Showing posts with label Mother's Day. Show all posts
Showing posts with label Mother's Day. Show all posts

Monday, May 13

Mother's Day card by X -- My first ever!!!


 Kadi yangu ya kwanza, ever!!!, ya kunitakia Happy Mother's Day...from my son, Xchyler...so proud of him...and thanks to the teachers for making this happen! 

Kaila is a big-boi now...huu mwandiko wake mwenyewe!!

Happy Mother's Day--from Ohio



It's Mother's Day! Aika na Mama yake Cecy Njau wakipozi kwa picha katika kusherekea siku hiyo muhimu duniani huko Columbus, Ohio nchini Marekani...



Tuesday, May 15

Feza's Mother's Day celebration

 Wamama wa watoto wanaosoma  Feza Nursery School tulialikwa Jumamosi iliyopita kwenye sherehe ya Mother's Day ambayo waalimu walituandalia.
Tulikaribishwa na mkuu wa Feza Nursery School. Ms Bushra...

...wamama tulikua wengi wa kutosha... 

 KGI, kina Xchyler, ndo walianza kwa kutuimbia...very touching song about mama...

...hapa wanasema I love you... 




Hawa ni KG III...nalifanya kama poem about mama...hapa wanasema, whatever I give you, you give it back much much more...sikumbuki maneno yote, ila maana ni kama hiyo...pia ilikua bomba sana! 

Sunday, May 13

Happy Mother's Day wadau...


Esther na mwanae anitwa Newton Newton. Hawa ni wadau wa Morogoro.

Christina & Jill

 Happyness & Aaliyah

Fatma & Nasreen

Rebecca & Rachel


Rachel & Risper

Happy Mother's Day wadau wote..
Love, Jiang.

Wednesday, May 9

Sherehekea Mother's Day na Mama na Mwana

Wadau mnajua huu ni ukumbi wa ku-celebrate kitu cha kipekee duniani, nacho ni kuwa mama.
Siku ya Mother's Day imewadia; ni tarehe 13, May, Jumapili hiii.
Kuna event kibao zinaendelea, na kuna vitu kibao unavyofanya kila siku kwa mama yako, ila swali ni tarehe hii maalumu kwa ajili ya mama:
Kama mama unaisherekeaje? 
Kama mume unaisherehekeaje?
Kama binti, kama mtoto wa kiume unaisherehekaje? 

Nitumie picha na ujumbe kwenda kwa mama yako au watoto wako kusherehekea Mother's Day, kuapreaicte kuwa mama, kumshukuru mama yako kwa malezi bora aliyokupa, kumshurkuru mkeo kwa malezi anayowapa watoto wenu. 
Picha na ujumbe huo utarushwa hapa bloguni siku yenyewe.

Karibu tusherekehe Mother's Day pamoja siku hiyo.

Tuma hapa: mamanamwana@gmail.com

Monday, May 10

Salamu za Mother's Day

( Michelle na ma'mtu, Sophia)
"This is Baby Michelle Felicia and Her Mom Sophia wish all mothers (Women) happy MOTHERS DAY."
 (Adam na mama, Grace)
"Nawatakiwa kina mama wote siku njema na Mungu awazidishie mapenzi kwa wote."

 Placid na Mama yake Sophia


Mdau Laura na ma'mtu Llilian wanawatakia wakinamama wote ulimwenguni furaha  na maisha mema yenye amani na upendo.

Fahim na ma'mtu Shufaa...


Glory na ma'mtu Jackline...


*****
Kwa niaba ya wadau wooote, nasema Akhsanteni!

Sunday, May 9

Nani kama mama?

Happy Mother's Day kwa wadau wooote wa Mama na Mwana, nina imani kwamba mmepata muda wa kuwapa heshima mama zenu, kupitia sikukuu hii ambayo ilianzishwa maalum kwa ajili hiyo.
Tofauti na sikukuu nyingine, hii sio sikukuu ya wingi, ndio maana ni Mother's sio Mothers day, nia ikiwa ni kila familia kusherehekea sherehe hii kwa kumkumbuka na kumshukuru mama yao.
Hivyo basi nachukua nafasi hii kumshikuru na kumwambia mama yangu kwamba nampenda sana.
Mama, wewe ndio mwongozo wangu katika kila nnalofanya, na  nashukuru kwa kuwa na wewe kama mama yangu, Akhsante mama.

Sunday, May 10

Happy Mother's Day

Mtoto akiongea na Mungu akamuuliza, “Wananiambia karibu utanipeleka duniani, lakini ntaishije kule wakati mimi ni mdogo sana na sina uwezo wowote?”
Mungu akajibu, “Kuna malaika wako atakayekua anakusubiri atakusaidia kwa kila kitu.”
Mtoto akazidi kuuliza, “Ila hapa peponi sifanyi chochote, nakaa tu na nina furaha kila siku kwa sababu malaika wananiimbia, nikifika duniani itakuaje?
Mungu akasema, “Hata duniani huyo maialka wako atakuimbia na utaona mapenzi yake na utakua na furaha sana.”
Mtoto akauliza tena, “Nitaelewaje lugha ya huko duniani watu wakinisemesha?”
Mungu akasema, “Usiwe na wasiwasi, Malaika wako atakufundisha hiyo lugha taratibu utaelewa, na hata kabla hujaelewa lugha hiyo jua kuwa kila maneno atakayokuambia malaika wako yatakua ni maneno matamu tu.”
‘Na nikitaka kuongea na wewe nitafanyaje?” akauliza tena mtoto.
Malaka wako atakufundisha kusali, na hiyo ndio njia ya kuongea na mimi, kwani nitasikia yote utakayoyasema,” alijibu Mungu.
“Na nani atanilinda?”
“Malaika wako ni wa kipekee, kwani atakulinda kwa gharama yeyote hata kama itasababisha apoteze maisha yake ili wewe uwe salama,” alijibu Mungu , na mtoto akatulia kwa amani.

Ile anataka kuondoka kuja duniani, mtoto akakumbuka, “Ila Mungu, hujaniambia jina la huyo malaika,”
Mungu akamjibu, “Ukifika mwite mama, naye atajawa na furaha isiyo kifani,” halafu akamwachia aende duniani.

*****
Kama wewe ni mama wa umri wowote, wa mtoto yeyote, Happy Mother's Day, na jua kuwa wewe ni Malaika maalum na wa kipekee.

Asante Mama, you are the best.

Happy Mother's Day - Wadau Woote!

Jamani, Happy Mother's Day wadau wengine woote mnaonisapoti katika blog hii ya jamii ndogo, ambao sina picha zao wakiwa na watoto wao. Naomba niwataje wachache ninaowakumbuka ambao nina picha za watoto wao ila zao sina kama mama Glory Moshi, mama Dorice, mama Joshua, mama Dorries Nkone, mama Kelvin Pongo, mama Daniel, mama Henry Mgwabati, mama Lisa-Joann, mama Jamil Jamidu, mama Sophy Mahanga, mama Louis Lusajo, mama John, mama Glory Mroki, mama Atelovi Manni na wengine woote ambao labda nimesahau majina.
Pia nawatumia salamu za Mother's Day wakina mama wooote wanaonnisapoti anonymously kwa salamu, mails, comments na hata kutembelea blog hii kimya kimya.
Na pia, kina mama wooote.

You may never know how speacial a woman is until you become a mother, yaani hapo ndio utajua kwa nini Mungu alimuweka mwanamke wa mwisho kabisa kwenye uumbaji wake, na baada ya kumuumba mwanamke akaona hamna haja ya kuongeza.
Mothers, you are all special.

Happy Mother's Day- Wadau Woote!

Zena Chande ni mama wa Nasri Charunga.

regina Kumba ni mama wa Harieth.

Justades Angelo ni mama wa Suri.

Hery ni mama wa Nicole.

' Love you mom'. Mamma G akipokea busu la upendo toka kwa mwanae G.











Edda Mmasi ni mama wa Prince






Patricia Patrick akimlisha keki mama yake Nelly Mtema.






Gladys Fahari ni mama wa Mwita.










Happy Mother's Day - Wadau Woote!

Stella Nyemenohi ni mama wa Brian Kamugisha.

Prisca Mbeswa akiwa out beach na mwanae Jada Donald.

Janeth Mushi ni mama wa Thiery Mukanda.




Joyce Macha ni mama wa Dalvis Mlingi.


Happy Mother's Day Kwa Wadau Woote!

Jacquline Sadik, mama wa Jayson James.

Margareth ni mama wa Brian Msongo.

Aneth Bengesi akiwa na Binzu Masoud ambaye ana kaka yake anayeitwa Tariq.

Upendo Hartsuiker mama wa Aurelia Croft.