Thursday, March 26

Lishe ya Mtoto Baada ya Maziwa-Uji, What Next?

Baada ya Uji, What Next?
Mtoto hawezi kushindia uji tu, hapa ndipo juisi za matunda mbali mbali zinaingia, nashauri zisiwe za madukani, ingawa huwa zinaandikwa 100% natural fruit, you never know. Matunda yamejaa kibao gengeni, so ni cheaper na healthier kusaga mwenyewe matunda unayotaka ukamtengenezea mwanao juice nzuuriii.
Pia ukiangalia huo mchangayiko wa uji hamna mboga ya kijani, so ni vizuri kumtengenezea kasupu kadogo ka mchicha au majani ya maboga, au majani ya kunde au spinach, mboga yeyote akanywa pia kidogo. Epuka kumpa mtoto vinywaji ambavyo havina virutubishi kwa mfano chai, kahawa, soda na vinywaji vya rangi na sukari (juisi bandia).
Sasa mwanao ameshaanza kula vyakula vya ukweli, maji ni muhimu.

Uji, Juisi, Supu, Then…?
Sasa baada ya hayo yoote ndio yanakuja mambo ya mtori, au ndizi ziliziponda au viazi vilivyopondwa, ambavyo utachanganya na vitu vingine.
Utayarishaji na uhifadhi salama wa chakula cha mtoto:
Tayarisha chakula katika mazingira safi na kifunikwe ili kuzuia wadudu na uchafu. Mtoto anapaswa kuwa na chombo chake cha kulia chakula. Ni muhimu kumlisha mtoto chakula mara baada ya kutayarishwa. Mtoto asipewe mabaki katika mlo unaofuata.
Hapa ndio umuhimu wa kuwa na msichana msafi na anayemjali mtoto unapokuja, la sivyo utashinda hospitali na infections zisizo na jina kula siku kumbe tatizo ni katika kutayarisha chakula cha mtoto.

Xchyler’s Experience
X alikua hapendi kabisa uji, ila kila kitu kingine alikua anakunywa bila tatizo, juice na supu zote alikua ok nazo. tulimpampa uji hadi akauzoea, sas hivi hakatai kitu, anafurahia tu akiona bakuli linakuja. Halafu ni vizuri kumpa akiwa na njaa as ndio atakua na hamu, sio ameshashiba maziwa yake nyie ndio mnampa mauji yenu, ni rahisi kukataa.
X alianza kwa kuchemshiwa viazi mviringo au ndizi bukoba pamoja na supu ya nyama, na carot kidogo, na njegere/mchicha au mboga yeyete ya majani kama vijani viwili.
Vikiiva vilikua vinatiwa kwenye blender na kusagwa unakua uji mzito ndio analishwa kama kawaida. Sasa hivi kakua anapondewa na kijiko ndio analishwa, ili visiwe vilaini sana, hata meno ya kutafunia anayo.

5 comments:

Anonymous said...

Jamani kina mama, pia kwenye akula cha mtoto waweza kumuwekea ipande cha parachichi na kitunguu swaumu na kitunguu maji,hii inasaidi kumlinda na vijigonjwa vidogovidogo. Mie wangu tokea ameanza kula chakula nilikuwa na muwekea vitunguu swaumu na kitunguu maji pia, ila kitunguu swaumu kama ni kikubwa weka kipunje kimoja tuu kinamtosha si mnajua harufu yake tena. Karoti kwa wingi saaana mtoto anatakiwa ale.

Anonymous said...

Wadau, eti watoto wetu hawa kwenye vyakula vyao, tukiwachanganyia na nyanya kidogo je?? mfano viazi au ndizi baada ya kuweka vitunguu,carrots,njegere, na vinginevyo je waweza kumuwekea na nyanya?? maana kama juisi ya nyanya wanakunywa sidhani kama itakuwa mbaya kumix kwenye msosi wao! au mwasemaje wenzangu??

Anonymous said...

Wadau nyama hasa nyekundu sio nzuri kwa watoto lakini nyama nyeupe kama samaki na kuku ni nzuri kwa watoto pia mboga kama nyegere carrots pasnips brocholi na cauliflower sijui hizi tatu za mwisho zinaitwaje kwa kiswahili ni nzuri kwa mtoto chakula cha mtoto kinaweza kuchanganywa na nyanya hapo baadae baada ya miezi tisa lakini habari ya vutunguu siijui.lingine la muhimu ni kuepeuka kuweka mafuta ana siagi ya aina yoyote kwenye chakula cha mtoto tofauti na ndizi za bukoba na viazi unaweza kutengeneza chakula cha mtoto kwa kutumia maboga ama viazi vitamu na ukaweka vegetables kama carrots na mchicha ama njegere na ukausaga mchanganyiko huo ukawa chakula tofauti na vegetables unaweza ukatumia fruits kama apples parachichi na ndizi za kuiva pia ukachanganya kwenye chakula cha mtoto kinchokaripia kupoa ila kumbuka kumenya na kupondaponda sana ili hayo matunda yawe malaini na yafae kuliwa na mtoto kwa wale watakaoamua kutumia apples yabidi limenywe maganda litolewe mbegu na lichemshekwa dakika tatu ili liwe rahisi kublend

Anonymous said...

naomba kuuliza vyakula vya makopo vina athari?niko uk niko bizy kama mnavojua wasaidizi huku hakuna namnunulia mtoto chakula cha makopo foer his age though..je ni mbaya naomba msaada wenu..

Anonymous said...

mdau wa hapo unaesema uko busy na uko uk bila msaidizi mimi pia niko uk sina msaidizi na sijawahi kumlisha mwanangu vyakula vya makopo kutokana na athari zake vingi huwa vimewekwa madawa makali kwa ajili ya kupreserve ingawa wenyewe watengenezaji hawasemi na madhara yake ni magonjwa ya kutisha kama cancer ninachokushauri usiwe busy kwa mwanao tafuta baby menus na upikee chakula cha mtoto mimi hujaribu kupika at least na kuweka kwenye freezer kama chakula cha wiki na baadae huwa natoa na kumpa hii kuliko makopo ambayo hujui yametengenezwa lini maana yana expiry date tuu je manafacture date unazitambuaje kuwa makini mwanao.