzoefu maana huyu ni mtoto wangu wa 3 so kumnywesha haikuwa tabu na wala manesi hawakuniona.
Sababu wanayokataa mtoto asipewe chakula chochote/maziwa na badala yake anyonye hadi miezi sita ziwa la mama ni usafi maana wakiruhusu watoto ni rahisi kupata magonjwa ya kuhara kutokana na uchafu katika uandaaji wa chakula cha mtoto na hivyo kupelekea vifo kwa watoto. Kuepusha hilo ndo maana wanasisitiza maziwa ya mama hadi miezi sita angalau mtoto anakuwa amekua kiasi fulani.

Pole sana dia Mungu akupe nguvu.

Anonymous said...

yaani hii inauma mpk basi wamemuua mtoto na njaa jamani eeh mungu hawana hata chembe ya huruma na malaika,hivi mtoto amekalishwa na njaa siku hizo zote walikuwa wanafikiria kama sio njaa inamuuma,mie nilifanyiwa operation na maziwa yangu yalikuwa hayatoki halafu mtoto sikupewa maana alikuwa na tatizo la tumbo so alipelekwa hospital nyingine nilipotoka hospital moja kwa moja nikaenda kumuona hata hivyo sikupewa mtoto mpk wiki ilipoisha kwa ajili ya uchunguzi ila mie nilipokuwa nyumbani nilikuwa naendelea kukamua ili yasikauke ila kule hospital alikuwa akipewa maziwa ya kopo mpk tulipo ruhusiwa kwenda kumchukua na hata hivyo niliendeleana yote maziwa yangu na pia ya kopo pia ila hii ni kwa hapa europe wala jali sana,inauma sana kutenganishwa na mtoto wako japo nilikuwa najikongoja kwenda kumuona ila nilikuwa sina raha kabisa nyumbani namshukuru mungu sana anaendelea vzr na afya njema pia,pole sana ndugu yangu inauma zaidi unapo muona mtoto analia mpk anakauka kisha watu hawana hata muda naye yaani nikifikiria niliyo pitia mimi mungu ni mwema takupatia mwingine ila inauma sana,mungu akupewa nguvu kwenye kipindi hiki kigumu na mungu atawahukumu hao manesi.

Anonymous said...

Ee Mungu msaidie mama huyu. mimi nilijifungua kwa operation nikaugua na mwanangu akapewa ya kopo mpaka nimepona hakudhoofika kabisa. Mungu ndo anajua ni kiasi gani unaumia. chukulia kuwa huu ni wakati wa ukimya kwako na muombe sana Mungu. Nakuombea sana Ndugu yangu. Machozi yananitoka nashindwa hata kukuambia kitu kingine
Mama Princess Ban Ki Moon

beatrice said...

jamani nimesikitika sana pole na mungu atakujalia upate mtoto mwingine ila hao madaktari ni wauaji kweli imagine mi nimejifungulia norway n,aishi huku sikuwa na maziwa kwa siku tatu wakawa wanakachukua mtoto na kumpa nan then wananirudishia siku ya nne nimeenda nyumban from hosp ndo nikaanza kumnyonyesha maziwa ndo yalianza kuja kwa kupump kwanza duh,imagine kuna wengine ambao hawanyonyeshi watoto wanawapa nan tu ingekuaje wangekuwa tz pole dada mungu amesikia kilio chako

Anonymous said...

nilijifungua kwa operation, maziwa yalikuwa hayatoki, siku ya kwanza alipewa glocose, walivyoona maziwa bado hayatoki ilibidi wampe S26, na aliendelea nayo mpaka anatimiza miaka 2.

Ysha said...

pole sana mama, i can imagine how u feel, inauma mno. mimi pia nilijifungua kwa operation (Regency) na maziwa hayakutoka na mtoto alikuwa nalia sana, so nurse alikuwa anaweka glucose katika bomba la sindano kubwa na kumnywesha mtoto huku na mimi naendelea kumpa chuchu avutevute tu. hadi yalipoanza kutoka maziwa akaendelea. BUT hao madaktari waliokukataza wewe ni wauaji kabisa. naungana na mchangiaji alosema lazima wawe na UTU, wamfikirie yule kiumbe malaika anayelia njaa. sasa walijisikiaje mtoto alipopoteza uhai wake? ungewafuata ukawaambia ili nafsi zao ziwasute. pole sana.

Naomba nami ni share tukio lililokaribia kunipotezea UHAI wa mtoto wangu wiki mbili zilizopita. mtoto (18 months) alikuwa anasumbuliwa sana na mafua na kifua, tukaenda hospital (Dr Hameer Kkoo DSM) akapata antibiotic na cough syrup. after 3 days akawa anapata homa, nikataka kumrudisha tena hapohapo kwa dr Hameer but muda ulikuwa umekwisha so nikaamua kumpeleka hospital moja ya polisi (kurasini) ili tucheck Malaria. kweli tukamuona Dr na akapima malaria but hakuwa nayo. wakati tunasubiri kurudisha majibu homa ikapanda saana hadi akapata conversion. Wakampa huduma ya kwanza akatulia then wakatulaza na kumuandikia dose ya quinine drip 3, x-pen sindano 3 na diclofenac 1. na dose ya kwanza ya sindano diclofenac, x-pen wakamchoma sa11 ile halafu wakasema tumfatie uji apewe then wamtundikie drip. Nikaulize manesi, Sijaelewa hizo Quinine ni za nini while mtoto hana malaria? nikajibiwa "wewe unafikiri kwanini mtoto ana homa kali kama siyo malaria? ukiona dr kamuandikia ujue malaria ipo ila haijaonekana tu" nikavuta pumzi kwanza, but moyo wangu unakataa kabisa. ikabidi babake akamfatie uji mi nibaki nae mtoto analia hataki kukaa wala kulala pale kitandani. wakaja wakwe na wifi zangu nikawaambia mimi sipo tayari mtoto awekewe ma drip, so tuondokeni naye. wakaogopa kwenda kuongea na dokta eti labda tuondoke kimya kimya nikasema hapana, the kid is mine so i have all the rights to take him wherever i belive tutapata the best services. Nikambeba hapo keshanyamaza yupo sawa kabisa nikaenda kwa dokta nikamwambia nataka kuondoka na mtoto nimpeleke anapotibiwa siku zote. akasema kwa hasira nenda kaandike maelezo kwenye file na usaini nkasema sawa. nikaomba file kwa nesi na kuandika maelezo kuwa lolote litakalotokea nimemchukua kwa hiari yangu mtoto nikaomba niandikiwe matibabu alopatiwa haoo tukaondoka. nikaambiwa x-pen ingine saa 5 usiku but hatukuchoma tena. asbh tukaamkia kwa dr.Hameer baada ya kumpa melezo yooote hayo nikaona Dr anashusha pumz akaniambia: MAMA NI BORA ULIKATAA HIZO QUININE MAANA SIJUI NINI KINGETOKEA KAMA ANGETUNDIKIWA HIZO DRIP NA SINDANO ZA X-PEN as vipimo vya pale vilionesha ana infection ilomsababishia PNEUMONIA kali.sasa hebu pateni picha, ni watoto wangapi wameshapoteza maisha kwa design hii? wamama/wagonjwa huwa na matuman=ini makubwa sana na madaktari, lakini madaktari hawataki kufuata kanuni na ethics zao, as siamini kuwa ndivo walivofundishwa kutoa matibabu kwa ugonjwa usiokuwepo. nawashauri wamama wenzangu tuwe makini sana na hawa madaktari kwani watatumalizia watoto wetu. no wonder why vifo vya watoto vinaongezeka kila kukicha, vingi ni vya kusababishiwa na madaktari wasiokuwa makini na kutumia MAZOEA na sio TAALUMA yao. Tujaribu kuwa madaktari wenyewe, jua tatizo la mtoto wako, angalia kvipimo alivyofanyiwa na soma majibu ya mtoto na ikiwezekana omba ufafanuzi kulekule maabara hata kabla hujaingia kwa daktari la sivyo tutalia na MUNGU kila siku. mtoto wangu alipata matibabu ya uhakika pale kwa Dr Hameer tukalzwa siku 1, akaendelea na matibabu ya siku 5 kifua kimepona na hiyo malaria hakuwa nayo hata kidogo. NAMSHUKURU MUNGU kwa kweli maana naamini ni yeye aliniongoza tu, otherwise hii story ingekuwa nyingine sasa hivi.

marc said...

pole sana mama yaani leo ndio siku ya kwanza kuingia hii blog na kusoma hii habari yaani naandika hii msg huku machozi yananitoka kwani najua jinsi moyo wako ulivyo na maumivu makali pole sana, Mungu wetu ni mwema na mwaminifu nitakuombea na wengine watazidi kuomba kwa ajili yako kabla ya mwaka huu uwe na ujauzito wa mtoto mwingine tena ikibidi mapacha yote yanawezekana mama kwani Mungu ndiye muumbaji wa yoye.kinachoniuma ni jinsi hao manesi walivyofanya kwani mimi nilizaa wa operation siku nne maziwa hayatoki manesi walikuwa nanamkorogea maziwa ya kopo wanampa ni hospital ya agakhan hawana shidaa na hilo wanajua siku za mwanza maziwa hayatoki sometimes ata ukijifungua kawaida,
pili kinachoniuma ni process nzima ya mimba na maangaiko ya miezi tisa yaani ,kwani hapa mimi ni mjamzito tena, lakini tangu mimba inaanza nikichefuchefu kutapika zaidi ya mara nne kwa siku ,matehayakauki mdomoni yaani ni mateso lakini najipa moyo kuwa ni ya muda tu nikimpata mtoto nitasahu kila kitu kwani ndio faraja sasa hapa nakufikiria wewe baada ya mateso yote umeambulia maumivu pole sana. kama ni mkristo ebu jaribu kuangalia picha ya yesu msalabani alivyoteseka sana kwa ajili yetu ili sisi tuweze kupona hivyo kila muda unapokaa katika maumivu yako mwambia yesu najua yesu unajua nilivyoteseka kwa ajili ya kumpata huyu mtoto na pia mweleze jinsi unavyoumia sana moyo mkabidhi yeye maumivu yote atakubebea utapata amani moyoni, Mungu akutie nguvu na kukupa faraja ya moyo amina