Thursday, January 15

Kubemenda Mtoto???

Wadau hivi nani hajawahi kusikia kuhusu kubemenda mtoto huko majumbani na mitaani kwetu. Ila mimi pamoja na kupekua huku na kule wakati wa ujauzito na hadi leo sijawahi kuona kubemenda kwa nchi zilizoendelea. Hivi kweli kuna kitu kama kubemenda mtoto? Ni nini hasa? na inasababishwa na nini?

11 comments:

Anonymous said...

Nimesikia lkn nafikiri ni imani ya watu. (na unajua ukiamini kitu huwa kinatokea) manake ingekua kweli inge aply hata nchi za nje ya Africa

Anonymous said...

Hellow aunt, asante sana kwa mjadala wako wa jinsi yakubemenda mtoto itatusaidia wengi maana kila mtu anaongea lakwake, naomba wanawake wenzangu mtusaidie kuchambua mada hiyo ili wengine tunufaike nayo maana tupo njia panda hatujui ukweli ni upi. Mama Kelvin

Anonymous said...

MIMI SIONO SABABU YA WATU KUBEMENDA WATOTO NI UPUUZI TU WA KUWAHI MAPENZI BILA USTAARABU TCHAO BABA WA WENGI.

Anonymous said...

kubemenda nfiyo nini tenaaa jamani?

Anonymous said...

hakuna kitu km icho,ukweli ni imani na ukiamini inatokea.nchi za wenzetu mbona hatujaona hivo vitu?alafu nyumbani(TZ)eti km mtoto kabemendwa basi dawa ni kila asubui baba akiamka awe anampigampiga mtoto mgongoni na uume wake.Mh kweli imani yako ndio itakuponya

Anonymous said...

Hi, Mimi binafsi siamini kama kuna kitu kama hicho, kwani ata nchi za wenzetu sijawahi kusikia, pili ata kiutaalamu pia hakuna. Wale wajuzi tunaomba ufafanuzi ili nasi tusiojua tupate elimu hiyo.

Anonymous said...

wat is kubemenda to start with?
mother of one

Anonymous said...

Wanasema kubembenda ni labda either baba au mama ana-cheat nje na inapelekea mtoto anakuwa na makuzi dhaifu .labda anachelewa kukua,kusimama,anakuwa legelege au anaharisha sana

wengine kubemenda ni kufanya mapenzi na bila kujisafisha inatoke aunamkamata mtoto na mwili mchafu bila kuoga au kujisafisha. Au mnalala pamoja na mtoto sasa lile joto na hewa za wazazi zinamsumbua mtoto
HIVYO NDO NINAVYOELEWA KWA UPEO WANGU MDOGO

Anonymous said...

MMH UPUUZI MTUPU, THANKS KWA HUO MJADALA MANA USWAZI KUNA MAMBO, WE MTU KUFANYA MAPENZI NA KUMSHIKA MTOTO AKADHOOFU KIAFYA WAPI NA WAPI, CONNECTION IKO WAPI HAPO KISAYANSI?????????????

KUNA WATU KIBAO WANABIA CHAFU NA WANAO AFYA IPO, KINA MAMA LISHENI WATOTO VIZURI, NA HAKIKISHA HOUSEGIRL NAE ANAHUDUMIA MTOTO SIO UKIENDA JOB NA YEYE KIGUU NA NJIA BADALA YA KULISHA MTOTO, ALAFU UNASEMA MTOTO KABEMENDWA MMMMMMH HATA NENO LENYEWE KUBEMENDA LINABOAH AAAARGH!

Anonymous said...

Nadhani ni old wives tales ili kuzuia watu wasi-cheat wakiwa na mtoto mchanga nyumbani, na badala yake ku concentrate na kumlea mtoto.

Anonymous said...

Nakubaliana na anonimous number 8, ".....joto linamzuru mtoto....."