Friday, February 1

Tujuzane tafadhali

Ni muda gani mzuri kwa watoto wa kike kuanza kusuka? 
Mi napenda kumsuka Patra ingawa naona kama namuonea
 vile kwani hajui chochote kuhusu urembo wa nywele
 wala chochote ingawa pia huwa anapendeza.
 


Tuambiane ukweli na tujadili wazazi. Upi ni muda muafaka?

7 comments:

Anonymous said...

Mie mwanangu alikuwa na nywele nyingi na nzuri toka mdogo sana but sikumsuka mpaka alipofikia 3yrs tena nilikuwa namsuka mabutu tu tena ya mlegezo,akiwa na mtoko namwekea vbanio basi.


Mama E.

Anonymous said...

YANI JAMANI NAPENDA MTOTO ANEYESUKA ILA MWANAGU ANA MWAKA VIPILIPILI UKICHANA AKITOKA NJE ZINARUDI KAMA NZI YANI NAMNYOA KILA MARA...... NISAIDIENI HZ PILIPILI ZITAONDOKA LINI?

Jiang said...

@Mama E...asante kwa tip...hata mie naona ntafanya hivyohivyo...mwanangu ana nywele nzuri kiasi chake, ila sitaki kuhangaika nazo now, ingawa walimsuka mara 2 nimewapiga stop...

@Anony...siju kama hizo pilipili zitaondoka bila kutia dawa, kitu ambacho sishauri kwa mtoto chini ya miaka 7...swali tu ujiulize kwani nyie wazazi hamna kipilipili kwenu? kama kipo kwa mmoja wenu basi ndio kakirithi...cha kufanya ni kuki-mantain tu, kwa kumnyoa mara kwa mara...utaanza kuhangaika nacho akikua, sasa mwache tu! kwanza watoto wanapendeza tu, vyovyote!!!

Anonymous said...

msisahau kuwa kila mtoto anakuja na asili yake ya nywele hata usipomsuka zinakuwa zenyewe daily huna haja ya kumsuka mtoto chini ya miaka mitatu kwani inachangia sana kumkomaza uso mtoto kutokana na kumvutamvuta kila unaposuka kama ana nywele nzuri hakikisha unampaka mafuta yake ya maji tena ya nazi nzuri ukitengeneza mwenyewe hali itakayomfanya umentain uzuri wa nywele zake

Anonymous said...

wangu ana nywele laini na ndefu ila huwa simsuki nambana tu na vibanio na muda mwingine tukiwa tu nyumbani naziweka tu mafuta ya nazi nazichana bila kubana,kumsuka bado mdogo inachangia kumkomaza sura na alivyo na tabasamu zuri mwenyewe sikushauri umuharibu sura yake nzuri mcute lil angel mbane tu itatosha ila anapendeza kweli mashallah.

Anonymous said...

Wa kwangu ana nyele nyingi tu lakini namnya mana naona kama nywele zinamkondesha. Siwezi kumsuka kamwe labda akiwa mkubwa. Naumia sana yani. Mimi sisuki mana nina kipilipili na natakiwa kuweka dawa lakini nina ubovu wa macho hivyo siruhusiwi mana niko kwenye critical stage. Napenda kusuka ila naumia sana. Hapo ndo ninapowaza je mwanangu akisukwa itakuwaje. Nasikia uchungu sana kwa kweli.

Jirani yangu alimpeleka mtoto wa miaka sita akasukwe nywele za uzi yaani ukimuona utamhurumia mana alivyorudi alianza kulia na mama yake anampiga na kumuweka barafu kichani ati ili kichwa kipoe. Nilienda kwake kumwambia nitamshitaki mana atamuua mtoto kwa maumivu.Nikamwambia amnyoe nitamrudishia hela aliyomsukia mana anasema ananipotezea hela yangu. Inatia uchungu sana. Uzuri ni kujiamini sio manywele. Watoto wote ni wazuri. Yanini kumpa mtoto madawa ya usingizi ili eti asuke? Je anaelewa maana ya kusuka? Nashauri wamama wenzangu tuache tu mana watoto wetu wanavutwa sana na wanaumia mno.
Mungu wangu ninayekuamini Nawaombea wamama wote wanaotimiza wajibu wao uwabariki na uwape ujasiri wa kusimamia malezi ya watoto wao.
Stay blessed Mamas
Mama Princess Ban Ki Moon

Anonymous said...

Mimi wakwangu nilianza kumsuka akiwa na umri wa mwaka mmoja. Alizaliwa na nywele sana na mpaka sana ananywele nzuri, laini na ndefu. Ila namsuka mwenyewe, simpeleki kwa mtu kumsuka, namsuka mwenyewe , wala simkazi namlegeza tu na simsuku nyingi namsuka chache tu maana hawawezi kutulia sehemu moja kwa muda mrefu.

Shida ni kwamba sasa nimesafiri kikazi yeye nimemuacha, na ananywele ndefu sasa, nilicho fanya kuna dada namjua na anapenda watoto, watoto wanampenda anasuka analegeza nimempa tenda kwenda kwangu kila juma mosi kumsuka coz sasa anamiaka 3 na anaenda kindergarten.