Saturday, August 29

Tahadhari - S26 Yapigwa Marufuku

Wadau, naomba mnisamehe kwa kuchelewesha taarifa hii...hata sina cha kujitetea.
*****
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imepiga marufuku matumizi ya maziwa ya watoto wachanga ya S26 yanayotengenezwa Afrika Kusini baada ya kubainika yana madhara kwa watoto.
Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Margareth Ndomondo, amesema kuwa mamlaka hiyo imefikia maamuzi hayo baada ya uchunguzi uliofanywa baada ya kupokea taarifa kwa nyakati tofauti ya kuwepo katika soko maziwa hayo ambayo yamesababisha madhara kwa watoto wachanga na kuamua kufanya ukaguzi katika maduka na maghala ya vyakula ili kubaini ukweli wake.
Alisema taarifa hizo zilieleza kuwa watoto waliotumia maziwa hayo yanayotengenezwa Afrika Kusini, walipiga chafya, kupata maumivu ya tumbo, kutapika na wengine kuharisha. Pia alisema taarifa nyingine zilidai kuwa maziwa hayo hayayeyuki vizuri katika maji na yana harufu mbaya kama mafuta ya kula yaliyoharibika ambapo kutokana na ukaguzi, taarifa hizo zilikuwa za kweli.
“Katika ukaguzi huo, jumla ya makopo 38,560 ya S26 yenye madini ya chuma ya ujazo wa gramu 400 kwa kila kopo yaliyotengenezwa na kampuni ya Pharmacare Ltd, Woodmead-Sandton yalikutwa sokoni na sampuli zake kuchukuliwa kwa uchunguzi zaidi,” alisema Ndomondo.
Alisema uchunguzi wa kimaabara ulibaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha tindikali huru za mafuta (free fatty acids) na kemikali aina ya peroxide, hali ambayo inaashiria kuharibika kwa mafuta yaliyomo katika maziwa hayo na hivyo kutofaa kwa matumizi ya binadamu.
TFDA imezuia matumizi ya maziwa hayo ya S26 kutoka Afrika Kusini na inawataka wananchi kutoyatumia na endapo watabaini kuwepo kwa maziwa hayo madukani, watoe taarifa kwa mamlaka makao makuu au katika ofisi za kanda na ofisi za afya za mikoa na halmashauri ili hatua zichukuliwe.

2 comments:

Anonymous said...

twashukuru jiang kwa information yako...wazazi tuna tabu saaana na maziwa ya watoto...Inshallah..mungu atatujalia..

shamim a.k.a Zeze said...

TENA NILITAKA NIKWAMBIE HII SERIKALI NAYO HAIJATULIA WAO WAMEBIPIGA MARUFUKU TUSITUMIE SASA WATUAMBIE TUTUMIE NINI AU WATOTO WETU TUWAPE CHAI??? NA IWEJE WAYARUHUSU HAYO MAZIWA YAINGIE NDANI YATUMIEKE NDO YAWAKATAZE...HAWAKO SERIOUZ HAWA WATU