Kumekuwa na matukio mengi ambayo
tumekuwa tukikutana nayo yanayowakabili watoto. Watoto wengine tunakuwa
tunawafahamu na wengine hatuwafahamu.
Watoto wamekuwa wakijeruhiwa,
wakifanyishwa kazi ngumu katika umri mdogo na pia hata kufanyishwa biashara ya
ukahaba.
Pia hata ukifatilia swala la takwimu
idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu (watoto wa mtaani) imekuwa
ikiongezeka kadri siku zinavyokwenda. Lakini inawezekana wote hatujui sababu ya
mambo hayo. Katika kuperuzi peruzi mtandaoni nilikutana na kitu kinachoitwa
Azimio la Haki za watoto baada ya kusoma na kumaliza niliamini kuwa endapo
maazimio hayo 10 yote yatatekelezwa Ulimwengu utakuwa Better place for Children to
live.
2.
Wana haki ya kukua na kukuzwa kimwili na
kiroho wakiwa katika afya njema, kuwa huru na mwenye utu.
3.
Wana haki ya kupatiwa majina na kuwa
mwanachama wa nchi.
4. Wana haki ya kupatiwa malezi maalum na ulinzi,
malazi na huduma za afya.
6.
Watoto wana haki ya kupendwa na
kueleweshwa na jamii nzima ikiwepo wazazi na wanafamilia, pia serikali inaweza
kuingilia kati pale inapoona hawajapatiwa na wanazistahili.
7.
Wanahaki ya kwenda shule na kupatiwa
elimu, kucheza na kuwa na nafasi sawa ya kujifunza na kujiendeleza. Mzazi
una majukumu kuhakikisha mtoto anapata elimu na
mwongozo wa yale anayoyahitaji.
8.
Wana
haki ya kuwa wa kwanza kupatiwa msaada pale tu wanapohitaji.
9.
Wana haki ya kulindwa dhidi ya ukatili
na unyonyaji.
| |
Unadhani nini kifanyike ili haya maazimio yaweze kutekelezeka? |
No comments:
Post a Comment