Monday, May 25

Jina La Xchyler

Watu wengi wamekua wakiniuliza matamshi, maana, asili na nilifikiria nini hadi nikampa mwanangu jina la Xchyler.
Ili kuondoa maswali mengi na kuwaridhisha wadau, nimeona tu subiri nijibu yooote kwa pamoja.
Kuna njia nyingi za kupata majina ya watoto, ila hilo ntaliongelea siku nyingine, kwa Xchyler, kabla sijapata ujauzito, nilifikiria nikija kupata mtoto ntamwita lenye maana ya Malaika, ila kwa lugha isiyozoeleka kabisa, ili liwe la kipekee. Na focus yangu kubwa ilikua ni kupata jina la kipekee (unique), as mimi nina jina la kipekee, kwa hapa bongo (China jina langu ni kama Amina Neema au Asha, maana kila mtu analo) hivyo najua faida na hasara za kuwa na jina la kipekee.
Basi, baada ya kuwa mjamzito nikatafuta sana malaika kwa lugha tofauti tofauti, ila zote sikuzipenda, baba yake akasema, tutafute tu unique names, zenye maana yeyote nzuri. Akatafuta, na mimi nikatafuta, tukapata jumla ya majina kama 20 tuliyoyapenda, 14 ya kike, 6 ya kiume, na Xchyler ndio lilikua pekee linaloweza kutumika kote.
Kwa mtoto wa kike mimi nilipenda jina flan hivi, Qiana, la wamarekani wale wa asili (Red Indians), ila lilimtatiza sana baba yake akidai kuwa wabongo kama kawaida yao kupenda urahisi watakua wanamkatisha Ana, na yeye hataki jina common kwa mwanae.
Yeye tangu mwanzo moyo wake wote kwenye Xchyler, tena akawa anaona urahisi maana hata akiwa wa kike au wa kiume hatutabadilisha, ila mimi niliona ni refu sana, ukizingatia jina kamili ni Xchyler Mapunda, ila baba yake akasema mbona na yeye ni refu, Sixtus Mapunda.
Alijitahidi kunishawishi, hadi baadae nikaona ni zuri, na kiukweli nalipenda sana, I cant imagine mwanangu huyu aitwe jina lingine, naona kama linamfit sana.
Asili: Hili jina linatoka kwa wa-Dutch, nchi inayoitwa Holand/Netherlands (hii nchi timu yake inavaaga jezi za orange, niliizimia tangu nasoma Jangwani).
Maana: Msomi, mwanazuoni (scholar/Intelectual)
Matamshi: Xchyler linatamkwa kama unavyoisoma skyler, na kuna watu wanaliandika hivyo.
Kukatisha: Mimi napenda kuliandika X, na watu wengi wanaliandika hivyo ili wasikosee, ila kumwita napenda kumwita 'kailer' ,na mwenyewe anaelewa. Watu wengi, waliokua siku nyingi wanatafuta sababu ili wasitamke jina langu, maana nalo mtihani, wananiita Mama X, na napenda kuitwa hivyo pia.
Spelling zingine: Skyler, Schyler, Schylar, Skylor, Skyller, Skuyler, Schuyler
*****
Nadhani hadi hapo hakutakua na maswali tena kuhusu jina la Xchyler.
Najua kila jina lina story nyuma yake, niandikie kuhusu jina la mwanao, ambatanisha na picha ya mtoto, tu-share na wadau, maana wengine bado wanatafuta majina.

3 comments:

Anonymous said...

Hi mama X,Mimi bwana naipenda sana blog yako naweza nisitoe comments but just looking at the angels{maana watoto ni malaika} nafarijika
Mungu akupe kila la kheri ,maana hii si kazi ndogo

Mwanao he is always HAPPY & SMILING. That's a good sign kwamba he is free from matatizo,maana mtoto asie tabasamu au hata kucheka ana matatizo flani

Mshukuru Mungu kwa hilo

Anonymous said...

ahsante sana mama X mana niliandika comments weeee hukutoa, nilikua nazungumzia majina unique mana kweli unaweza msababishia mtoto ataniwe na awe na low self esteem badae, ila maelezo yako yamenikuna kweli.

kweli jina ni zuri, matamshi yana sound vizuri, and as a mother i know how you feel, mana tena mtoto wa kwanza, yani mtu unachambua majina mpaka unakoma, kila ulalotajiwa unaliona halitamfaa ila maana mi ndo hua naona ni nzuri, mana sasa nimeelewa kwanini umemuita xchyler, kaila just sounds cutee. so all the best, am waiting to comment more. Mungu ampe X mazuri yote ya jina lake, awe msomi, intellectual na kama malaika

Anonymous said...

yaa mama X, so what the meaning of that dutch name?