Wednesday, April 1

Ijue Chanjo Mpya ya Watoto Inakayoanza Kutolewa Leo

Naibu waziri wa Afya, Mhe. Aisha Kigoda akitoa chanjo mpya kwa watoto aina ya ENTAVALENT yenye uwezo wa kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa sita ambayo inaanza kutolewa leo nchi nzima.
Hapa ni kwenye uzinduzi uliofanyika Kisarawe Juamtatu hii.
*****

Leo chanjo mpya kwa ajili ya watoto wenye umri kuanzia wiki 8 na hadi miaka mitano inaanza kutolewa nchi nzima. Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imetangaza kuanza kutumika rasmi kwa chanjo mpya aina ya “Pentavalent Vaccine” itakayokinga watoto dhidi ya magonjwa sita. Chanjo hiyo ni mbadala wa chanjo za aina tatu za zamani zilizokuwa zikitumika kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa hayo ambayo ni kifua kikuuu, polio, dondakoo, pepopunda, kifaduro, ugonjwa wa ini na surua.
Akitangaza kuanza kutumika kwa chanjo hiyo jijini wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Huduma wa Wizara ya Afya Dk. Donnan Mmbando, amesema chanjo hiyo imeongezwa nguvu ya protini na imeshaonyesha mafanikio katika nchi za Kenya na Uganda ambako imekuwa ikitumika miaka tisa iliyopita, na taarifa nilizonazo, sisi ni moja ya nchi za mwisho kuanza kutumia chanjo hiyo. Chanjo hiyo itatolewa bure kwa watoto wakati watakapokuwa akihudhuria kliniki zao za kawaida.
Kama unaishi Tanzania na mwanao bado anaenda klinik na hajapata zile chanjo za zamani kuzuia magonjwa hayo, au bado u mjamzito, basi jiandae na chanjo hii, ila pia shukuru kwani sindano zitapungua kwa wanetu wachanga.

2 comments:

mama nashdigo said...

samahani jamani naomba kueleweshwa juu ya hilo. inamaana kama mtoto alichoma zile za mwanzo hachomi tena au? maana hapo umetuambia kama unaishi Tanzania na mwanao hajapata zile chanzo za zamani jiandae, inamaana kama amepata basi hiyo mpya hapati? naomba ufafanuzi jamani

Anonymous said...

hongera sana dada Jian kwa kuletea watanzania mambo ya muhimu kama haya. (mimi ni yule mdau ambaye siku moja nililalamika kuhusu picha fulani) but kusema kweli sasahivi nafurahi sana jinsi unavyo jitahidi kuelimisha uma tena elimu ya bure, mimi binafsi sina mtoto wala mimba but napenda kusoma sana haya mambo muhimu unayo andika najua siku moja yatanisaidia nitakapo amua kuwa na mtoto. Mungu akubariki sana ili uendelee kutoa hii elimu ya bure