Friday, March 27

Lishe ya Mtoto Baada ya Maziwa- Ratiba ya Chakula

Ratiba ya Kumlisha Mtoto
Anza kumpa mtoto chakula cha nyongeza anapotimiza miezi 6
Nini: Uji au chakula kilichopondwa au kusagwa vizuri
Mara ngapi: Mara 2 kila siku
Kiasi gani: Mlishe vijiko vya chakula 2-3 kila mlo
Umri wa miezi 7 – 8
Nini: Chakula kilichopondwa
Mara ngapi: Mara tatu kwa siku
Kiasi gani: Mlishe theluthi mbili (2/3) ya kikombe kila mlo (kikombe 1=mls 250)
Umri wa miezi 9 – 12
Nini: Chakula kilichokatwa vipande vidogo vidogo au kilichopondwa na vile ambavyo mtoto anaweza kushika mwenyewe.
Mara ngapi: Mara 3 kila siku pamoja na asusa moja.
Kiasi gani: Mlishe robo tatu (3/4) ya kikombe kila mlo (kikombe 1=mls 250)
Umri wa miezi 12 – 24
Nini: Vyakula vinavyoliwa na familia, vikatwekatwe au kuponda kama inahitajika.
Mara ngapi: Mara 3 kila siku pamoja na asusa mbili
Kiasi gani: Mlishe kikombe kilichojaa kila mlo (kikombe 1=mls 250)

Xchyler’s Experience
Ratiba ya X ya sasa hivi:
Saa 12 asubuhi: akiamka tu, chupa moja ya maziwa, anaimaliza yote bila ubishi, lakini huku nacheza nae.
Saa tatu asubuhi: Uji kibakuli kimoja (vile vibakuli vyake vinasaidia kujua as akiongeza mlo watu wote mnajua sasa hivi uji ufika sehemu flani ya kibakuli).
Hapa kati:maziwa na juisi.
Saa saba mchana: mchanganyiko wake, kama leo ni wa viazi, kesho ni ndizi, pia kibakuli kimoja. Tulitaka kumuanzishia ugali, halafu hiki awe anakula jioni, kagoma kabisaaa, hata Bibi starring kamshindwa.
Hapa kati:tunda na maziwa na supu na juisi.
Saa kumi na moja jioni: uji tena, kibakuli kimoja.
Hapa kati: maziwa na kipapatio cha kuku, kile kipande kabla ya kipapatio, anapenda sana kuku. Ukitaka atulie mpe kuku tu!
Saa mbili usiku: siku hizi ubwabwa, uliochanganywa na maziwa.
Then kuoga, maziwa kidogo afu kulala. Hadi kesho asubuhi tena.

NB: - Maji muhimu kila baada ya mlo.
- X anamaliza lita moja ya maziwa (anatumia maziwa ya ng’ombe siku hizi, mama yake sina maziwa tena) kila siku.
- Maziwa ni muhimu sana kwa mtoto, mimi ndio yanamwamsha mwanangu kila asubuhi wataalam wanashauri hadi atakapofikisha miaka miwili, haijalishi ni maziwa gani, kama unanyonyesha mnyonyeshe, kama ni ya kopo haya, kama ya ng’ombe twende kazi. Hivyo vyakula vyote havi-replace maziwa.

2 comments:

Unknown said...

thanks a lot jiang kwa msaada huu. mimi mwanangu alikuwa anapenda sana maziwa ila tangu afikishe miez 22 hamu ya maziwa imempungua sana sasa sijui ni kwasababu anakula vitu vingi maana hakuna chakula ambacho hali. Nifanyeje ili awe anakunywa maziwa kama zamani maana alikuwa anamaliza ml 250 sasa anakunywa ml 150 tu.
thanks
magreth
http://womenofchrist.wordpress.com/

Anonymous said...

Mama X mwanao anapiga menu sana bwana angalia asipate obesity!