Friday, February 22

Msaada--Mtoto ana mwaka na miezi minne, ila bado haongei

Nina mtoto wa kiume anaelekea mwaka 1 na miezi 4 sasa. tatizo ni kwamba hadi sasa hajaweza kutamka hata baba wala mama. mara moja moja utamsikia akitamka "kaka" au "dada"lakini baada ya muda husahau na inachukua muda mrefu tena anaanza kuyatamka tena. Mara moja moja hutamka km neno baba lakini kwa kuingiza mdomo wa chini ndani km anaung'ata hivi. Nilishawahi kumpeleka hospital wakaniambia bado ni mapema mno kusema km ni tatizo hilo, lakini mimi linanikosesha amani sana. Je tatizo litakuwa ni nn?
--Mdau. 

Kwa umama wangu wa watoto wawili, kwa kweli sidhani kama mwanao ana tatizo...maana kama ameshanyanyua ulimi, na hosptali wamesema ni mapema, basi ni mapema...watoto wanatofautiana katika ukuaji, wengine hawaongei hadi wakifika miaka miwili hadi mitatu saa nyingine!! 
Mi naona wako ni mdogo mno kuanza ku-worry kuhusu kuongea. Just make sure kuwa anasikia; ita uone kama atageuka, wahs TV au redio yeye akiwa opposite direction uone kama atageuka...angekua hasikii nadhani mngekua mmeshajua.

Pia mwache achanganyike na watoto wenzake, ukute mnamfungia sana ndani, na wenzake atakua independent na atajua value ya ku-communicate kutumia maneno, as watoto wenzake hawatamuelewa kwa vitendo kama hapo ndani, na atajisikia raha kuongeaongea na wenzake!

Nakushauri endelea tu kumfatilia kwa karibu maana kama ana tatizo utajua tu.
Ila botom line naona kama mwanao bado mdogo kuona kuwa ana tatizola kuongea.
Wadau wengine mnaweza kutusaidia uzoefu wenu.
--Love, Jiang.

8 comments:

Anonymous said...

Hi. Naungana mkono na wewe mtoto bado mdogo, ataongea tuu maana kama hata anaweza kutamka hayo machache jaribu kumuweka na wenzie akisikia wanavyoongea ataongea tuu na yeye.

Anonymous said...

Mdogo sana huyo wala usijali. Nina mdogo wangu mtoto wake alianza kuongea miaka mitatu tena baada ya kupelekwa day care. Ni mzima kabisa hana tatizo na ondoa wasiwasi.

mama wawil said...

naungana na jiang mtoto huyo bado mdogo na kitu kingine siku hizi wamama wengi watoto wao huwafungia ndani tu bila hata kupata kuongea ma wenzake. na anabaki na dada ambaye yupo busy na kazi hebu jaribu kumchanganya na wenzie huo uzungu tuuache

Anonymous said...

Dada mwenye mtoto wala usijipe presha hata katika tafiti za Ulaya wanasema mtoto wa kiume huwa anachelewa kuongea kwa asilimia kubwa kulinganisha na wa kike.....kwa hiyo vuta subira shost huyo bado mgogo sana for you to be worried.

Mie mwanangu wa kike aliota meno anakaribia mwaka wakati wa umri wake walikuwa na meno 6 mdomoni lols,nilipataje presha ahahahaha so sometimes kila mtoto anaukuaji wake.

Anonymous said...

bado mdogo wala usiwe na shaka mama yangu mie alisema mie niliongea mapema kabla ya kaka yangu ambaye alikuwa na miaka 3 alikuwa bado hajui kuongea ila pia wanasema mtoto wa kiume wanachelewa kuongea na pia inategemea mtu anae kaa nae nyumbani kama huwa anamuongelesha mara kwa mara,mie nina mtoto alikuwa bado hajatimiza hata mwaka na nusu ila nilikuwa namuongelesha sana aliongea mapema kushinda hata wale walio mzidi umri kuongea kwa mtoto haraka kunachangia pia na mtu anae kaa nae na hata hivyo mtoto wako bado ni mdogo ataongea tu usijali muongelesheni kila muda na yeye atakuwa anaiga maneno.

Anonymous said...

huyo bado mdogo sana , mie mwanangu wa kike alianza kuongea na mwaka na nusu, yani hapo ndo alianza kusema mama, so usiogope kwa hilo , mwache ajichanganye na wenzake ataongea tu.

Anonymous said...

mtoto bado mdogo ataongea tu. Nami nilipata hilo tatizo kwa mtoto wa kiume, nikampeleka hosp. docta alimchunguza kwa kumuita akageuka akasema atasema tu muda bado. Ila alitushauri tupendelee kumuongelesha mara kwa mara tusimtegemee mdada msaidizi. Kweli mtoto alianza kuongea mpaka akawa anababaika kama kigugumizi lakini sasa anaongea vizuri tu. Usiwe na wasiwasi muhimu endelea kumchunguza mtoto

Anonymous said...

mi naona bado mdogo huyo mtoto. ataongea tu, mi wa kwangu ana mwaka na miezi mitatu karibu minne. lakini anaita mama baba hajaweza kuongea zaid, lakini wala cina wasiwasi najua ataongea tu. so mama usiogope bado mapema sana.