Saturday, November 7

Shemsa ndani ya joho la mama!

Mdau Shemsa Kachwamba(2yrs) akiwa ndani ya kofia na scarf ya graduation ya mama'ke, Jamillah Kilahama kama mama anavyohadithia:
"Basi hapo ilikuwa nimetokea kwenye graduation yangu nikaacha gauni la graduation sebuleni kurudi nikakuta kavaa ile kofia na kile kitambaa kingine kinachovaliwa juu ya joho na alipomaliza kuvaa akanifuata eti mama nimependeza nipige picha!.. kwa kweli nilifurahi sana nikajua kumbe na yeye ana goals za kufika university... kingine anapenda sana kunyonya vidole hadi sasa vidole vyake vimeota sugu kupita maelezo!"
Hizo ndo habari za mdau wa blog hii Shemsa bint Abubakar Kachwamba, ukimuona mpoleeee, kumbe akiwa kwao...

No comments: