Saturday, September 19

Collins Akifanya Sarakasi

Mdau mgeni, Collins Johnson (6yrs) akiwa anapiga sarakasi, ma'mtu, Judith Rwakyendela, analalamika kwa utundu wa kupandia vitu, kibinuka binuka na kukimbia kitu ambacho anafanya kila baaada ya sekunde moja, majeraha hayaishi, shuleni, kwenye play ground, yani ni kama haoni danger...
mmmh, hapa kama namuona Xchyler miaka michache ijayo, maana nae kwa kupandia na utundu uliopitiliza usiseme.
Nnachoweza mwambia mama Collins ni kwamba, usiogope, ndio utoto huo, akikua ataacha, atakuwa mpole hadi utashangaa.
Halafu, mama Collins ameniambia kitu kingine kinachomfanya Collins azidi kufanana na X, Collins anasema wana nyumba mbili, "kwa mama sinza na kwa bibi salasala", kama X, kwa mama K'nyama na kwa bibi Chang'ombe.

No comments: