Tuesday, February 19

Form IV 2012 Results: Zaidi ya nusu wana zero, tunaenda wapi?

Hii sio news mpya, maana sasa ni mwaka wa tatu matokeo ya sekondari hayaridhishi kabisa!!!
Kama ulikua hujui, mwaka huu ndio kali zaidi maana zaidi ya nusu ya wanafunzi wote aliofanya mtihani mwaka 2012, yaani 65% wamefeli kwa kupata zero!!!
Nimekaa hapa nayaangalia haya matokeo wala siamini ninachokiona...inasikitisha kwa kweli!!!

Sasa tatizo kama hili wote tunajua haliwezi kuwa la wanafunzi wala la eneo, wala sisi tunaowalipia wanetu private hatutatiwi tuliacha kwa vile tu sio wanetu...HAPANA! Kwa sababu hii nchi ni yetu sote, mwisho wa siku tunachanganyikana wote na kwa effort za kila mmoja, kwa nafasi yake ndio tutaweza either kupeleka mbele gurudumu la maendeleo or kuliacha liserereke nyuma na kutuangamiza...so si suala la kufun=mbia macho hata kama mwanao anasoma St. Academy!

Katika vitu vyote, nimelelewa na kufunzwa kuwa hakuna kitu cha muhimu ka a ELIMU!!!
Na kwa kweli, nakumbuka nilivyomshangilia JK alipoingia madarakani first timekuhutubia bungeni alisema kwenye serikali yake kitu cha kwanza ni Elimu, cha pili ni Elimu, na cha tatu i Elimu!!!!
Elimu sio kitu cha kuchezea...

Sasa inasikitisha sana kusikia kuwa zaidi ya nusu ya form four wamefeli, zero kabisaaaa, yaani wamezungusha!!! Sio kwamba nasema hivyo kuwakejeli, as siamini kuwa ni kosa lao, ila ndio ukweli!!!!
Ile exception iliyokuwepo wakati sisi tunasoma ya  kumshangaa mtu aliyepata zero, maana wanakua wawili watatu sasa wanashangaliwa waliopata one  hadi three maana ni wawili watatu!!!
Ingia website ya baraza HII HAPA chagua shule yeyote uone hali inavyosikitisha...yaani ni zero na four ndio zilizojaa!!! Sasa hawa watoto waliopewa hope na kufaulu kwenda sekondari za kata kwa wingi wanaenda wapi after this? 

Hii inamaanisha nini? Yaani hamna kilichoingia kichani kwao tangu wainge Form I? Maana mtu akipata zero maana yake hajajifunza kitu, au? Kwa hiyo tunawapeleka sekondari ili iweje? Wakakue? Wakakutane na kujuana? Maana kiukweli hamna walichojifunza!!!

Na kwa future ya taifa letu inamaanisha nini? Tunatengeneza taifa la wajinga au sio? Ila tofauti na wa zamani, hawa tumewapa hope kidogo...ingawa wamefeli na kupata zero wamefunguka kiduchu...afu tunawaacha tu mtaani...tunatengeneza bomu, litakuja kulipuk baadae...maana kama wenye vyeti vya 

Nashauri serikari itafute mkakati wa kutatua hili tatizo maana so far tulichofanya ni kujenga shule kila kata tu...sio kwamba napinga uwepo wa shule za kata, nazisapoti sana na tangu mwanzo wakati wengi wanapinga shule za kata mie nilizisapoti, as lazima tuanzie sehemu na kwenye sector ya elimu ni majengo....

Ila sasa baada ya majengo, tumekaa tumebweteka...kama vile hayo majengo, tena madarasa mawili matatu na ofisi, ndio yatafundisha wanafunzi...kupitia kazi yangu nimeona kwa macho yangu shule ya sekondari yenye mwalimu mmoja...mazingira yenyewe tata , msituni!!! kijana ambaye hazidi miaka 27, kamaliza chuo, ndio kapangiwa kufundisha hiyo shule, iko porini mbali na makazi ya watu, afu nyumba yake iko hukohuko....afu hakuna hata network (kwa wakati huo ilikua 2008 kama sikosei)...hawezi hata kuchat na vijana wenzie aliosoma nao angalau asijione mnyonge, halafu kufata mshahara ni wilayani, mbali, kukodi pikipiki kwenda na kurudi si chini ya 80,000/- (hakukuwa na usafiri mwingine kati ya wilaya na vijijni) halafu unategemea huyo mwalimu akae!!! Kila mwalimu akikaa mwezi mmoja, ukifika mwisho wa mwezi akienda wilayani kuchukua mshahara harudi tena!!!!
Kwa mazingira hayo niambie hata huyo mwalimu akiwa na moyo mgumu akaamua akae ana moyo wa kufundisha? mwanafunzi ana moyo wa kosoma? na mwalimu mmoja, wawili au watatu watafundisha masomo yote kwa form one hadi four? Happo unategemea nini kama si zero, hata mwenye four kajitahidi sana...kwanza hao wenye zero wapewe cheti cha kufanya mtihani ingawa wanajua hawajui chochote!

Katika hili nadhani serikali inatutatia...seriously, serikali haiko serious kwenye elimu, future ya nchi yetu, kwa hiyo 10 years, 20 years to come, tusilalamike nchi yetu ikizidi kutitimia kwenye lindi la umasikini, uhalifu, ujinga na kila kitu cha ovyo, maana kwenye maisha ya karne hizi hamna kitu muhimu kama elimu....tutaibiwa madini na gesi zetu weeee hadi ziishe tubaki na mashimo, maana kama nchi tumechagua kuwa taifa la wajinga!!!! kama asilimia 6.2, tu ndio waliofaulu basi it is hightime Tanzania kama taifa tujiulize tunakwenda wapi???

Kiroho safi tu, mimi ningekua waziri wa elimu, ningepisha, ili aje mwinine anayeweza atatue tatizo, as for the time being ameshindwa kutatua tatizo. Kibongobongo, najua hatopisha, ndio maana nasema ningekua mimi! Ila Kawambwa ameshasikia maoni ya wengi katika ili, na bosi wake kasikia, tufanyeni tuone mnafanya kitu basi, sio kila kitu hadi kiundiwe tume...waziri utakua shujaa sana usema viatu havinitoshi, subiri nivue ajaribu mwingine, labda, narudia tena labda atatokea mvaaji vinayemtosha!

Kwa upande wetu wananchi, watanzania wenzangu, hebu tutafute kitu cha kufanya...lets brainstorm nini kifanyike kuokoa elimu yetu, kuokoa nchi yetu!!! 1 comment:

Anonymous said...

nimesikitikaje kuhusu matokeo ya form four kuna mtoto wa marehemu mdogo wangu namsomesha kapata four mbaya hapa nakuna kichwa nimfanyeje hakubaliki sehemu yoyote si kwenda form five, sipati chuo sipati chochote yaani ni sawa kama hakumaliza secendary niko njia panda mwenzenu, maoni yangu naomba serikali ifikirie watoto warudie mtihani au wawafanyishe somo moja moja na kuangalia mapungufu yako wapi, hatuwezi kuwajaji watoto kwa mtihani wa siku moja au wiki moja utaratibu wa matokeo ubadilishwe watoto wapimwe kwa kazi za darasani na masomo waliyosoma, kama kuna masomo hawakusoma au hawakufundishwa kabisa kwa kukosa mwalimu mtawapa vipi mtihani waufanye? waziri kawambwa unajikanyaga na kuropoka ovyo jiuzulu baba unatengeneza bomu litakuja lilipuke, wadau wenzangu nisaidieni huyu mtoto mimi namfanyaje? ndoto zake zote zimegota hapa nina pesa mfukoni ya kumsomesha lakini cheti hakiniruhusu kumpeleka popote