KWA AJILI YA MAMABrazia za kunyonyeshea: hiki ni moja ya kitu nilichopenda kupita kiasi, sijui nani alilivumbua hili wazo, lazima alikua mwanamke. Zimejaa kibao kwenye maduka ya watoto, (elfu kumi hadi 15)ila unapochagua size kuwa mwangalifu usijesahau ukachagua size yako ya kawaida wakati maziwa yamekua.
Pedi za maziwa: hizi zinasaidia kunyonya maziwa yanayotoka wakati mtoto hanyonyi, hasa kwa wenye maziwa mengi, hizi ni must have!

Khanga: nilipoolewa nilipewa zawadi ya khanga nyiiingi, nikiwa si mvaaji khanga, nikazishangaa, nikagawa baadhi na zingine ngine zikabaki kabatini bila kuguswa wala kukatwa. Hadi hapo alipozaliwa Xchyler ndipo nilipojua kwamba vazi hili la mwambao, ni zaidi ya mavazi yote yaliyopatwa kubiniwa, we nunua angalau doti tatu, believe me, utazitumia tu!
MengineyoTaa ya kuchaji: umeme wa ndugu zetu wa Tanesco si mnaujua, sasa afadhali uwe na rechagable light mapema, ili usiku wakichukua umeme wao, usipate tabu ya kutafuta kibetiti kwenye giza totoro wakati kichanga kinalia.
Vikatia kucha/Nail clippers: watu wengi wanatumia nyembe za kawaida, ila mimi wembe siwezi kutumia naona kama ntakosea nimkate mtoto, so ikabidi ninunue nail cutter/clipper za watoto, hizi ni laini flan hivi kuliko za watu wazima.
Sabuni za kufulia: kama unaweza nunua paketi moja, kama ya 500g kila mwezi, ile miezi mitatu ya mwisho, ili mtoto akija
Madumu ya maji: bongoland kila kitu kwa mgao, kama unakaa sehemu kama Tabata nunua tu madumu ya ziada ya kuwekea maji, ili kufua nepi isiwe shida.
BABA
Maua: Ni muhimu kujua kabisa maua ya zawadi kwa mama mtoto utayanunulia wapi.
Kamera: wadau wa mama na mwana tutakua tunasubiri wa hamu picha za mwanzo za mdau mpya, baba tayarisha kamera kabisa, au azima mapema.

2 comments:
Asante sana Jiang mimi pia ni mama mtarajiwa ndio niko miezi ya katikati nilikuwa nasema bado mapema sana kuanza kufanya shopping. na nilikuwa sijui hata cha kununua ni nini itabidi nianze kidogkidogo kumbe vitu vinavotakiwa ni vingi. Asante kwa kuniamsha
Hi Jiang mbona kimya?
Mzima ww? mdau alokumiss
Post a Comment