Showing posts with label News. Show all posts
Showing posts with label News. Show all posts

Monday, April 30

Mtoto azaliwa na sehemu za siri kichwani


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mtoto wa ajabu amezaliwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, mjini Songea, ambapo maumbile yake ya sehemu za siri yako kichwani.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Mathayo Chanangula, alisema mtoto huyo alizaliwa Aprili 25, mwaka huu, saa saba mchana akiwa na uzito wa kilo 1.9 licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa.

Chanangula lifafanua kuwa kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa na uzito wa kilo 2.5. Pia alieleza sababu za kitaalamu zilizosababisha mtoto huyo kuzaliwa katika hali hiyo kuwa ni unywaji wa dawa zisizostahili kwa mama mjamzito kabla ya kutimiza miezi mitatu ya ujauzito.

Mtoto huyo kila anaponyonya, sehemu hiyo za siri ya jinsia ya kiume iliyo kichwani kwake inasimama kama vile anataka kujisaidia haja ndogo.

STORY KAMILI PATA HAPA

PICHA (sorry siwezi kuziweka hapa) ZIKO HUKU

Sunday, November 28

Mwanafunzi afa baada ya kucharazwa viboko

MWANAFUNZI wa kike wa darasa la sita, amekufa kutokana na madai ya kupigwa viboko na mwalimu wake aliyekuwa akimtuhumu kufeli jaribio la hisabati.

Mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi Mawenzusi wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, alifikwa na mauti hayo juzi katika Hospitali ya Dk. Atman alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka mjini humo, Kamanda wa Polisi, Isuto Mantage alidai mwanafunzi huyo alipata kipigo hicho Novemba 16, mwaka huu.

Alidai kuwa siku ya tukio mwalimu wa somo hilo, Richard Langson (23) aliingia darasani na kutoa jaribo la hisabati na kuwaonya wanafunzi wake kwamba atakayepata alama chini ya asilimia 70, atapata adhabu ya viboko. 
Jamani, mi viboko sijawahi kuvipenda, na wala sivipendi, hasa vinapokua havina nia ya kufundisha bali kukomoa, naona tu tuanzishe kampeni viboko vifutwe mashuleni, kama watoto hawasikii basi, hasara kwetu wazazi sio kutuulia watoto wetu!!!

Thursday, November 25

Mtoto azaliwa ubongo nje Morogoro


Kichwa cha mtoto huyo kinavyoonekana

Mtoto mmoja amezaliwa ubongo ukiwa nje baada ya kukosa ngozi ya kichwa huku akiwa mwenye afya njema katika hospitali ya Wilayani Ulanga mkoani Morogoro .
Mtoto huyo wa kiume aliyezaliwa siku ya jumatatu majira ya saa tatu usiku,
atampelekwa katika hospitali kubwa mkoani Morogoro kwa uchunguzi zaidi wa nini kifanyike kukabiliana na tatizo la mtoto huyo ambaye hadi sasa yupo hai na afya njema.

Matroni wa wodi ya kina mama bi. Haule akimhudumia mtoto na aliyembeba ni Bi Sabina Lyombo mama wa mtoto

Kaimu Mganga Mkuu (W) Dkt Amani Kombe amesema  kuwa hali ya mtoto kuzaliwa na kukosa ngozi ya kichwa hutokea wakati wa uumbaji wa viungo mbalimbali vya mwili wa mtoto na hali hiyo huweza kusababishwa na ukosefu wa madini mbalimbali kwa mama wakati wa ujauzito aidha ni tukio la kwanza kutokea katika hospitali hiyo ya wilaya.
Mama wa mtoto bi. Silvia Lyombo (20) ambaye ni ujauzito wake wa kwanza alisema kuwa hakupata matatizo yoyote ya kiafya wakati wa ujauzito na alijifungua katika hali ya kawaida mtoto mwenye uzito wa kilo 2.9 na kuwa ananyonya kama kawaida na hana tatizo lolote zaidi ya kukosekana kwa ngozi ya kichwa aidha hakuna dawa zozote ambazo alizitumia katika kipindi chote cha ujauzito wake.

Friday, August 13

NAN 2 nayo out!


NAN 2 ya ukweli ikilinganishwa na ya bandia...yote yamepigwa marufuku hadi taarifa zaidi itakapotolewa.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imepiga marufuku  marufuku uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya maziwa yote ya NAN 2 baada ya kugundua uwepo wa maziwa hayo ya bandia.

Akizungumza na  waandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, alisema mamlaka hiyo imechukua hatua hiyo kutokana na ugumu wa mwananchi wa kawaida  kugundua maziwa bandia ya NAN 2 kutokana na makopo yake kufanana sana na maziwa halisi.

Pamoja na hayo mamlaka hiyo bado iko katika uchunguzi wa kubaini mtengenezaji na athari zitokanazo na maziwa hayo bandia ukifanyika.

TFDA ilikamata  makopo 2,261 ya maziwa bandia ya watoto wachanga aina ya NAN 2.
Maziwa ya watoto yanayoruhusiwa na TFDA Lactogen 1 Infant Formula, Lactogen 2 Follow up Formula and Cowberry Infant Formula ambayo yametengenezwa Ufaransa na NAN 1 Starter Infant Formula yatangenezwayo Uholanzi.

Tuesday, May 25

Tangazo la utoaji mimba kwenye Tv

Shirika la afya ya uzazi, ambalo pia lina clinic hata hapa nchini, Marie Stopes limetengeneza tangazo la televisheni kuhusu huduma za utoaji mimba.

Tangazo hilo litakalorushwa Uingereza (kasoro Ireland ambako kutoa mimba ni kosa) kuanzia wiki ijayo linauliza 'ARE YOU LATE ?' likimaanisha umechelewa siku zako?

Ingawa limeshaanza kuzua maswali mengi hasa kwa wanaharakati wa kupinga utoaji mimba, wenyewe Marie Stopes wanasema kuwa nia sio kuwaamasisha watu watoe mimba, bali kuwapa wanawake waliopata mimba bila kupanga ushauri usioegemea upande wowote na hivyo kumpa mwanamke huyo nafasi ya kuchagua kutoa au kubaki na hiyo mimba akiwa na taarifa sahihi.




Tuesday, December 15

Hatimaye TFDA waorodhesha maziwa yanayoruhusiwa

At last, Mamlaka ya Uthiditi wa Chakula na Dawa (TFDA) wametoa orodha na ku-endorse (sijui kiswahili chake) maziwa yanayofaa kwa watoto, ambayo ni yafuatayo, na nchi zinazotengeneza:
  • Lactogen 1 infant Formula - South Africa
  • Lactogen 2 Follow up Formula - South Africa
  • NAN 1 Infant Formula - South Africa
  • NAN 2 Infant Formula - South Africa
  • Lactogen 1 Infant Formula- France
  • Lactogen 2 Follow-up formula - France
  • NAN 2 Infant Formula - France
  • Cow Bell Infant Formula - France
  • NAN 1 Infant Formula - Holland
(sorry, picha nimeshindwa kupata, maana nimeona zinanichanganya, so ili kutowachanganya na nyie nimeona niachane nazo).

Akiongea na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Margareth Ndomondo-Sigonda alisema kuwa mamlaka hiyo imeamu kuwa waingizaji wa bidhaa hizo lazima wapate kibali cha mamlaka hiyo kila wanapotaka kuingiza bidhaa hizo.
Pia amewashauri wananci kutumia bdhaa zilizohalalishwa na mamlaka hiyo kujiepusha na matatizo ya kiafya.
Hayo yote yalikuja kutokana na kukamata makopo zaidi ya 14,000 ya vyakula feki, yakiwemo maziwa ya watoto ya S-26 (yalishakatazwa haya), SMA, Isomil, Cow & Gate Infant Formula, Infantcare, Nutrient optium na Ifasoy.
Wazazi tujiadhari na hizi formula, nunua hayo yaliyoklua endorsed na hakikisha ni kutoka nchi zilizotajwa hapo, au kama vipi, jichanganye kwenye maziwa ya ng'ombe wa mtaa wa pili, ila kama mwanao ni chini ya mwaka mmoja, inabidi ufuate process maalum ili yamfae.

Saturday, September 12

Mtanzania Kushtakiwa Kwa Kuua Mwanae Marekani

Mtanzania aitwae Ibrahim Kibayasi (29), anategemewa kushtakiwa kwa mauaji ya mtoto mwenye umri wa miezi mitano, ambaye ni mwanae mwenyewe, aliyefariki Jumatano iliyopita huko Marekani.

Mtanzania huyo tayari alishakamatwa tarehe 3 mwezi huu na kufunguliwa kesi ya kumtesa mtoto wakati mtoto huyo akiwa amelazwa hospitali, ambapo kesi hiyo itabadilishwa baada ya mtoto huyo kufariki dunia hospitalini hapo.

Kibayasi alikua anamwangalia mtoto huyo wakati mama wa mtoto ambaye ni Mmarekani akiwa kazini. Lakini mtanzania huyo alikasirishwa na mtoto huyo na kuamua kumtikisatikisa kwa nguvu kabla ya kumrushia kitandani.

Baadae, Kibayasi akamchukua mtoto na kwenda nae kumchukua mama kazini, ambapo mama mtu aligutukia kwamba mtoto hapumui vizuri, na kuamua kupiga 911, ambapo mtoto alipelekwa hospitali.

Madaktari waligundua kuwa mtoto huyo alipata majeraha mwilini, na pia alikua na mbavu zinazoanza kupona ambapo uchunguzi ulionyesha kuwa zizovunjika zamani.

Bila aibu mtanzania huyo alikiri kuwa zamani kidogo alishawahi kumbana kwa nguvu mbavuni maialka huyo wa miezi mitano na kusababisha majeraha hayo, lakini hakumpeleka mtoto hospitali.

Mtanzania huyo alikua anaishi Marekani kinyume cha sheria kwani aliingia miaka saba iliyopita kwa viza ya wanafunzi ambayo ilishaisha muda. Alikua anaishi Mount Prospect Illinois.

Mungu ailaze roho ya malaika asiye na hatia mahali pema peponi, na katili huyo ahukumiwe ipasavyo!

Wednesday, September 2

Maziwa Yapi Bora?

Wadau, kama mnavyojua S26 yashakatazwa kwani ni hatari kwa watoto, sasa wadau wengi wanauliza maziwa yapi ni mazuri? Mi siwezi kushauri chochote hapa, X hajawahi kunywa maziwa ya kopo, nilimnyonyesha halafu baadae akaanza kunywa maziwa ya ng'ombe, bahati mtaani kwangu kuna watu wanafuga, na ni waaminifu, hawachanganyi maji wala kukamua ang'omba akitoka kuchoma sindano.
Mwenye ushauri atusaidie jamani, maana watoto waliokuwa wanatumia S26 hawana maziwa sasa, wazazi wamechanganyikiwa.

Tuesday, September 1

Tahadhari Zaidi...S 26 Bado Zinauzwa

Taafira za kuaminika nilizopokea hivi pinde zinasema maziwa haya yaliyokatazwa, S26 bado yapo madukani, kwa hiyo nachukua nafasi hii kuwataadharisha tena wadau ambao walikua hawajajua kwamba maziwa haya yamekatazwa kwani ni hatari kwa watoto.

Saturday, August 29

Tahadhari - S26 Yapigwa Marufuku

Wadau, naomba mnisamehe kwa kuchelewesha taarifa hii...hata sina cha kujitetea.
*****
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imepiga marufuku matumizi ya maziwa ya watoto wachanga ya S26 yanayotengenezwa Afrika Kusini baada ya kubainika yana madhara kwa watoto.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Margareth Ndomondo, amesema kuwa mamlaka hiyo imefikia maamuzi hayo baada ya uchunguzi uliofanywa baada ya kupokea taarifa kwa nyakati tofauti ya kuwepo katika soko maziwa hayo ambayo yamesababisha madhara kwa watoto wachanga na kuamua kufanya ukaguzi katika maduka na maghala ya vyakula ili kubaini ukweli wake.
Alisema taarifa hizo zilieleza kuwa watoto waliotumia maziwa hayo yanayotengenezwa Afrika Kusini, walipiga chafya, kupata maumivu ya tumbo, kutapika na wengine kuharisha. Pia alisema taarifa nyingine zilidai kuwa maziwa hayo hayayeyuki vizuri katika maji na yana harufu mbaya kama mafuta ya kula yaliyoharibika ambapo kutokana na ukaguzi, taarifa hizo zilikuwa za kweli.
“Katika ukaguzi huo, jumla ya makopo 38,560 ya S26 yenye madini ya chuma ya ujazo wa gramu 400 kwa kila kopo yaliyotengenezwa na kampuni ya Pharmacare Ltd, Woodmead-Sandton yalikutwa sokoni na sampuli zake kuchukuliwa kwa uchunguzi zaidi,” alisema Ndomondo.
Alisema uchunguzi wa kimaabara ulibaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha tindikali huru za mafuta (free fatty acids) na kemikali aina ya peroxide, hali ambayo inaashiria kuharibika kwa mafuta yaliyomo katika maziwa hayo na hivyo kutofaa kwa matumizi ya binadamu.
TFDA imezuia matumizi ya maziwa hayo ya S26 kutoka Afrika Kusini na inawataka wananchi kutoyatumia na endapo watabaini kuwepo kwa maziwa hayo madukani, watoe taarifa kwa mamlaka makao makuu au katika ofisi za kanda na ofisi za afya za mikoa na halmashauri ili hatua zichukuliwe.

School Bus Zote Kupakwa Rangi ya Njano

Karibuni mabasi ya yote ya wanafunzi yatafananania hili.
*****

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), itaanza kutoa leseni maalumu, kuyapaka rangi ya njano na kuandikwa maandishi makubwa ya ‘Basi la Wanafunzi’ au 'School Bus' kwa rangi nyeusi kwenye mabasi yanayobeba wanafunzi nchi nzima.

Utaratibu huo ni kwa mabasi yanayomilikiwa na shule binafsi, za umma na taasisi za kidini, na wamiliki wake wamepewa miezi sita kuwa wameshachukua leseni hizo na kupaka rangi, na baada ya kipindi hicho kumalizika, watachukuliwa hatua.

Imeelezwa kuwa hatua hiyo itaanzia katika Jijini dsm baada ya kugundua idadi kubwa ya daladala zilizosajiliwa kubeba abiria, zinabeba wanafunzi wa shule mbalimbali katika nyakati za asubuhi na jioni, hivyo kusababisha usumbufu kwa abiria.

SUMATRA imesema kuwa awali mabasi ya kubeba wanafunzi yalikuwa yakipewa leseni zinazowataka kupita katika njia zote, lakini sasa itakuwa na leseni maalumu ya kubeba wanafunzi tu zenye rangi ya njano na kuandikwa kwa maandishi makubwa kwa rangi nyeusi School Bus au Basi la Wanafunzi. Mziray alisema pia wamewaagiza wamiliki kuyaweka mabasi hayo ya wanafunzi katika hali ya usalama na ubora na kuepuka kuwapakia zaidi ya idadi ya viti vilivyomo.

*****

Mi naona ni vizuri kwa utambulisho, hata kwa mbali, na maderava wengine wanajua kabisa hili ni basi la wanafunzi, ni vizuri kwa usalama wa watoto…na kweli hiyo tabia ya kukodi basi la abiria kila asubuhi na jioni itaisha. Big up Sumatra!

Tunasubiri school bus za public schools, mavumbini kwetu, tu!

Tuesday, June 2

Daktari Bingwa Mtoa Mimba Auawa

Dr George Tiller
*****
Daktari bingwa wa kutoa mimba kubwa, Dr. George Tiller amepigwa risasi na kufa hapohapo, alipokua anahudhuria misa kwenye Kanisa la Kirutheri la Reformation Jumapili hii, huko Marekani.
Kwa muda mrefu Dr Tiller alikua anatafutwa na watu wanaopinga utoaji mimba nchini marekani, na mara kwa mara yeye na familia yake wamepokea vitisho mbalimbali kutokana na kazi yake. Mkewe alishuhudia mauaji hayo akiwa amesimama anaimba kwaya mbele ya kanisa.
Br Tiller alikua anamiliki klinik moja kati ya tatu tu nchini Marekani ambazo zinatoa mimba iliyopita wiki 21, ila mimba hizo ziliku hazitolewi kwa sababu ya kutoa mimba tu, zilikua na sababu zake.
Dr Tiller alikuwa akiamini kwamba akina mama ambao imeshaonekana kuwa watoto wao ambao bado hawajazaliwa wana ulemavu uliopitiliza au magonjwa mabaya sana wana haki ya kuamua kutoa au kutotoa mimba.
Na kwa sababu matatizo hayo mara nyingi yanagundulika mimba ikishakua kubwa, ndio maana Dr Tiller alikua anatoa mimba ambazo ni kubwa sana, kitu ambacho ni hatari kwa mama mjamzito, na ni madaktari wachache kama yeye waliokua wanakiweza.
Kutokana na kazi yake hiyo Dr Tiller alishapigwa risari kwenye mikono yote miwili mwaka 1993 na klinik yake, Women's Health Care Services, ilishapigwa mabomu mwaka 1985.
Kutokana na hayo, Dr Tiller alikua anatembea na walinzi na madirisha ya klinik yake yalikua hayapitishi risasa, lakini wauaji hao walimpata kwenye sehamu ambayo hakutegemea kabisa, kanisani. Pia cha ajabu zaidi ni kwamba, hawa waaliomuua daktari huyu wanajiita pro-life (yani wanahamasisha watu wasitoe mimba kwa sababu kila mtu ana haki ya kuishi).
Sijui wadau mnaonaje kuhusu hili, ila mimi binafsi sijapenda, ukizingatia huyu dokta alikua hatoi tu mimba kwa sababu zisizo za msingi, sababu zake zilikua za msingi kabisa.

*****

Hapa kwetu kutoa mimba ni kosa la jinai, ingawa ni ukweli usiopingika kwamba wasichana wengi wanatoa mimba kila siku, na wengine wanakufa au kupata matatizo ya kiafya ambayo yanawafanya wasije kuzaa tena maishani mwao.
Hili suala limewagawanya watu kwenye makundi matatu makubwa, (ingawa kuna mengine madogodogo):
  • Watu wengi wanapinga kabisa utoaji mimba kwani wanaona kuwa kutoa mimba ni dhambi kubwa kama kuua, hivyo isihalalishwe kabisa.
  • Baadhi ya nchi wanaruhusu hadi mimba ya wiki 12 (ambayo ni kidaktara inakua bado ni salama kutoa) ila zaidi ya hapo ni kosa, na wanaounga mkono hili wanasema sababu ni kwama mtoto anakua bado hajaumbika vizuri.
  • Na kuna wachache wanaoona kutoa mimba yeyote ile ni sawa, na wanaona kutoa mimba ihalalishwe.
Wadau mnaonaje?
Piga kura hapo kulia...

Thursday, May 21

Watoto wa Mbagala Wakipimwa Masikio


Wanafunzi wa shule za msingi Mbagala takriban wiki sasa wanapatiwa huduma ya kuangalia masikio na macho iwapo kama yameathiriwa na milipuko ya mabomu.
Wadau wa Mama na Mwana tuzidi kuwaombea kheri hawa wenzetu, maana yaliyowakuta ni makubwa, kuna waliopoteza watoto, wengine hawajawaona hadi leo, na wengine ndio wamepate ulemavu wa viungo.
(Picha hisani ya Father Kidevu)

Wednesday, May 20

Pacha Wenye Baba Tofauti



Huyu ni Jordan, na mama, Mia.

Huyu ni Justin, na mama, Mia.
Mwanadada Mia Washngton na mchumba wake James Harrison walikua watu wenye furaha baada ya watoto waliowasubiri kwa miezi tisa, kuzaliwa wakiwa na afya njema.
Pacha hao, Jordan na Justin walizaliwa miezi 11 iliyopita, wakipishana dakika saba, na hamna mtu aliyehisi kuwa watakua na baba tofauti
Ila mama na baba waliamua kupata ushauri wa kitaalam baada ya kuona mapacha wao wa kiume wanazidi kuwa na sura tofauti kadri wanavyokua.
Vipimo navyo havikufanya hiana, kwani vikaonyesha kuwa uwezekano wa mapacha hao, waliokua kwenye tumbo moja kwa muda wa miezi tisa na kuzaliwa siku moja, kuwa na baba mmoja ni 0.01% .
Si mama tu aliyeshangaa, hadi madaktari wa maabara hiyo huko Texas walishangazwa na majibu hayo, kwani hawajawahi kuyaona, huwa wanasikia tu.Baada ya maji kumwagika ikabidi bibie Mia akiri kwamba wakati yuko na mchumba wake huyo alikua ana-cheat na jamaa mwingine, kusababisha pacha hao kuwa na baba tofauti.
“Nimeshtushwa sana, yani katika watu wote duniani, kitu hiki kinatokea kwangu,” alisema. Ila mchumba wake kaamua kusamehe na kusema yaliyopita si ndwele…na kusema kuwa ana nia ya kulea mapacha hao wote wawili kama wote wake.
Lakini alikiri kuwa ni alijisikia vibaya baada ya kupata ukweli huo, “Itachukua muda kujenga uaminifu kama ilivyokua mwanzo,” alisema.
Wazazi hao wamesama watawaambia hao watoto ukweli kuwa ingawa ni mapacha, baba zao ni tofauti watakapokua na akili ya kuelewa mambo hayo.

Inatokeaje Mapacha Wakawa na Baba Tofauti?
Kuna wakati mwanamke huwa anatoa mayai mawili, toka ovary zote mbili, kwa pamoja. Ikitokea mimba ikatunga wakati huu, ndio wanazaliwa mapacha wasiofanana, au kidhungu wanaitwa fraternal twins.
Kama mnavyojua, yai la mwanamke lina uwezo wa kukaa kwa masaa 24 kabla halijaharibika, na mbegu za mwanaume zinaweza kukaa hadi siku tano ndani ya mwili wa mwanamke.
Hapo ndipo mapacha kuwa na baba tofauti inapoweza kutokea, iwapo mwanamke atalala na wanaume wawili tofauti, ndani ya wakati yai liko tayari, na mayai yakawa yalitoka mawili tofauti, basi kuna uwezekano mkubwa yai moja likapevishwa na mbegu ya mwanaume mwingine, na lingine likapevushwa na mbegu ya mwanaume mwingine. Watoto watakua mapacha na watu watadhani ni wa baba mmoja, kumbe ni baba tofauti.
Ingawa inaonekana kama ni kitu kigumu kutokea, tafiti za karibuni nchini Marekani zinaonyesha kuwa katika seti 12 za mapacha, seti moja ni ya baba tofauti, huku watu wakilaumu mmomonyoko wa maadili kwenye jamii hiyo, sijui hapa kwetu ikoje.

Monday, March 9

Sehemu Zenye Mkusanyiko wa watu ni Hatari Kwa Watoto

Mwanafunzi wa shule ya msingi Mnazi mmoja, Abdulatif Selemani (aliyelala) akipepewa na wasamaria wema baada ya kuzirai kukanyagwa kutokana na vurugu za kutaka kuwaona wachekeshaji wa kundi la ‘Orijino Komedi’ wakati wa uzinduzi wa Siku ya Wanawake Duniani, Viwanja vya Mnazi Mmoja, wiki ilkiyopita.
Ni muhimu sana wazazi na walezi kuwafundisha watoto kuwa makini sehemu zenye watu wengi, saa nyingine watoto huwa wanaumia kwa kukanyagwa. (Picha na Fadhili Akida)

Tuesday, February 24

Mtoto Mzuri Aliuzwa Laki Moja!

Fatma Kisawiro akiwa na mama yake mzazi, Tabu William Polisi, Dar es Salaam.
*****
MTOTO, Fatma Kisawiro mwenye umri wa miezi tisa aliyezua utata baada ya mama yake mzazi, Tabu William(36) kudai kuwa amemuuza kwa sh 100,000 amepatikana akiwa hai Chalinze mkoani Pwani.
Mtoto huyo kwenye picha yake hapo juu amerudishwa kwa mama huyo huyo anayeandaliwa mashitaka ili ajibu tuhuma za kumuuza mwanae.
Jamani wazazi tunaenda wapi?
Wakati wengine wanatafuta watoto kwa udi na uvumba, wengine hawawataki.

Monday, February 9

Matokeo ya Form Four- Girls Wanazidi Kuwaburuza Boys

Wasichana wa Marian Girls, ya Bagamoyo, wakifurahia matokeo ya dada zao. Ukimleta mwanao hapa (ila kuingia ni kazi!) una uhakika wa kufaulu, maana mwanzilishi wa shule hiyo, Father Bayo anasema wao wanataka wote wapate one, na wote wafike chuo kikuu, mzazi utake nini kingine...?
*****
Matokeo yametoka jana, ila coz ya mizunguko ya hapa na pale, nilishindwa kurusha jana. Lakini, nimewaletea picha ya mmoja wa wasichana walopo kwenye top ten ya mmojammoja, ambapo tisa ni wasichana, watano toka Marian, wanne St Francis na huyo mvulana mmoja ndio toka Uru.

Hongera wooote mliofanya vizuri, walimu asanteni kwa kazi nzuri, wazazi na wengine wote hongereni, wasichana mliochana asanteni.


Top Ten
  1. St Francis Girls (Mbeya)
  2. Marian Girls (Pwani)
  3. St Joseph-Kilocha Seminary (Iringa)
  4. Uru Seminary (Kilimanjaro)
  5. Dungunyi Seminary (Singida)
  6. Anwarite Girls (Kilimanjaro)
  7. St Mary Goreti (Kilimanjaro)
  8. Feza Boys (Dar es Salaam)
  9. Don Bosco Seminary (Iringa)
  10. Rosmini (Tanga)

Na zile shule zilizofanya vibaya tunazitangaza ili zione aibu zijivute kidogooo.
Last Ten
  1. Selembala (Morogoro)
  2. Kilindi (Pemba)
  3. Ngwachani (Pemba)
  4. Michiga (Mtwara)
  5. Ummusalama (Pwani)
  6. Chunyu (Dodoma)
  7. Busi (Dodoma)
  8. Uondwe (Pemba)
  9. Nala (Dodoma)
  10. Maawal (Tanga)