Mara nyingi kadri inavyowezekana. Kumbuka unavyozidi kumnyonyesha mtoto ndivyo mwili wako nao unavyozidi kuyatengeneza.
Jitahidi unyonyesha kilamtoto anapohitaji kuyonya na akionyesha dalili za njaa, kama kuhangaika hangaika, mara anapoamka baada ya kulala, kujitafunatafuna…na zingine utakazozijua kutokana na kumzoea mwanao. Kwa ufupi usisubiri alie ndio umnyonyshe kwani kilio ni dalili ya mwisho kabisa njaa.
Watoto wengine wanapenda sana kulala na wanajisahau, kwa hiyo kama mwanao analala sana mwamshe ili anyone. Inashauriwa mtoto mchanga asikae au asilale zaid ya masaa manne bila kunyonya. Anavyozidi kukua ndivyo atakavyopunguza kunyonya usiku, na atakua anajua kudai nyonyo kwa ishara mbalimbali yeye mwenyewe!
1 comment:
MAMA X, KWANZA HONGERA KWA KAZI NZURI MANA SIKU HIZI BLOG KILA KONA MPAKA WATU HAWAJUI CHAKUWEKA MWENYE BLOG ZAO, WANAANZA VIZURI ALAFU NJIANI WANACHEMSHA
ILA HONGERA KWA KUENDELEA KUTUPA VITU. TATIZO JAMANI BLOG YAKO IKO SOO BORING IN TERMS OF COLOURS AND GRAPHICS, YANI HII NI BLOG YA MAMBO YA WATOTO, JARIBU KUWEKA BACKGROUND YENYE MVUTO BASI JAMANI BIBIE. YANI IKO TOOOOOOO PLAIN FOR A MOTHER AND CHILD BLOG. PLEASE NI USHAURI TU
Post a Comment