Friday, February 1
Tujuzane tafadhali
Tuesday, February 9
Dawa ya watoto wanaokataa kula!
Inawezekana unandaa chakula safi sana lakini bado mtoto anasumbua kula ili kumbadilisha tabia apende kula unatakiwa kumtengenezea kwanza hamu ya kula maana bila ya kuwa na hamu ya kula hata chakula kiwe kizuri vipi huwezi kula vizuri.
Hamu ya kula inatakiwa kuanzia asubuhi unapofungua kinywa, tengeneza chai iwe ya rangi au ya maziwa weka tangawizi ya unga kwenye nusu lita ya maji au maziwa weka tangawizi kijiko kidogo cha chai mzoweshe mwanao chai hii kila siku asubuhi tangawizi ni kiungo kizuri kinachosaidia kumengenya chakula tumboni na kusababisha njaa haraka na hamu ya kula.
Hapo utakua umemtengenezea mtoto hamu ya kula mchana, kwa kumuandalia mtoto hamu ya kula chakula cha usiku tengeneza juisi ya Pasheni au Embe au Nanasi au tunda lolote lile kumbuka kuchanganya tena kijiko kidogo cha chai kilicho jaa tangawizi na usage pamoja na mchanyanyiko wako mpe mtoto glasi moja saafi kabla ya kula na mabadiliko utayaona usimpatie baada ya kula maana itamsababishia njaa.
*****
Nashkuru sana mdau uliyenitumia ushauri huu kwa e-mail, kwa kweli umetuelimisha sana.
*****
Sahihisho, source ya ushauri huu ni kutoka kwa Chef Issa.
Tuesday, November 10
Unajua nini kuhusu sheria ya mtoto iliyopitishwa bungeni juzijuzi?
Kwa furaha napenda kuwatangazia wadau kuwa Bunge letu tukufu kwa mara ya kwanza limepitisha sheria ya mtoto. Nasema kwa mara ya kwanza sababu Tanzania hatujawahi kuwa na sheria ya mtoto.
Sasa wewe kama mzazi na mtanzania kwa ujumla, una wajibu wa kujua yaliyomo kwenye sheria hii, maana unaweza kujikuta unapelekwa mahakamani bila kujua na na ukaishia kulipa fine kubwa au kutupwa lupango.
Ila kwa kuwa nipo hapa kwa ajili yako, huna shida ya kuusoma msheria woooote,(si mnawajua wanasheria kwa kutumia lugha ngumu?) usijali mi ntasoma, afu ntakua nakurushia vipande kidogo kidogo kwenye blog yako pendwa kwa lugha yetu (wanatuita laymen/women) tuliyoizoea.
Hata ukitaka Mama Sitta (waziri husika) ntaenda uongea nae, kwanza tumpe hongera kwa kufanikisha hilo, maana nae ana nia watanzania wengi waijue na kuielewa sheria hii.
Kwa kuanzia, ni kwamba sheria hii ni kwa mara ya kwanza imekusanya vipengele vyote vinavyohusu mtoto kwenye sheria nyingine na kuviweka pamoja, na hivyo kutengeneza mkusanyiko wa sheria moja ya issues za watoto tu. Zamani kila kitu kuhusu mtoto kilikua kwenye sheria mbalimbali, ukitaka mirathi, basi uende sheria ya mirathi, ukitaka matunzo, sijui uende wapi, ili mradi kila kitu kwake.
Katika sheria hii, pamoja na kuainisha haki za mtoto, zinawabana ipasavyo wazazi na walezi, pia kuna wajibu wa mtoto.
Pamoja na mambo mengine mengi, pia inazungumzia kuhusu kutumikisha watoto, haki ya mirathi kwa watoto (wa nje na ndani ya ndoa) kuasili watoto (adoption) na mambo mengine kibao.
Stay tuned hapahapa, wakati nikikupa kipengele kimoja baada ya kingine.
Friday, July 31
Unataka Mwanao Awe Genius?
Wednesday, May 20
Pacha Wenye Baba Tofauti
Huyu ni Jordan, na mama, Mia.Pacha hao, Jordan na Justin walizaliwa miezi 11 iliyopita, wakipishana dakika saba, na hamna mtu aliyehisi kuwa watakua na baba tofauti
Ila mama na baba waliamua kupata ushauri wa kitaalam baada ya kuona mapacha wao wa kiume wanazidi kuwa na sura tofauti kadri wanavyokua.
Vipimo navyo havikufanya hiana, kwani vikaonyesha kuwa uwezekano wa mapacha hao, waliokua kwenye tumbo moja kwa muda wa miezi tisa na kuzaliwa siku moja, kuwa na baba mmoja ni 0.01% .
Si mama tu aliyeshangaa, hadi madaktari wa maabara hiyo huko Texas walishangazwa na majibu hayo, kwani hawajawahi kuyaona, huwa wanasikia tu.Baada ya maji kumwagika ikabidi bibie Mia akiri kwamba wakati yuko na mchumba wake huyo alikua ana-cheat na jamaa mwingine, kusababisha pacha hao kuwa na baba tofauti.
“Nimeshtushwa sana, yani katika watu wote duniani, kitu hiki kinatokea kwangu,” alisema. Ila mchumba wake kaamua kusamehe na kusema yaliyopita si ndwele…na kusema kuwa ana nia ya kulea mapacha hao wote wawili kama wote wake.
Lakini alikiri kuwa ni alijisikia vibaya baada ya kupata ukweli huo, “Itachukua muda kujenga uaminifu kama ilivyokua mwanzo,” alisema.
Wazazi hao wamesama watawaambia hao watoto ukweli kuwa ingawa ni mapacha, baba zao ni tofauti watakapokua na akili ya kuelewa mambo hayo.
Inatokeaje Mapacha Wakawa na Baba Tofauti?
Kuna wakati mwanamke huwa anatoa mayai mawili, toka ovary zote mbili, kwa pamoja. Ikitokea mimba ikatunga wakati huu, ndio wanazaliwa mapacha wasiofanana, au kidhungu wanaitwa fraternal twins.
Kama mnavyojua, yai la mwanamke lina uwezo wa kukaa kwa masaa 24 kabla halijaharibika, na mbegu za mwanaume zinaweza kukaa hadi siku tano ndani ya mwili wa mwanamke.
Hapo ndipo mapacha kuwa na baba tofauti inapoweza kutokea, iwapo mwanamke atalala na wanaume wawili tofauti, ndani ya wakati yai liko tayari, na mayai yakawa yalitoka mawili tofauti, basi kuna uwezekano mkubwa yai moja likapevishwa na mbegu ya mwanaume mwingine, na lingine likapevushwa na mbegu ya mwanaume mwingine. Watoto watakua mapacha na watu watadhani ni wa baba mmoja, kumbe ni baba tofauti.
Ingawa inaonekana kama ni kitu kigumu kutokea, tafiti za karibuni nchini Marekani zinaonyesha kuwa katika seti 12 za mapacha, seti moja ni ya baba tofauti, huku watu wakilaumu mmomonyoko wa maadili kwenye jamii hiyo, sijui hapa kwetu ikoje.
Wednesday, May 13
34
Kumi
Kula ni Muhimu
*****
Watu wote tunajua kuwa mwili haujengwi kwa matofali, na pia tukumbuke kwamba pia haulindwi na wamasai wala Knight Support, kula ni muhimu sana kwa mtoto, ila iwe lishe bora sio bora lishe, watoto wengi hawapendi kula, so mlazimishe ale hata kama ni mlo mdogomdogo mara nyindi kwa siku, lakini usimwache anadhoofu kwa kusema mbishi sana kula.
Pia unene uliopitiliza sana haufai, mwili wa wastani kama Prince hapo ni mzuri.
Tuesday, May 12
Toys kwa Watoto Wadogo (0-9mths)
Toy hii, pamoja na pop-up toys zinafaa sana kwa watoto wadogo tangu kuzaliwa hadi miezi tisa (9).
Wataalam wanasema zinasaidia kuendeleza milango ya fahamu ya mtoto pia inasaidia mtoto kujua kuwa akifanya hivi hiki kinatokea, mfano akitingisha hiyo toy itatoa mlio.
Friday, May 8
Feni na Mtoto
Mtoto akiwa amelazwa sebuleni kwenye hewa ya kutosha
*****
Najua watu wengi wanaona, na mimi nikiwa mmojawapo, kuwa feni inasababisha magonjwa ya vifua kama mafua na kikohozi lakini utafiti unaonyesha kuwa feni inamsaidia mtoto, hasa kwenye vyumba ambapo hamna hewa nyingi.
Utafiti huo uliofanywa Califonia kwa jumla ya familia 497 kiila moja ikiwa na mtoto mchanga uligundua kuwa matumizi ya feni yalipunguza uwezekano wa vifo vya watoto visivyojulikana chanzo chake kwa asilimia 72.
Kati ya familia hizo, 185 zilikua zimeshafiwa na watoto kutokana na ugonjwa huo ambao kitaalam unaitwa SIDS, na wataalam waligundua kuwa watoto hao walikua wanalala kwenye vyumba ambavyo havikua na mzunguko wa hewa wa kutosha. Vifo vya SIDS huwa vinatokea watoto wakiwa wamelala tu, na hadi leo, ingawa research zilianza tangu miaka ya 80, haijulikani sababu ya vifo hivyo.
Moja ya njia ya kuzuia au kupunguza vifo hivyo ni kulaza watoto wachanga kimgongo (chali), badala ya kitumbotumbo (kifudifudi), na kuhakikisha kuwa chumbani anakolala mtoto kuna hewa ya kutosha au kutumia feni, ila usimwelekezee mtoto.
Thursday, April 9
Athari ya Chuchu Bandia Kwa Vichanga
Wednesday, April 1
Ijue Chanjo Mpya ya Watoto Inakayoanza Kutolewa Leo
Naibu waziri wa Afya, Mhe. Aisha Kigoda akitoa chanjo mpya kwa watoto aina ya ENTAVALENT yenye uwezo wa kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa sita ambayo inaanza kutolewa leo nchi nzima.Leo chanjo mpya kwa ajili ya watoto wenye umri kuanzia wiki 8 na hadi miaka mitano inaanza kutolewa nchi nzima. Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imetangaza kuanza kutumika rasmi kwa chanjo mpya aina ya “Pentavalent Vaccine” itakayokinga watoto dhidi ya magonjwa sita. Chanjo hiyo ni mbadala wa chanjo za aina tatu za zamani zilizokuwa zikitumika kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa hayo ambayo ni kifua kikuuu, polio, dondakoo, pepopunda, kifaduro, ugonjwa wa ini na surua.
Monday, January 12
Ufahamu: Apple Linasaidia Mtoto Tumboni
Utafiti uliyofanywa karibuni unaonyesha kuwa mjamzito anayekula tunda la apple mara kwa mara wakati akiwa mjamzito anapunguza uwezekano wa mwanae kupata ugonjwa wa pumu, yes, ukila apple tu mwanao anaweza asipate pumu.
Watafiti waliofanya utafiti huo, uliofanyika Holland, wanasema bado hawajajua kwa nini apple linasaidia watoto wasipate pumu, ila wanahisi ni virutubisho vilivyopo ndani ya tunda hilo.
Usitake kujua inakuaje, we kazana kula maaaple tu!



