Mtoto huyu sikupata jina lake, ni wale watoto wanaoweka vibao vya kuonyesha magoli pale uwanja wa zamani wa taifa (shamba la bibi), sasa kule ni juu sana, so huwa wanapanda na ngazi, naambiwa juzi kati huyu akaanguka wakati anaweka vibao, watu walimdaka fulani, lakini alifika chini.
Aliwahiwa na watu wa huduma ya kwanza, kama inavyoonekana hapa nesi akimhudumia, na ilionekana hakuumia sana.
SWALI:
- Kwa nini hadi leo hicho kibao bado ni cha mwaka 47, kinawekwa kwa mkono, yani hakijawa digitalised?
- Lakini swali kubwa zaidi, kama bado tunajikongoja kwenye teknolojia ya kuwa digital, kwa nini wasipande watu wazima kidogo, vijana, badala ya watoto wadogo kama hawa ambao wanahatarisha maisha yao???
- ILO vipi, hii si kazi hatari???
(Picha hisani ya Anko Evans Ng'ingo)
3 comments:
Nchi hii
Wakati mwingine watoto nao ving'ang'anizi! Hasa watoto wa uswahilini kwetu,wanajifanya wakubwa kung'ang'ania kazi zilizo nje ya umri wao kisa apate hela ya kwenda kuangalia Video!! Na umasikini nao pia unachangia huenda anatafuta japo mia tano apeleke nyumbani wakanunue tembele!huwezi kukuta mtoto toka Masaki au osterbay au Upanga anang'ang'ania kupanda kuweka hivyo vibao!
hi aunty,
asante kunipa nafasi ya kujimwaga,,, mimi siwezi laumu watoto wetu. Kama tungekua tuna wa provide with their essentials na kuwa keep safe at home si dhani km ajali hii ingetokea. Na kama hatuna uwezo tuwaelimishe watoto wetu wata appreciate....
pole kwako mtoto na familia yako... enyi kina mama tuwajali wanetu na hata kama tunakula vumbi, tuwaelimishe wanetu kwa nini....
Nasi kina dada/kina mama tujitahidi kujiendeleza....
Thanx Jiang,
mama D
Post a Comment