Hivi jamani?
Hakuna adhabu mdabala wa kiboko?
Mtoto akifanya kosa kitu cha kwanza kutafutwa huwa ni fimbo ili aadhibiwe.
Hii imekuwa adhabu kubwa na wengi wetu tumekutana nayo katika makuzi yetu ikiwemo nyumbani na shuleni. Lakini je kule kuchapwa kulikusaidia katika kubadilisha tabia zilizokuwa zinakukabili?
Kwa mtazamo wangu:
1. Kiboko ni kitu kizuri ambacho kikitumiwa ipasavyo na kwa utaratibu humbadilisha mtoto kabisa.
2.Watoto wengi huogopa viboko hivyo kuwafanya wawe makini katika mienendo yao ya kila siku.
3. Mtoto asinyimwe kiboko ila apatiwe pale tu kinapomstahili.
Nini kifanyike wakati wa kumwadhibu mtoto kwa kiboko?
wazazi wengi wamekuwa na haraka ya kumwadhibu mtoto biila kumpa nafasi ya kujitetea, na wengi huchanganya na hasira na kutokea mkuwaadhibu vibaya. hapa ndipo husikia zile kesi za kupigwa na waya na kuchomwa moto mikono.
- Ni muhimu kabla mtoto hajachapwa apewe nafasi ya kujitetea. Ingawa wengine husema uongo ili apone lakini ni vizuri kupewa hiyo nafasi kwani humjengea mtoto hata uwezo wa ku argue.
- Kisha ni muhimu aambiwe kosa lake kwa utaratibu na kwa nini anaadhibiwa. Pia aambiwe madhara ya kufanya hilo kosa na kuonywa kuwa asirudie tena kulifanya.
- Mtoto asipigwe sehemu nyingine yoyote zaidi ya matakoni pia asipigwe ovyo ovyo viboko visivyo na idadi.
Hebu tujadili kama unakubaliana na kiboko au lah.
1 comment:
Mie kiboko natumia sana, yaani kadri kinavyohitajika...makosa makubwa ni kiboko tu!!!
Ila kubalance ni muhimu, maana mtoto anaweza akawa sugu bure, so sometymes natumia mkwara; huendi bichi, au karipio, au timeout, (kuna kikona ig Brother hakipendi huyo) namuweka hapo 3-5 min.
At the end of the day inategemea mzazi na mtoto, watoto wengine sio watundu na wasikivu so hamna sababu za kuwachapa, au mzazi mwingine hapendi kuchapa, yeye mwenyewe hajakuzwa kwa kuchapwa na anajiona yuko ok, so haoni sababu ya kuchapa mtoto...mi nimechapwa na nachapa na naona inasaidia kunyoosha hawa malaika wetu.
Post a Comment