Wednesday, January 14

Ubatizo- Glory Moshi

Hayo mapambo sio harusi jamani, msije mkadhani nimeanza kupost picha za harusi bure, ni ubatizo wa mtoto Glory Moshi (mtoto wa Jacquline Moshi) aliyebatizwa kanisa la Mt Anuarite (Makuburi RC). sherehe hii ilifanyika nyumbani kwa bibi yake, Ubungo River Side, na amini usiamini, bibi huyo huyo ndie aliyefanya mapambo hayo ya kufa mtu!







3 comments:

Faustine said...

Naona siku hizi sherehe za ubatizo,komunio ya kwanza, kipaimara zimekuwa sio shughuli za familia, bali zimegeuka kuwa ni shughuli za jamii.
Cha kusikitisha zaidi watu wanachangishwa ili kufanikisha shughuli hizi.
Mimi nina mtazamo tofauti na baadhi ya wanajamii kuhusiana na hili, ingawa najua kuwa watu wanatumia nafasi kama hizi kuonyesha ufahari na "maendeleo" waliokuwa nayo.
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/

Anonymous said...

Naungana na wewe ndugu faustin,tena inasikitisha sana,unakuta wazazi wanamfanyia mtoto kipaimara au ubatizo wanapeleka sherehe ukumbini tena baa,watu wanakunywa na kulewa kupita kiasi,sasa hawa watoto wetu tunawafundisha nini?jamani enyi wakristo,yaani watoto/wana wa YESU yatupasa kuwalea watoto katika maadili ya dini zetu jamani,tumwogope Mungu,maana mbegu za ulevi tunaanza kuzipandikiza kwa watoto wetu sisi wenyewe,mtoto akija kuwa chapombe/mlevi tunasema jamani huyo mtoto ee Mungu nimekukosea nini mbona mwanangu ni mlevi hivi!kumbe nyie wenyewe mlimkabidhi kwenye kundi la walevi wakati mnambatiza/pata kipaimara.
Mtoto akipata kipaimara inamaana amekuwa kipa mzuri wa kudaga magoli ya shetani,matokeo yake anapigwa mabao kibao na shetani,tuwasaidie watoto wetu jamani wasije potelea kwa shetani,mara nyingi ulevi unamshawishi mtu kufanya mambo mabaya.Sherehe ya mtoto inapendeza ikifanyiwa nyumbani,tena kuwe na soft drinks tu,ndio toto part yenyewe,soda,juice,biskuit etc.Kwa kweli ninamengi ila muda umenibana,kesho ee!
ILA UBATIZO ULIKUWA SAFI,NA NI HOME NIMEPENDA UTUNDU WA BIBI MTU,KAJIPAMBIA SAFI,HALAFU HOME,sijui na bia zilikuwepo au la!maana baby mwenyewe bado mdogo wala haelewi kinachoendelea maskini,mwee,Mungu akukuze mwanangu,natamani kweli mtoto tena na kike kama huyu!

Anonymous said...

mi sina tatizo na mtu kafanya sherehe kubwa, pesa yako ila tu usichangishe watu kwajili ya ubatizo wala kipaimara, na kupeleka ukumbini sio hoja mana wengine wanakaa uswahilini, hata baraza hamna, ila tu kwa pesa yako

na vinyaji viwe soft drinks, si sherehe ya mtoto jamani, alikeni watoto wenzie waje wajumuike nae, sio watu wazima na nuksi zao