Wednesday, September 2

Maziwa Yapi Bora?

Wadau, kama mnavyojua S26 yashakatazwa kwani ni hatari kwa watoto, sasa wadau wengi wanauliza maziwa yapi ni mazuri? Mi siwezi kushauri chochote hapa, X hajawahi kunywa maziwa ya kopo, nilimnyonyesha halafu baadae akaanza kunywa maziwa ya ng'ombe, bahati mtaani kwangu kuna watu wanafuga, na ni waaminifu, hawachanganyi maji wala kukamua ang'omba akitoka kuchoma sindano.
Mwenye ushauri atusaidie jamani, maana watoto waliokuwa wanatumia S26 hawana maziwa sasa, wazazi wamechanganyikiwa.

3 comments:

Anonymous said...

jamani mama X,labda watu wajaribu maziwa ya SMA GOLD kwa mwenye kuzaliwa mpaka 6month na SMA PROGRESS kwa 6month up to 2yrs. ni mazuri sana. watafute ya Ireland. ni expensive kidogo lakini ni bora. kuliko kumpa mtoto kisicho bora. safari njema kuelekea mbinga wasalimie wakina mapunda, matembo na wotewote si unajua tena tunapenda majina ya wanyama.

joyce said...

hello wadau! poleni sana wale walinaopata shida ya maziwa ya kuwapa watoto wao,kwa kweli ni kazi, mimi mdau colman nilimwanzishia maziwa ya ng`ombe bahati yakamkataa nikashauriwa na dr wawatoto huku arusha nimpe maziwa ya SOYA REGULAR, niliambiwa nimpe mpaka afikishe mwaka mmoja, kwakweli hayakumletea shida yoyote ni mazuri sana tu, ila sasa mdau Colman ana mwaka na mwezi sasa

Anonymous said...

hello wadau! poleni sana wale walinaopata shida ya maziwa ya kuwapa watoto wao,kwa kweli ni kazi, mimi mdau colman nilimwanzishia maziwa ya ng`ombe bahati yakamkataa nikashauriwa na dr wawatoto huku arusha nimpe maziwa ya SOYA MILK REGULAR,kutoka south Afrika,yako kwenye box ya bluu ni ya maji sio ya unga, wakati unachemsha unapima maziwa yawe sawa na maji,km ni nusu lita maziwa, nusu lita ya maji, niliambiwa nimpe mpaka afikishe mwaka mmoja, kwakweli hayakumletea shida yoyote ni mazuri sana tu, ila sasa mdau Colman ana mwaka na mwezi sasa