Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), itaanza kutoa leseni maalumu, kuyapaka rangi ya njano na kuandikwa maandishi makubwa ya ‘Basi la Wanafunzi’ au 'School Bus' kwa rangi nyeusi kwenye mabasi yanayobeba wanafunzi nchi nzima.
Utaratibu huo ni kwa mabasi yanayomilikiwa na shule binafsi, za umma na taasisi za kidini, na wamiliki wake wamepewa miezi sita kuwa wameshachukua leseni hizo na kupaka rangi, na baada ya kipindi hicho kumalizika, watachukuliwa hatua.
Imeelezwa kuwa hatua hiyo itaanzia katika Jijini dsm baada ya kugundua idadi kubwa ya daladala zilizosajiliwa kubeba abiria, zinabeba wanafunzi wa shule mbalimbali katika nyakati za asubuhi na jioni, hivyo kusababisha usumbufu kwa abiria.
SUMATRA imesema kuwa awali mabasi ya kubeba wanafunzi yalikuwa yakipewa leseni zinazowataka kupita katika njia zote, lakini sasa itakuwa na leseni maalumu ya kubeba wanafunzi tu zenye rangi ya njano na kuandikwa kwa maandishi makubwa kwa rangi nyeusi School Bus au Basi la Wanafunzi. Mziray alisema pia wamewaagiza wamiliki kuyaweka mabasi hayo ya wanafunzi katika hali ya usalama na ubora na kuepuka kuwapakia zaidi ya idadi ya viti vilivyomo.
*****
Mi naona ni vizuri kwa utambulisho, hata kwa mbali, na maderava wengine wanajua kabisa hili ni basi la wanafunzi, ni vizuri kwa usalama wa watoto…na kweli hiyo tabia ya kukodi basi la abiria kila asubuhi na jioni itaisha. Big up Sumatra!
Tunasubiri school bus za public schools, mavumbini kwetu, tu!
No comments:
Post a Comment