Wednesday, March 17

Adhabu hizi zinafundisha au udhalilishaji?

Wengi tiliosoma Saint Government aka St. Mchangani tushashika masikio kwa style hii sana tu!
Ukiona kama mchezo, ila unaumia, acha tu, miguu inakosa nguvu kabisa, afu kama una ugonjwa wa kutoka damu puani, au kusikia  kizunguzungu inakua balaa!
Afu kuna ya kuita juu, mkiwa wengi mtu anaweza kudhani mnafanya choreography, maana inapendeza, kumbe mnateseka, ila fimbo ndio kiboko ya wote!
Ingawa siku hizi watoto wengi wanasoma St Private aka English Academy, no fimbo, no adhabu kali, je adhabu hizi zilikua zinasaidia?

3 comments:

Anonymous said...

Inawezekana inafundisha lakini sijui kama haina madhara kiafya.

disminder.

Anonymous said...

ina madhara makubwa/tena hao wanaofanya hivyo wachukuliwe hatua hebu wao wapewe hii adhabu kama wataweza,kwani mi naona mtoto akikosa sema naye ,au mpe kazi za masomo zaidi azifanye hadi

Anonymous said...

Hizi adhabu hazisaidii chochote waliopanga kuharibika wameharibika japokua walipigwa mpaka, imewafanya wawe sugu na makatili. Haya maadhabu ni kunyanyasa watoto tuu, tuliokulia kwenye mambo haya tumekua ni waoga, hatujiamini na yote hayo ni madhara ya haya maadhabu.