Watoto huathirika vibaya na madawa kuliko watu wazima, kwa hiyo kuumpa mtoto madawa ya hospitali au hata madawa ya asili inaweza kuleta matatizo. Yafuatayo ni madawa usijaribu kumpa mtoto wa umri kati ya miaka miwili (2) hadi mine(4).
Bofya hapo kushoto na mie hapa uzione....
Aspirin
Usithubutu kumpa mtoto wako aspirin au dawa yenye aspirin ndani yake. Aspirin inamfanya mtoto kuwa katika hatari ya ugonjwa wa REYES. Ni mara chache lakini ni gonjwa hatari na kupelekea kifo. Usifikiri kwamba madawa yanayopatikana katika duka la dawa hamna aspirin. Aspirin mara ingine huitwa kwa neno la kitaalamu ‘salicylate’ au ‘acetysalicylic acid’. Kuwa makini sana katika kusoma lebo za madawa na muulize daktari au muuza madawa kama huna uhakika dawa uliyopewa ina aspirin au la.
Kwa homa na maumivu , kama ukitaka kumpa dawa mwanao , ni bora kumpa dozi ya dawa za kupunguza maumivu kama panadol.
Dawa baridi (over the counter) za kikohozi na mafua
Wataalamu wanashauri kutotumia dawa baridi (over the counter) kutibu magonjwa ya kikohozi na mafua kwa watoto wadogo. Tafiti zinaonesha kwamba hazisaidii kupunguza dalili za ugonjwa kwa watoto wenye umri mdogo. Na huweza kuwa sumu, hasa pale ambapo hutumika zaidi ya dose iliyowekwa(over dose) .
Dawa hizi zina madhara kama kutopata usingizi, muungurumo katika tumbo, vipele, mtoto anaweza kupata madhara zaidi kama moyo kuongezeka mapigo na hata kifo.
Kama mtoto wako anasumbuliwa na baridi, jaribu dawa za nyumbani kama tangawizi, kufukizia, asali, juices za matunda nk.
Madawa ya kuzuia kichefuchefu
Usimpe mwanao dawa za kuzuia kichefuchefu labda kama daktari amesema apewe. Mara nyingi husababisha kutapika, na watoto huwa wanavumilia kichefuchefu hadi kinaisha chenyewe bila dawa. Pia dawa za kuzuia kichefuchefu zina hatari na madhara makubwa.
Madawa ya watu wazima
Kumpatia mtoto madawa ya watu wa wazima hata kama ni dozi ndogo yake ni hatari kwa watoto wadogo. Kama dawa inaonesha kuwa si nzuri kwa watoto usimpe mtoto dawa hiyo.
Dawa yoyote aliyoandikiwa mtu mwingine, au ugonjwa mwingine
Dawa zilizoandikiwa kwa ajili watu wengine au kutibu ugonjwa mwingine haitakiwi na ni hatari ikipewa kwa mtoto wako. Mpatie mwanao dawa ambayo imepewa kwa ajili yake na kutokona na ugonjwa alionao.
Chochote kilicho-expire
Tupilia mbali madawa mara tu yanapokwisha muda wake wa matumizi. Pia yaache madawa machafu au yaliyoganda hasa endapo yatakuwa yamepoteza muonekano wake wa awali pindi uliponunua. Dawa yeyote ile ikiisha muda huwa sumu. Pia, sometimes utunzaji wetu unapelekea dawa kuharibika kabla ya muda uliowekwa kwenye lebo. Chunguza rangi na harufu za dawa kugundua kama zishaaribika hata kama muda walioweka kiwandani haujafika (mimi huwa natupa dawa zote za maji zilizofunguliwa baada ya mtoto kupona muda huo). Usitupe dawa chooni kwani huweza kupelekea madhara katika mlolongo wa maji na baadae hudhuru mgawanyo maji ya kunywa.
Dawa za kupunguza maumivu zenye nguvu zaidi
Si tunasiakiaga matngazo yake, sijui nini nini extra power. Hizo kama zinakuponyesha wewe usimpe mtoto.
Madawa ya kienyeji
Madawa mengi ya asili ni mazuri na salama, lakini ni kwa sababu tu ni kitu ambacho ni asili, kilichotolewa katika mmea, haimaanishi ni salama kwa mtoto wako. Kama dawa za kizungu dawa za asili pia zinaweza kusababisha madhara kama ya aleji, huaribu ini na shinikizo la damu. Dozi zingine au kuchanganywa na madawa ya kizungu zinaweza kusababisha kifo. Just make sure unazijua vizuri hizo dawa za kienyeji au aliyekupa anazijua na unafuata maelekezo vizuri usije ukamzidishia.
Tahadhari: Dawa za kutafuna
Madawa ya kutafuna hayako asilimia mia salama isipokuwa unatakiwa kuwa makini wakati wa kumpatia na kivipi mwanao.
Watoto wengi wa umri wa miaka miwili(2) hadi minne (4) huweza kutafuna vidonge, hasa zile zinazoyeyuka mapema. Lakini kuwa mwangalifu sana kwa mtoto wakati unampa dawa za kutafuna, pia hasa kabla hajaanza kutafuna vitu vigumu.
Kama unafikiri kuwa madawa ya kutafuna ni hatari kwa mwanao, vunja vunja kisha weka katika kijiko cha chakula. Na pia hakikisha mwanao anaingiza kijiko chote mdomoni ili kuhakikisha anakunywa dozi yote.
1 comment:
Pole na majukumu mama X! Aisee asante sana kwa kutujuza. Ubarikiwe sana.
Mama E.
Post a Comment