Saturday, March 28

Lishe ya Mtoto Baada ya Maziwa - Nyongeza

Hii ni toka kwa mdau Fatma Ally
Nafurahia sana kijiwe chako kwa siku naweza kukipitia hata mara tano na wala sichoki. Naomba na mimi leo nichangie kuhusu mlo wa watoto. Kwa ushauri wangu ukiwa mama unatakiwa uwe kama mwanafunzi, yaani kila siku unasoma na kujifunza kitu kuhusu mwanao. Kabla ya kutoa nijuavyo ningeshauri hivi kuhusu chakula cha mtoto.
1:Usichanganye aina nyingi za chakula kwenye mlo mmoja.kwasababu inaondoa ladha .
2:Weka ratiba ya chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku kuanzia aina ya mlo na muda gani mtoto apate kula na kiasi gani.Sio unazoea uji wa karanga kila siku.Na unampa mtoto chakula kingi mpaka akitapike ndio unajua kashiba weka kipimo maalum.
3:Jifunze kujua kila aina ya chakula na ubora wake mfano vitamini a inapatikana kwenye kitu gani na kitu gani ili kuepuka kumpa mtoto aina moja ya chakula.Na kinafaida gani mwilini . Ikiwezekana mpe chakula ambacho unaona kina kiasi kikubwa cha madini au vitamini uitakayo.
Baada ya kufuata kanuni hizo na zingine unazozijua, naomba niwaeleze kinamama kuwa tusifikiri juice hutokana na matunda tu tuelewe kuwa mbogamboga za majani pia zinatengenezwa juice mfano mchicha,kabeji, karoti,na hoho badala ya kuchemsha na kutengeneza supu tengeneza juice. Tusidharau vitu kama maboga ni kitu muhimu sana katika lishe ya mtoto , na nimejifunza kuwa ukipika viazi mviringo unatakiwa uche mshe na maganda ndio uvimenye hiyo ndio sheria ya afya.
Ombi: Mama X naomba utuletee habari kuhusu watoto wanaozaliwa na magonjwa ya kurithi mfano circle cell (unirekebishe kama nimekosea) na namna ya kuwahudumia.Na hata namna ya kuepuka kama utaweza. Shukrani mdau.
*******
Thanx for the support mamie Fatma, Usiwe na shaka, ntatafuta articles za magonjwa mbalimbali ya watoto niwaandikie, ila it is better kama mtu anataka ugonjwa flani anitumie request yake ili niutafutie taarifa, maana sitaweza kutafuta kila ugonjwa.
Love, Jiang.

No comments: