Saturday, September 12

Mtanzania Kushtakiwa Kwa Kuua Mwanae Marekani

Mtanzania aitwae Ibrahim Kibayasi (29), anategemewa kushtakiwa kwa mauaji ya mtoto mwenye umri wa miezi mitano, ambaye ni mwanae mwenyewe, aliyefariki Jumatano iliyopita huko Marekani.

Mtanzania huyo tayari alishakamatwa tarehe 3 mwezi huu na kufunguliwa kesi ya kumtesa mtoto wakati mtoto huyo akiwa amelazwa hospitali, ambapo kesi hiyo itabadilishwa baada ya mtoto huyo kufariki dunia hospitalini hapo.

Kibayasi alikua anamwangalia mtoto huyo wakati mama wa mtoto ambaye ni Mmarekani akiwa kazini. Lakini mtanzania huyo alikasirishwa na mtoto huyo na kuamua kumtikisatikisa kwa nguvu kabla ya kumrushia kitandani.

Baadae, Kibayasi akamchukua mtoto na kwenda nae kumchukua mama kazini, ambapo mama mtu aligutukia kwamba mtoto hapumui vizuri, na kuamua kupiga 911, ambapo mtoto alipelekwa hospitali.

Madaktari waligundua kuwa mtoto huyo alipata majeraha mwilini, na pia alikua na mbavu zinazoanza kupona ambapo uchunguzi ulionyesha kuwa zizovunjika zamani.

Bila aibu mtanzania huyo alikiri kuwa zamani kidogo alishawahi kumbana kwa nguvu mbavuni maialka huyo wa miezi mitano na kusababisha majeraha hayo, lakini hakumpeleka mtoto hospitali.

Mtanzania huyo alikua anaishi Marekani kinyume cha sheria kwani aliingia miaka saba iliyopita kwa viza ya wanafunzi ambayo ilishaisha muda. Alikua anaishi Mount Prospect Illinois.

Mungu ailaze roho ya malaika asiye na hatia mahali pema peponi, na katili huyo ahukumiwe ipasavyo!

1 comment:

Anonymous said...

Shaken baby syndrom au la
http://www.thenhf.com/vaccinations_18.htm

http://www.shirleys-wellness-cafe.com/shakenbabysyndrome.htm