Ingawa nchi yetu huwa hatuwathamini wasanii, ila research
zinaonyesha tofauti na tunachofikiri…maana nasi kwa kudhani!!!!
Ndio maana kwa wenzetu wanakazania kuchora, kupaka rangi na
aina mbalimbali za sanaa kwa watoto wadogo, kwani wameshafanya research
wakagundua kwamba vitu hivyo vinawafanya watoto kuwa na akili.
Watoto wanaojifunza sanaa huwa wanaperform vizuri sana hata
kwenye masomo mengine, pia huwa wana ubongo wa kujitegemea akak independent
mind.
Ufanyeje?
Nunua vitu vya kumsaidia kufanya mambo haya…rangi, painting books,
drawing papers au hata A4 za kawaida tunazotumia maofisini, markers, crayons,
udongo wa kuchezea watoto nk.
Usiogope ukuta kuchafuka, unaweza ukamtengea kasehemu ka
ukuta ukabandika makaratasi meupe, achore wee hadi achoke, pakichafuka, unatoa
ukuta wako unabaki msafi.
Hata kama mama/baba hujui kuchora (note
tu kuwa mie ni mchoraji mzuri sana, so huwa naenjoy sana hivi vitu)
jitahidi ufanye naye ukimsifu hata akichora mtu wa kijiti, sio lazima awe
mchoraji mahiri, ila nia ni kutanua ubongo wake…
No comments:
Post a Comment